0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

201. Riyadhu Swalihina Mlango wa Maamrisho ya kutekeleza Amana Hadithi 03

BUSTANI YA WATU WEMA


وعن حُذَيْفَةَ ، وَأَبي هريرة ، رضي اللَّه عنهما، قالا : قال رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : «يَجْمعُ اللَّه ، تَباركَ وَتَعَالَى ، النَّاسَ فَيُقُومُ الْمُؤمِنُونَ حَتَّى تَزْلفَ لَهُمُ الْجَنَّةُ ، فَيَأْتُونَ آدَمَ صلواتُ اللَّه عَلَيْهِ ، فَيَقُولُون : يَا أَبَانَا اسْتفْتحْ لَنَا الْجَنَّةَ ، فَيقُولُ : وهَلْ أَخْرجكُمْ مِنْ الْجنَّةِ إِلاَّ خَطِيئَةُ أَبِيكُمْ ، لَسْتُ بصاحبِ ذَلِكَ ، اذْهَبُوا إِلَى ابْنِي إبْراهِيمَ خَلِيل اللَّه ، قَالَ: فَيأتُونَ إبْرَاهِيمَ ، فيقُولُ إبْرَاهِيمُ : لَسْتُ بصَاحِبِ ذَلِك إِنَّمَا كُنْتُ خَلِيلاً مِنْ وَرَاءَ وراءَ ، اعْمَدُوا إِلَى مُوسَى الذي كَلَّمهُ اللَّه تَكْلِيماً ، فَيَأْتُونَ مُوسَى ، فيقُولُ : لسْتُ بِصَاحِب ذلكَ، اذْهَبُوا إِلَى عِيسى كَلِمَةِ اللَّه ورُوحِهِ فَيقُولُ عيسَى : لَسْتُ بِصَاحِبِ ذلكَ. فَيَأْتُونَ مُحَمَّداً صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، فَيَقُومُ فَيُؤْذَنُ لَهُ ، وَتُرْسَلُ الأَمانَةُ والرَّحِمُ فَيَقُومَان جنْبَتَي الصراطِ يَمِيناً وشِمالاً ، فيَمُرُّ أَوَّلُكُمْ كَالْبَرْقِ » قُلْتُ : بأَبِي وَأُمِّي ، أَيُّ شَيءٍ كَمَرِّ الْبَرْقِ ؟ قال : « أَلَمْ تَرَوْا كَيْفَ يمُرُّ ويَرْجعُ في طَرْفَةِ عَيْنٍ ؟ ثُمَّ كَمَرِّ الريحِ ثُمَّ كَمرِّ الطَّيْرِ ؟ وَأَشَدُّ الرِّجالِ تَجْرِي بهمْ أَعْمَالُهُمْ ، ونَبيُّكُمْ قَائِمٌ عَلَى الصرِّاطِ يَقُولُ : رَبِّ سَلِّمْ ، حَتَّى تَعْجِزَ أَعْمَالُ الْعَبَادِ ، حَتَّى يَجئَ الرَّجُلُ لا يَسْتَطِيعُ السَّيْرَ إلاَّ زَحْفاً ، وفِي حافَتَي الصرِّاطِ كَلالِيبُ مُعَلَّقَةٌ مَأْمُورَةٌ بأَخْذِ مَنْ أُمِرَتْ بِهِ ، فَمَخْدُوشٌ نَاجٍ وَمُكَرْدَسٌ في النَّارِ » وَالَّذِي نَفْسُ أَبِي هُرَيْرَةَ بِيَدِهِ إِنَّ قَعْرَ جَهنَّم لَسبْعُونَ خَريفاً . رواه مسلم


Kutoka kwa Hudhayfah na Abuu Hurayrah Radhi za Allah ziwe juu yao wamesema: amesema Mtume ﷺ: [Mwenyezi Mungu (Subhaanahu Wa Ta’aalaa) Atawakusanya watu. (siku ya Qiyama) Watasimama waumini mpaka watakuja karibu na Pepo, na hapo watamuendea Adam (‘Alayhis Salaam) na kumwambia: “Ewe baba yetu, tufungulie na sisi Pepo. Atasema: Je kuna jambo lililowatoa Peponi ila sikosa la baba yenu (ndio lililowatoa nyinyi katika Jannah). Mimi si mwenyewe wa jambo hilo, hivyo nendeni kwa mtoto wangu Ibrahim (‘Alayhis Salaam), kipenzi cha Mwenyezi Mungu (Subhaanahu Wa Ta’aalaa). Amasema: Watakwenda kwa Ibrahim (‘Alayhis Salaam), na watamwambia. Atasema: Mimi si mwenyewe wa jambo hilo, hakika mimi nilikuwa kipenzi tu na wala sina darja hiyo ya juu. Nendeni kwa Musa ambaye Allaah (Subhaanahu Wa Ta’aalaa) Alizungumza naye kwa uwazi kabisa. Watakuja kwa Musa (‘Alayhis Salaam), naye atasema: Mimi si mwenyewe wa jambo hilo. Nendeni kwa Issa (Alayhi Salaam) yeye ni kalima ya Mwenyezi Mungu na Roho yake Issa (alayhi Salaam) atasema: Mimi si mwenyewe wa jambo hilo Hapo watakuja kwa Muhammad ﷺ. Atasimama mbele ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu Wa Ta’aalaa) na atakubaliwa kuwatetea watu. Itatumwa Amana na kuunganisha kizazi, nazo zitasimama pembezoni mwa Swiraat (njia) kulia na kushoto. Wa mwanzo wenu watapita kama umeme. Nikasema: Baba yangu na mama yangu wawe fidia kwako unamaanisha nini? Akasema: “Huoni cheche za umeme zinazokwenda na kurudi katika kupepesa jicho? Kisha watapita kama upepo, kisha kama ndege, na wengine kwa kasi ya watu wanaokimbia, na tofauti hii (ya kasi) itakuwa kwa sababu ya ‘amali za kila mmoja wenu. Na Mtume ﷺ atakuwa amesimama juu ya Swiraat, anasema: Mola wangu! Wasalimishe, wasalimishe. Mpaka matendo ya waja yashindwe, mpaka mtu aje hawezi kupita isipokuwa kwa kutambaa na katika pande zote mbili za Swiraatw kuna koleo zimening’ing’izwa, ambazo zimeamriwa (na Allaah Subhaanahu Wa Ta’aalaa). Yule atakayekwaruzwa atakuwa ni mwenye kufaulu na wasiokuwa wao wataingia motoni]. Na yule ambaye kwamba nafsi ya Abuu Hurayrah ipo mikononi Mwake, hakika urefu wa Jahannam ni masafa miaka sabini. [Imepokewa na Muslim]


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله





Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.