باب فضل البكاء من خشية الله تَعَالَى وشوقاً إِليه
وعن أَبي هريرة – رضي الله عنه -، قَالَ: قَالَ رسول الله – صلى الله عليه وسلم -: {سَبْعَةٌ يُظِلُّهُمُ اللهُ في ظِلِّهِ يَوْمَ لا ظِلَّ إِلاَّ ظِلُّهُ: إمَامٌ عَادِلٌ، وَشَابٌ نَشَأَ فِي عِبَادَةِ اللهِ تَعَالَى، وَرَجُلٌ قَلْبُهُ مُعَلَّقٌ بِالمَسَاجِدِ، وَرَجُلاَنِ تَحَابّا في الله اجْتَمَعَا عَلَيْهِ وتَفَرَّقَا عَلَيْهِ، وَرَجُلٌ دَعَتْهُ امْرَأَةٌ ذَاتُ مَنْصِبٍ وَجَمَالٍ، فَقال: إنِّي أَخَافُ الله، وَرَجُلٌ تَصَدَّقَ بِصَدَقَةٍ فَأخْفَاهَا حَتَّى لاَ تَعْلَمَ شِمَالُه مَا تُنْفِقُ يَمِينُهُ، وَرَجُلٌ ذَكَرَ الله خَالِياً ففاضت عَيْنَاهُ} متفقٌ عَلَيْهِ.
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka Abû Huraira (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Mtume ﷺ amesema: [Watu saba, Allâh Atawafunika katika kivuli Chake siku ambayo hakutakuwa na kivuli ispokuwa kivuli Chake: Kiongozi mwadilifu, kijana aliekulia katika kumwabudu Mwenyezi Mungu Aliyeshinda na Kutukuka, mtu ambaye moyo wake umefungamana na Misikiti, watu wawili waliopendana kwa ajili ya Allâh waliojumuika kwa ajili Yake na wakafarikiana kwa ajili Yake, mtu aliyeitwa na mwanamke mwenye sharafu (cheo) na uzuri, akamwambia: Mimi namuogopa Allâh, mtu alietoa sadaka kwa kuficha hata mkono wake wa kushoto usijue kilichotoa mkono wake wa kulia na mtu aliemtaja Allâh faraghani macho yake yakabubujikwa machozi.] [ Wameafikiana Bukhari na Muslim.]