BUSTANI YA WATU WEMA
وعن ابن عمرَ رضي اللَّهُ عنهما أَن رسولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال : «المسلمُ أَخــو المسلم لا يَظلِمُه ولا يُسْلِمُهُ . ومَنْ كَانَ فِي حاجةِ أَخِيهِ كانَ اللَّهُ فِي حاجتِهِ، ومنْ فَرَّجَ عنْ مُسلمٍ كُرْبةً فَرَّجَ اللَّهُ عنه بها كُرْبةً من كُرَبِ يومَ القيامةِ ، ومن سَتَرَ مُسْلماً سَتَرَهُ اللَّهُ يَومَ الْقِيامَةِ » متفق عليه
Kutoka kwa Ibnu Umar (Radhi za Allah ziwe juu yao) Amesema kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ Amesema: [Muislamu ni ndugu yake Muislamu hamdhulumu wala hamsalimishi kwa Adui. Na mwenye (kumkidhia) Haja ndugu yake Mwenyezi Mungu atakuwa katika (kumkidhia) Haja yake, na mwenye kumfariji Muislamu kwa kumuondoshea shida Mwenyezi Mungu atamfariji na shida miongoni mwashida za siku ya Qiyama, na mwenye kumsitiri Muislamu Mwenyezi Mungu atamsitiri siku ya Qiyaam]
[Imepokewa na Bukhari na Muslim]
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله