باب فضل البكاء من خشية الله تَعَالَى وشوقاً إِليه
وعن أنس – رضي الله عنه -، قَالَ: قَالَ أَبو بكر لِعُمَرَ، – رضي الله عنهما -، بعد وفاة رسول الله – صلى الله عليه وسلم -: انْطَلِقْ بِنَا إِلى أُمِّ أيْمَنَ – رضي الله عنها – نَزورُهَا، كَمَا كَانَ رسول الله – صلى الله عليه وسلم – يَزُورُها، فَلَمَّا انْتَهَيَا إِلَيْهَا بَكَتْ، فقالا لها: مَا يُبْكِيكِ؟ أمَا تَعْلَمِينَ أنَّ مَا عِنْدَ الله تَعَالَى خَيرٌ لرسولِ الله – صلى الله عليه وسلم – ! قالت: مَا أبْكِي أَنْ لاَ أَكُونَ أَعْلَمُ أنَّ مَا عِنْدَ اللهِ خَيْرٌ لرسولِ الله – صلى الله عليه وسلم -، وَلكِنِّي أبكِي أَنَّ الْوَحْيَ قَد انْقَطَعَ مِنَ السَّمَاءِ؛ فَهَيَّجَتْهُما عَلَى البُكَاءِ، فَجَعَلا يَبْكِيَانِ مَعَهَا. رواه مسلم،
وقد سبق في بابِ زِيارَةِ أهلِ الخَيْرِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka Anas (Radhi za Allah ziwe juu yake) amehadithia: “Abûbakar alimwambia ‘Umar (Radhi za Allah ziwe juu yake) baada ya Mtume ﷺ kuondoka duniani: “Tukamtembelee Ummu Ayman (Radhi za Allah ziwe juu yake) kama alivyokuwa Mtume ﷺ akimtembelea.” Walipofika kwake, (Ummu Ayman) alilia. Wakamwuliza: “Jambo gani likulizalo, kwani hujui kuwa lililo kwa Allâh ndio kheri kwa Mtume ﷺ ” Akasema: “Mimi silii kwamba sijui kuwa lililo kwa Allâh ndio kheri kwa Mtume ﷺ , lakini nalia kwa kuwa Wahyi umekatika (kuja) kutoka mbinguni.” Akawachochea kwa kilio, nao wakawa wanalia pamoja naye.” [ Imepokewa na Muslim. ]
Imetangulia katika Mlango wa kuwatembelea watu wa kheri.