BUSTANI YA WATU WEMA
وعن ابن عمر – رضي الله عنهما -، قَالَ: سمعت رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -، يقول: {كُلُّكُمْ رَاعٍ، وَكُلُّكُمْ مسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتهِ: الإمَامُ رَاعٍ وَمَسْؤولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ، والرَّجُلُ رَاعٍ في أهْلِهِ وَمَسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ، وَالمَرْأةُ رَاعِيَةٌ في بيْتِ زَوْجِهَا وَمَسْؤُولَةٌ عَنْ رَعِيَّتِهَا، وَالخَادِمُ رَاعٍ في مَالِ سَيِّدِهِ وَمَسؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ، فَكُلُّكُمْ رَاعٍ وَمَسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ} مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa Abdullâh bin ‘Umar Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: “Nilimsikia Mtume ﷺ akisema: “Nyote ni wachunga na kila mmoja wenu ataulizwa kuhusu alichokichunga. Kiongozi ni mchunga, na ataulizwa kuhusu alichokichunga, mume ni mchunga juu ya mkewe, na ataulizwa kuhusu alichokichunga, mke ni mchunga juu ya nyumba ya mumewe na ataulizwa kuhusu alichokichunga, na mtumishi ni mchunga juu ya mali ya bwana wake na ataulizwa kuhusu alichokichunga; kwa hivyo nyote ni wachunga na kila mmoja wenu ataulizwa kuhusu alichokichunga. [Wameafikiana Bukhari na Muslim].