باب توقير العلماء والكبار وأهل الفضل وتقديمهم عَلَى غيرهم ورفع مجالسهم وإظهار مرتبتهم
وعن ابن عباس – رضي الله عنهما -، قَالَ: قَدِمَ عُيَيْنَةُ بنُ حِصْن، فَنَزَلَ عَلَى ابْنِ أخِيهِ الحُرِّ بنِ قَيسٍ، وَكَانَ مِنَ النَّفَرِ الَّذِينَ يُدْنِيهِمْ عُمرُ – رضي الله عنه -، وَكَانَ القُرَّاءُ أصْحَاب مَجْلِس عُمَرَ وَمُشاوَرَتِهِ، كُهُولاً كاَنُوا أَوْ شُبَّاناً، فَقَالَ عُيَيْنَةُ لابْنِ أخيهِ: يَا ابْنَ أخِي، لَكَ وَجْهٌ عِنْدَ هَذَا الأمِيرِ، فَاسْتَأذِنْ لِي عَلَيهِ، فاسْتَأذَن له، فَإذِنَ لَهُ عُمَرُ – رضي الله عنه -، فَلَمَّا دَخَلَ قَالَ: هِي يَا ابنَ الخَطَّابِ، فَواللهِ مَا تُعْطِينَا الْجَزْلَ، وَلا تَحْكُمُ فِينَا بالعَدْلِ، فَغَضِبَ عُمَرُ – رضي الله عنه – حَتَّى هَمَّ أنْ يُوقِعَ بِهِ، فَقَالَ لَهُ الحُرُّ: يَا أميرَ المُؤْمِنينَ، إنَّ الله تَعَالَى قَالَ لِنَبيِّهِ – صلى الله عليه وسلم -: ﴿خُذِ الْعَفْوَ وَأْمُرْ بِالْعُرْفِ وَأَعْرِضْ عَنِ الْجَاهِلِينَ﴾ وَإنَّ هَذَا مِنَ الجَاهِلِينَ. واللهِ مَا جَاوَزَهاَ عُمَرُ حِينَ تَلاَهَا عليه، وكَانَ وَقَّافاً عِنْدَ كِتَابِ اللهِ تَعَالَى. رواه البخاري
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka ‘Abdullâh bin ‘Abbâs Radhi za Allah ziwe juu yao amesema: “‘Uyainah bin Hisni alikuja kutoka safari, akashukia kwa mpwa wake al-Hurri bin Qais, naye alikuwa ni katika watu ambao ‘Umar alikuwa akiwakurubisha karibu naye, wanavyuoni walikuwa ndio watu wa majilisi ya ‘Umar Radhi za Allah ziwe juu yake na katika washauri wake; wawe ni wazee au vijana. ‘Uyainah akamwambia mpwa wake: “Ee mpwa wangu, wewe una wajihi kwa huyu Amiri, basi niombee idhini (niingie kwake).” Akamwombea idhini, ‘Umar akamruhusu. Alipoingia alisema: “Hi! Ee mwana wa Khattâb! Wallahi hutupi kitu kingi, wala huhukumu kwa uadilifu kati yetu.” ‘Umar Radhi za Allah ziwe juu yake akakasirika hata akataka kumuadhibu. al-Hurru akamwambia: “Ee Amiri wa Waumini, hakika Allâh Alimwambie Mtume Wake: [Shikamana na kusamehe, amrisha mema na wapuze masafihi.] [7: 199] Hakika huyu ni katika masafihi. Basi Wallahi ‘Umar hakumfanya kitu al-Hurru alipoisoma Aya hii. Alikuwa ‘Umar amesimama wima katika Kitabu cha Allâh.” [Imepokewa na Bukhari.]