0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

259. Riyadhu Swalihina Mlango wa Ubora wa Waislamu wanyonge Hadithi 08


BUSTANI YA WATU WEMA


وعن أَبي هريرة رضي اللَّه عنه عن النبي صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال : « لَمْ يَتَكَلَّمْ فِي المَهْدِ إِلاَّ ثَلاثَةٌ : عِيسى ابْنُ مرْيَمَ ، وصَاحِب جُرَيْجٍ ، وكَانَ جُرَيْجٌ رَجُلاً عَابِداً ، فَاتَّخَذَ صَوْمَعةً فكانَ فِيهَا ، فَأَتَتْهُ أُمُّهُ وَهَو يُصلي فَقَالَتْ : يا جُرَيْجُ ، فقال : يَارَبِّ أُمِّي وَصَلاتِي فَأَقْبلَ عَلَى صلاتِهِ فَانْصرفَتْ فَلَمَّا كَانَ مِنَ الْغَدِ أَتَتْهُ وهُو يُصَلِّي ، فقَالَتْ : يَا جُرَيْجُ ، فقال : أَيْ رَبِّ أُمِّي وَصَلاتِي . فَأَقْبَلَ عَلَى صَلاتِهِ ، فَلَمَّا كَانَ مِنَ الْغَد أَتَتْهُ وَهُو يُصَلِّي فَقَالَتْ : يَا جُرَيْجُ فقال : أَيْ رَبِّ أُمِّي وَصَلاتِي ، فَأَقْبَلَ عَلَى صَلاتِهِ ، فَقَالَتْ : اللَّهُمَّ لا تُمِتْه حَتَّى ينْظُرَ إِلَى وُجُوه المومِسَاتِ . فَتَذَاكَّرَ بَنُو إِسْرائِيلَ جُريْجاً وَعِبَادَتهُ ، وَكَانَتِ امْرَأَةٌ بغِيٌّ يُتَمَثَّلُ بِحُسْنِهَا ، فَقَالَتْ : إِنْ شِئْتُمْ لأَفْتِنَنَّهُ ، فتعرَّضَتْ لَهُ ، فَلَمْ يلْتَفِتْ إِلَيْهَا ، فَأَتتْ رَاعِياً كَانَ يَأَوي إِلَى صوْمعَتِهِ ، فَأَمْكنَتْهُ مِنْ نفسها فَوقَع علَيْهَا . فَحملَتْ ، فَلَمَّا وَلدتْ قَالَتْ : هُوَ جُرَيْجٌ ، فَأَتَوْهُ فاسْتنزلُوه وهدَمُوا صوْمعَتَهُ ، وَجَعَلُوا يَضْرِبُونهُ ، فقال : ما شَأْنُكُمْ ؟ قالوا: زَنَيْتَ بِهذِهِ الْبغِيِّ فَولَدتْ مِنْك . قال : أَيْنَ الصَّبِيُّ ؟ فَجاءَوا بِهِ فقال : دَعُونِي حَتَّى أُصَلِّي فَصلىَّ ، فَلَمَّا انْصَرَفَ أَتَى الصَّبِيَّ فَطَعنَ فِي بطْنِهِ وقالَ : يا غُلامُ مَنْ أَبُوكَ ؟ قال : فُلانٌ الرَّاعِي ، فَأَقْبلُوا علَى جُرَيْجُ يُقَبِّلُونَهُ وَيَتَمَسَّحُونَ بِهِ وقَالُوا : نَبْنِي لَكَ صوْمَعَتَكَ مِنْ ذَهَبٍ قال : لا، أَعيدُوهَا مِنْ طِينٍ كَمَا كَانَتْ ، فَفَعَلُوا . وَبيْنَا صَبِيٌّ يرْضعُ مِنْ أُمِّهِ ، فَمَرَّ رَجُلٌ رَاكِبٌ عَلَى دابَّةٍ فَارِهَةٍ وَشَارةٍ حَسَنَةٍ فَقالت أُمُّهُ : اللَّهُمَّ اجْعَل ابْنِي مثْلَ هَذَا ، فَتَرَكَ الثَّدْيَ وَأَقْبَلَ إِلَيْهِ فَنَظَرَ إِلَيْهِ فقال : اللَّهُمَّ لا تَجْعَلْنِي مِثْلهُ ، ثُمَّ أَقَبَلَ عَلَى ثَدْيِهِ فَجَعْلَ يَرْتَضِعُ» فَكَأَنِّي أَنْظُرُ إِلَى رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم وَهُوَ يحْكِي ارْتِضَاعَهُ بِأُصْبُعِه السَّبَّابةِ فِي فِيهِ ، فَجَعلَ يَمُصُّهَا، قال : « وَمَرُّوا بِجَارِيَةٍ وَهُمْ يَضْرِبُونَهَا، وَيَقُولُونَ : زَنَيْتِ سَرَقْتِ ، وَهِي تَقُولُ : حَسْبِيَ اللَّهُ وَنِعْمَ الْوكِيلُ . فقالت أُمُّهُ : اللَّهُمَّ لا تَجْعَلْ ابْنِي مِثْلَهَا ، فَتَركَ الرِّضَاعَ وَنَظَرَ إِلَيْهَا فقال : اللَّهُمَّ اجْعَلْنِي مِثْلَهَا ، فَهُنالِكَ تَرَاجَعَا الحَدِيثِ فقالَت : مَرَّ رَجُلٌ حَسنُ الهَيْئَةِ فَقُلْتُ : اللَّهُمَّ اجْعَلْ ابْنِي مِثْلَهُ فَقُلْتَ : اللَّهُمَّ لا تَجْعَلنِي مِثْلَهُ ، وَمَرُّوا بِهَذِهِ الأَمَةِ وَهُم يَضْربُونَهُا وَيَقُولُونَ : زَنَيْتِ سَرَقْتِ ، فَقُلْتُ : اللَّهُمَّ لا تَجْعَلْ ابْنِي مِثْلَهَا فَقُلْتَ : اللَّهُمَّ اجعَلْنِي مِثْلَهَا ؟، قَالَ : إِنَّ ذلِكَ الرَّجُلَ كَانَ جَبَّاراً فَقُلت : اللَّهُمَّ لا تجْعَلْنِي مِثْلَهُ ، وإِنَّ هَذِهِ يَقُولُونَ لها زَنَيْتِ ، وَلَمْ تَزْنِ ، وَسَرقْت ، وَلَمْ تَسْرِقْ ، فَقُلْتُ : اللَّهُمَّ اجْعَلْنِي مِثْلَهَا »   متفق عليه.
« والمُومِسَاتُ » : بضَمِّ الميم الأُولَى ، وإِسكان الواو وكسر الميم الثانيةِ وبالسين المهملَةِ وهُنَّ الزَّوانِي . والمُومِسةُ : الزانية . وقوله : « دابَّةً فَارِهَة » بِالْفَاءِ : أَي حاذِقَةٌ نَفِيسةٌ . «الشَّارَةُ » بِالشِّينِ المعْجمةِ وتَخْفيفِ الرَّاءِ : وَهِي الجمالُ الظَّاهِرُ فِي الهيْئَةِ والملْبسِ . ومعْنى وصل « ترَاجعا الحدِيث » أَيْ : حدَّثَتِ الصَّبِي وحدَّثَهَا ،


Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurairah Radhi za Allah ziwe juu yake , kutoka kwa Mtume ﷺ amesema: [Hawajazungumza katika kitanda cho utoto au katika utoto isipokua watoto watatu : Issa Bin Maryam, na rafiki wa Jureyj, na alikua Jureyj mtu wa kufanya ibada, basi akijijengea kijumba chake cha ibada akawa anaishi ndani yake, siku moja mama yake akamjia akiwa anaswali akasema: (akamitwa) Ewe Jureyj, akasema: Ewe Mola wangu Mama yangu na swala yangu, (niafanyeje ni endelee na Swala ama nimuitkie mamangu) basi akaendelea na Swala yake basi mama yake akaondoka ilipofika kesho yake mama yake akamjia akiwa anaswali, akasema: (akamitwa) Ewe Jureyj, akasema: Ewe Mola wangu mama yangu na Swala yangu. Basi akaendelea na Swala yake, ilipofika kesho yake mama yake alimjia akiwa anaswali akasema : Ewe Jureyj akasema: Ewe Mola wangu mama yangu au swala yangu, akaendelea na Swala yake, mama yake akasema: Ewe Mola usimfishe huyu mpaka aangalie nyuso za makahaba. basi wana waisraeli wakawa wanatajiana Jureyja na ibada zake, na kulikua na mwanamke kahaba anapigiwa mfano kwa uzuri wake, akasema: mkipenda nitamfitinisha, mwanamke yule akajitokeza kwa Jureyj , lakini Jureyj hakumuangalia wala kushughulika nae, mwanamke yule akaenda kwa mchunga wanyama ambae alikua anaishi katika kijumba chake akajirahisisha kwake yule mchunga wanyama akafanya nae tendo la ndoa. Akabeba uja uzito, alipojifungua (yule kahaba) akasema: Ni Jureyj (aliyenipa huyu mtoto,) watu wakaenda kwa Jureyj wakamkamata na kuvunji kijumba chake cha ibada, na wakawa wanampiga, Jureyj akasema : Muna nini nyinyi ? Wakasema: umezini na huyu kahaba na amejifungua kutokana na mimba yako. jureyja akasema : Yuko wapi mtoto? wakamleta mtoto akasema: Niacheni mpaka niswali basi akaswali, alivyomaliza kuswali alienda kwa yule mtoto akamdunga tumboni kwake kisha akasema : Ewe kijana baba yako ni nani ? Yule mtoto akasema : jamaa fulani ambae ni mchungaji, basi wakamuendea Jureyja wakawa wanambusu na wanampapasa na wakasema: Tutakujengea kijumba chako cha ibada kutokana na dhahabu akasema: Hapana ‘ ijengeni tena kwa udongo kama ilivyokua basi wakafanya hivyo. Na wakati mmoja mtoto mchanga akiwa ananyonya katika ziwa la mama yake , akapita mtu mmoja akiwa juu ya kipando cha kifahari na muonekano mzuri mama yake akasema: Ewe Mwenyezi Mungu mjaalie mwanangu awe kama huyu, yule mtoto akaacha kunyonya titi la mama yake kisha akamuelekea yule mtu na Akamuangali kisha akasema: Ewe Mwenyezi Mungu usinijaalie kama yeye kisha akarudia titi lake akaendelea kunyonya}} kana kwamba namuona Mtume ﷺ na yeye anahadithia kunyonya kwake kwa kidole chake cha shahada katika mdomo wake akawa ananyonya hicho kidole chake akasema : {{walipita kwa kijakazi na watu wanampiga huku wakiwa wanasema : umezini umeiba, na yeye kijakazai anasema : Ananitosha Mwenyezi Mungu na yeye ndie mbora wa kutegemewa . Basi akasema mama yake: Ewe Mwenyezi Mungu usimjaalie mwanangu kama mwanamke huyu, mtoto akawacha kunyonya kisha akamuangalia mama yake kisha akasema: Ewe Mola nijaalie mfano wake, hapo wakahadithiana basi akasema yule mwanamke: Alipita mtu mmoja ambae alikua na muonekano mzuri basi nikasema: Ewe Allah Mjaalie mwanangu mfano wake basi nikasema : Ewe Allah usinijaalie mfano wake, na walipita kwa huyu kijakazi na wao wakiwa wanampiga huku wakiwa wanasema: Umezini umeiba, nikasema: Ewe Allah usimjaalie mwanangu mfano wake nikasema: Ewe Allah nijaalie mfano wake ?, Akasema: Hakika yule mtu alikua jabari na mjauri basi nikasema: Ewe Allah usinijaalie mfano wake, na huyu kijakazi wanamwambia umezini, na hakuzini, na umeimba, na hakuiba, basi nikasema: Ewe Allah nijaalie mfano wake}}
[Imepokelewa na Bukhary na Muslim.]


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.