0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

205. Riyadhu Swalihina Mlango wa Uharamu wa kudhulumu na Amri ya kurudisha Vilivyodhulumiwa Hadithi 03


BUSTANI YA WATU WEMA


1463655589


وعن ابن عمر رضي اللَّه عنهما قال : كُنَّا نَتحدَّثُ عَنْ حَجَّةِ الْوَدَاعِ ، وَالنَّبِيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم بَيْن أَظْهُرِنَا ، وَلاَ نَدْرِي مَا حَجَّةُ الْوداع ، حَتَّى حمِدَ اللَّه رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، وَأَثْنَى عَليْهِ ثُمَّ ذَكَر الْمسِيحَ الدَّجَالَ فَأَطْنَبَ في ذِكْرِهِ ، وَقَالَ : « ما بَعَثَ اللَّه مِنْ نَبيٍّ إلاَّ أَنْذَرَهُ أُمَّتهُ : أَنْذَرَهُ نوحٌ وَالنَّبِيُّون مِنْ بَعْدِهِ ، وَإنَّهُ إنْ يَخْرُجْ فِيكُمْ فما خفِيَ عَليْكُمْ مِنْ شَأْنِهِ فَلَيْسَ يَخْفِي عَلَيْكُمْ، إِنَّ رَبَّكُمْ لَيس بأَعْورَ ، وَإِنَّهُ أَعورُ عَيْن الْيُمْنَى ، كَأَنَّ عيْنَهُ عِنبَةٌ طَافِيَةٌ . ألا إن اللَّه حرَّم علَيْكُمْ دِمَاءَكُمْ وَأَمْوالكُمْ ، كَحُرْمَةِ يوْمكُمْ هذا ، في بلدِكُمْ هذا ، في شَهْرِكُم هذا ألاَ هل بلَّغْتُ ؟ » قَالُوا : نَعَمْ ، قال : « اللَّهُمَّ اشْهَدْ ثَلاثاً ويْلَكُمْ أَوْ : ويحكُمْ ، انظُرُوا: لا ترْجِعُوا بَعْدِي كُفَّاراً يضْرِبُ بَعْضُكُمْ رِقَابَ بَعْضِ »          رواه البخاري ، وروى مسلم بعضه


Kutoka kwa Ibn ‘Umar Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Tulikuwa tukizungumza (Hijjatul Wadaa’) Hijja ya kuaga  baina yetu wala hatujui nini Hijja ya kuaga mpaka Mtume ﷺ alipomuhimidi Mwenyezi Mungu (Subhaanahu Wa Ta’aalaa) na kumtukuza. Baada ya hapo akamtaja Masiyh Dajjaal na kuzungumza kwa kirefu. Kisha akasema: [Mwenyezi Mungu hakumtumila Nabii ila (Nabii hiyo) aliwatahadharisha Umma wake kuhusu yeye (Masih Ddajjaal). Nuh na Mitume waliokuja baada yake walionya kumhusu. Na hakika yeye atakapo miongoni mwenu, hataweza kujificha, ukweli wake hautafichika kwenu. Hakika Mola wenu si chogo, bali yeye (Masihi Ddajjaal) ni chogo jicho lake la kulia kama kwamba jicho lake ni zabibu iliyovimba. Tahadharini! Hakika Mwenyezi Mungu  (Subhaanahu Wa Ta’aalaa) Ametahadharisha kwenu damu zenu na mali yenu kama utukufu wa siku yenu hii (siku ya Hijja), katika mji wenu huu (yaani Makkah), katika mwezi wenu huu (Dhul Hijjah). Je, nimefikisha ujumbe? Wakasema (Maswahaba): Ndio. Akasema Mtume ﷺ: Ewe Mwenyezi Mungu ! Shuhudia – mara tatu. Ole wenu tizameni sana! Msirudi baada yangu makafiri mukawa baadhi yenu wanazipiga Shingo za baadhi yenu (mnauana).]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim amepokea baadhi yake]    


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله



Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.