باب الخوف
عن ابن مسعود – رضي الله عنه -، قَالَ: حدثنا رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم – وَهُوَ الصادق المصدوق: {إنَّ أحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ في بَطْنِ أُمِّهِ أربَعِينَ يَوماً نُطْفَةً، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذلِكَ، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذلِكَ، ثُمَّ يُرْسَلُ المَلَكُ، فَيَنْفُخُ فِيهِ الرُّوحَ، وَيُؤْمَرُ بِأرْبَعِ كَلِمَاتٍ: بِكَتْبِ رِزْقِهِ وَأجَلِهِ وَعَمَلِهِ وَشَقِيٌّ أَوْ سَعِيدٌ. فَوَالَّذِي لا إلهَ غَيْرُهُ إنَّ أحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أهْلِ الجَنَّةِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وبيْنَهَا إلاَّ ذِرَاعٌ فَيَسْبِقُ عَلَيهِ الكِتَابُ، فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أهْلِ النَّارِ فَيدْخُلُهَا، وَإنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أهْلِ النَّارِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلاَّ ذراعٌ، فَيَسْبِقُ عَلَيهِ الكِتَابُ فَيعْمَلُ بِعَمَلِ أهْلِ الجَنَّةِ فَيَدْخُلُهَا} مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa Abdullâh bin Masûd (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Mtume ﷺ alituhadithia – naye ndiye mkweli mwenye kusadikiwa: [Hakika kila mmoja wenu hukusanywa umbile lake katika kizazi cha mama yake (mchanganyiko wa mbegu ya uzazi ya mwanamume na mwanamke) kwa muda wa siku arubaini likawa ni tone la manii, kisha huwa kipande cha damu kwa muda kama huo, kisha huwa kipande cha nyama kwa muda kama huo, kisha hutumwa Malaika akampulizia roho ndani yake, na akaamrishwa mambo manne: kuandika riziki yake, muda wa kuishi kwake, amali yake na kama ni mwema au ni muovu. Naapa kwa Ambaye hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki ila ni Yeye, hakika mmoja wenu huja akatenda amali ya watu wa Peponi, mpaka ikawa hakuna baina yake na Pepo ila dhiraa, akatanguliwa na aliloandikiwa, akafanya amali ya watu wa motoni, akaingia motoni. Na mmoja wenu huja akafanya amali ya watu wa motoni mpaka ikawa hakuna baina yake na moto ila dhiraa, akatanguliwa na aliloandikiwa, akafanya amali ya watu wa Peponi, akaingia Peponi.] [ Wameafikiana Bukhari na Muslim. ]