0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

38 DUA YA MWENYE KUOGOPA DHULMA YA MWENYE KUTAWALA

KINGA YA MUISLAMU

اللهم رب السموات السبع ، ورب العرش العظيم ،كن لي جاراً من فلان بن فلان ، وأحزابه من خلائقك ؛ أن يفرط على أحد منهم أو يطغى ، عز جارك ،وجل ثناؤك ، ولا إله إلا أنت

 البخاري في الأدب المفرد برقم 707 وصححه الألباني

[Ewe Mwenyezi Mungu  Mola wa mbingu saba, na Mola wa arshi tukufu, kuwa mlinzi wangu kutokana na (fulani bin fulani ) na vikosi vyake miongoni mwa viumbe vyako, kwa kunisaliti mmoja miongoni  mwao, au kunifanyia uadui, amehishimiwa  mwenye kulinda, na zimetukuka sifa zako na hapana mola apasae kuabudiwa kwa uhaki ila Wewe.]        [Imepokewa na Bukhari katika kitabu cha Adabul-Mufrid na Kusahihishwa na Al-Baaniy.]

الله أكبر، الله أعز من خلقه جميعاً ، الله أعز مما أخاف وأحذر ،أعوذ بالله الذي لا إله إلا هو ، الممسك السموات السبع أن يقعن على الأرض إلا بإذنه ،من شر عبدك فلان ،وجنوده وأتباعه وأشياعه ، من الجن والأنس ، اللهم كن لي جاراً من شرهم ، جل ثناؤك وعز جارك ، وتبارك اسمك ، ولا إله غيرك    ثلاث مرات

 البخاري في الأدب المفرد برقم 708 وصححه الألباني

[Mwenyezi Mungu  ni mkubwa, Mwenyezi Mungu  ni mwenye nguvu (cheo) kuliko viumbe vyake vyote, Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu, kuliko kila nikiogopacho nakujihadhari, najikinga na Mwenyezi Mungu  ambae hapana mola ila yeye tuu, ambae ameshikilia mbingu saba ili zisiangukie ardhi ila kwa idhini yake, kutokana na shari ya mja wako (fulani)  na majeshi yake, na wanaemfuata, na wafuasi wake miongoni mwa majini na watu.  Ewe Mwenyezi Mungu  kuwa mlinzi wangu kutokana na shari yao.  Zimetukuka  sifa zako na umehishimika ulinzi wako na limetakasika jina lako, na hapana apasae kuabudiwa kwa uhaki asie kuwa Wewe.]    mara tatu   [Imepokewa na Bukhari katika kitabu cha Adabul-Mufrid na kusahihishwa na Al-Baaniy.]

DUA YA MWENYE KUOGOPA DHULMA YA MWENYE KUTAWALA

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.