باب زيارة أهل الخير ومجالستهم وصحبتهم ومحبتهم وطلب زيارتهم والدعاء منهم وزيارة المواضع الفاضلة
وعن أَبي هريرة – رضي الله عنه -، عن النَّبيِّ – صلى الله عليه وسلم -: {أنَّ رَجُلاً زَارَ أَخَاً لَهُ في قَريَة أُخْرَى، فَأرْصَدَ الله تَعَالَى عَلَى مَدْرَجَتِهِ مَلَكاً، فَلَمَّا أتَى عَلَيهِ، قَالَ: أيْنَ تُريدُ؟ قَالَ: أُريدُ أخاً لي في هذِهِ القَريَةِ. قَالَ: هَلْ لَكَ عَلَيهِ مِنْ نِعْمَة تَرُبُّهَا عَلَيهِ؟ قَالَ: لا، غَيْرَ أنِّي أحْبَبْتُهُ في الله تَعَالَى، قَالَ: فإنِّي رَسُول الله إلَيْكَ بَأنَّ الله قَدْ أَحَبَّكَ كَمَا أحْبَبْتَهُ فِيهِ} رواه مسلم
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa Abû Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake amesimulia: “Mtume ﷺ amesimulia: [Mtu mmoja alimzuru nduguye (kwa Uislamu) katika kijiji kingine. Allâh Akamuwakilishia Malaika wa kumlinda njiani mwake. Alipomwendea, alimwuliza: Waelekea wapi? Akamjibu: Naenda kwa ndugu yangu katika kijiji hiki. Akamwuliza: Una neema fulani unayoisimamia na kujipatia maslahi? Akamjibu: Hapana. Ela mimi nimempenda kwa ajili ya Allâh. Akamwambia; Mimi ni Mjumbe wa Allâh nilietumwa kwako (nikupe bishara) kwamba Allâh Amekupenda kama ulivyompenda kwa ajili Yake. ] [Imepokewa na Muslim.]