BUSTANI YA WATU WEMA
وعن أَبي العباس سهلِ بنِ سعدٍ السَّاعِدِيِّ رضي اللَّهُ عنه ، أَن رسولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم بلَغهُ أَنَّ بَني عَمْرِو بن عوْفٍ كان بيْنهُمْ شَرٌّ ، فَخَرَجَ رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يُصْلِحُ بَيْنَهمْ فِي أُنَاسٍ مَعَه ، فَحُبِسَ رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم وَحَانَتِ الصَّلاَةُ ، فَجَاءَ بِلالٌ إِلَى أَبي بَكْرٍ رضي اللَّه عنهما فقال : يَا أَبَا بَكْرٍ إِنَّ رسولَ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قَدْ حُبِسَ ، وَحَانَتِ الصَّلاةُ ، فَهَلْ لكَ أَنْ تَؤُمَّ النَّاس؟ قال : نَعَمْ إِنْ شِئْتَ ، فَأَقَامَ بِلالٌ الصَّلاةَ ، وَتقَدَّمَ أَبُو بَكْرٍ فَكَبَّرَ وكبَّرَ النَّاسُ، وَجَاءَ رسول اللَّه يمْشِي في الصُّفوفِ حتَّى قامَ في الصَّفِّ ، فَأَخَذَ النَّاسُ فِي التَّصْفِيقِ ، وكَانَ أَبُو بَكْر رضي اللَّه عنه لا يَلْتَفِتُ فِي صلاتِهِ، فَلَمَّا أَكَثَرَ النَّاسُ التَّصْفِيقَ الْتَفَتَ ، فَإِذَا رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، فَأَشَار إِلَيْهِ رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، فَرَفَعَ أَبْو بَكْر رضي اللَّه عنه يدَهُ فَحمِد اللَّه ، وَرَجَعَ القهقرى وَراءَهُ حَتَّى قَامَ فِي الصَّفِّ ، فَتَقدَّمَ رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، فَصَلَّى للنَّاسِ ، فَلَمَّا فرغَ أَقْبلَ عَلَى النَّاسِ فقال : « أَيُّهَا النَّاسُ مالَكُمْ حِين نَابَكُمْ شَيْءٌ في الصَّلاَةِ أَخذْتمْ فِي التَّصْفِيقِ ؟، إِنَّما التَّصْفِيقُ لِلنِّسَاءِ . منْ نَابُهُ شيءٌ فِي صلاتِهِ فَلْيَقلْ: سُبْحَانَ اللَّهِ ؟ فَإِنَّهُ لا يَسْمعُهُ أَحدٌ حِينَ يَقُولُ : سُبْحانَ اللَّهِ ، إِلاَّ الْتَفَتَ . يَا أَبَا بَكْرٍ : ما منعَك أَنْ تُصَلِّيَ بِالنَّاسِ حِينَ أَشرْتُ إِلَيْكَ ؟ » فقال أَبُو بكْر : مَا كَانَ ينبَغِي لابْنِ أَبي قُحافَةَ أَنْ يُصلِّيَ بِالنَّاسِ بَيْنَ يَدَيْ رسولِ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم . متفقٌ عليه
معنى « حُبِس » : أَمْسكُوهُ لِيُضيِّفُوه
Kutoka kwa Abi Abbas Sahl bin Said Assaidy radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehma na amani ziwe juu yake ilimfikia habari ya kwamba katika ukoo wa (Banii Amru bin Auf) baina yao kulikua na shari na ugomvi, basi akatoka Mtume ﷺ ili kusuluhisha baina yao akiwa na watu pamoja na yeye, akazuiliwa Mtume wa Mungu ﷺ (kwa ajili ya kuandaliwa) mpaka ukafika wakati wa Swala basi akaja Bilal (Radhi za Allah ziwe juu yake) kwa Abuu Bakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) akasema: Ewe Abuu Bakar hakika Mtume rehma na amani ziwe juu yake amezuiliwa, na wakati wa Swala umefika, jee unaonaje uwe Imam uwaswalishe watu? Akasema Abuu Bakar:Ndio ukitaka, basi Bilal akakimu Swala, na akatangulia Abuu Bakar akatoa Takbiira na watu pia wakatoa takbiira, na akaja Mtume wa Allah rehma na amani ziwe juu yake akiwa anatembea katika safu za watu mpaka akasimama katika safu fulani, basi watu wakaanza kupiga makofi, na alikua Abubakar radhi za Allah ziwe juu yake hageuki katika swala yake, lakini pindi watu walipozidisha kupiga makofi akageuka, hapo akamuona Mtume rehma na amani ziwe juu yake Mtume akamuashiria aendelee, basi Abubakar (radhi za Allah ziwe juu yake) akaenua mkono wake kisha akamhimidi Mwenyezi Mungu, kisha akarudi kinyume nyume nyuma yake mpaka akasimama katika safu, basi hapo Mtume rehma na amani ziwe juu yake akatangulia na akawaswalisha watu, alipomaliza Mtume kuswalisha akawaelekea watu kisha akasema: [Enyi watu mna nini nyinyi pale lilipowatatiza nyinyi jambo katika swala mukaanza kupiga makofi ? Kwa hakika makofi ni kwa ajili ya wanawake . Atakaepatwa na kitu katika swala yake basi na aseme : SUBHANALLAH ? Kwani hamsikii mtu yeyote anaposema: SUBHANALLAH . Isipokua atageuka. Ewe Abubakar kitu gani kumekuzuia kuwaswalisha watu pale nilipokuashiria uendelee ?] akasema Abuu Bakar : “haifai kwa kwa mtoto wa Abii Quhafah kuwaswalisha watu mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani ziwe juu yake “. [Imepokelewa na Bukhary na Muslim.]
Maana ya Mtume kuzuiwa ni kwamba walimzuia ili wamkaribishe.
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى