BUSTANI YA WATU WEMA
وعن أَبي العباسِ سهلِ بنِ سعدٍ الساعِدِيِّ رضي اللَّه عنه قال : مرَّ رجُلٌ على النَبيِّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم فقالَ لرجُلٍ عِنْدهُ جالسٍ : « ما رَأَيُكَ فِي هَذَا ؟ » فقال : رَجُلٌ مِنْ أَشْرافِ النَّاسِ هذا وَاللَّهِ حَريٌّ إِنْ خَطَب أَنْ يُنْكَحَ وَإِنْ شَفَع أَنْ يُشَفَّعَ . فَسَكَتَ رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، ثُمَّ مَرَّ رَجُلٌ آخرُ ، فقال له رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : « مَا رأُيُكَ فِي هَذَا ؟ » فقال : يا رسولَ اللَّه هذا رَجُلٌ مِنْ فُقَرَاءِ الْمُسْلِمِينَ ، هذَا حريٌّ إِنْ خطَب أَنْ لا يُنْكَحَ ، وَإِنْ شَفَع أَنْ لا يُشَفَّعَ، وَإِنْ قَالَ أَنْ لا يُسْمع لِقَوْلِهِ . فقال رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : « هَذَا خَيْرٌ منْ مِلءِ الأَرْضِ مِثْلَ هذَا» متفقٌ عليه
Kutoka kwa Sahli bin Sa’ad Assaidy (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: Mtu mmoja alipita kwa Mtume wa Mungu ﷺ akamwambia mtu alieketi pamoja naye: [Nini maoni yako kuhusu mtu huyu?] Akasema: “Mtu huyu ni miongoni mwa watu watukufu, Wallahi huyu anastahiki akienda kuposa aozeshwe na akiombea akubaliwe ombi lake” Mtume ﷺ akanyamaza. Halafu akapita Mtu mwengine, Mtume ﷺ Akamuliza: [Nini maoni yako juu ya huyu?]
Akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu huyu ni mtu miongoni mwa Mafukara wa Waislamu huyu afaa akaenda kuposa asiozeshwe na akiombea asikubaliwe ombi lake na akisema neno lake lisisikizwe Mtume ﷺ Akasema: [Huyu ni bora kuliko yule (mtu wa kwanza) hata wakijaa katika Ardhi kama yeye] [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى