BUSTANI YA WATU WEMA
عَنْ أُمِّ المُؤْمِنِينَ أُمِّ سَلَمَة هِنْدٍ بنتِ أَبِي أُمَيَّةَ حُذيْفَةَ رضي اللَّه عنها ، عن النبي صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم أنه قال : « إِنَّهُ يُسْتَعْملُ عَليْكُمْ أُمَراءُ فَتَعْرِفُونَ وتنُكِرُونَ فَمِنْ كَرِه فقَدْ بَرِىءَ وَمَنْ أَنْكَرَ فَقَدْ سَلِمَ ، وَلَكِنْ منْ رَضِيَ وَتَابَعَ » قالوا : يا رَسُولَ اللَّه أَلاَ نُقَاتِلُهُمْ ؟ قَالَ : «لاَ، مَا أَقَامُوا فِيكُمْ الصَّلاَةَ » رواه مسلم
مَعْنَاهُ : مَنْ كَرِهَ بِقَلْبِهِ ولَمْ يَسْتطِعْ إنْكَاراً بِيَدٍ وَلا لِسَانٍ فَقَدْ بَرِئَ مِنَ الإِثمِ وَأَدَّى وَظِيفَتَهُ ، ومَنْ أَنْكَرَ بَحَسَبِ طَاقَتِهِ فَقَدْ سَلِمَ مِنْ هَذِهِ المعصيةِ ، وَمَنْ رَضِيَ بِفِعْلِهمْ وتابعهم ، فَهُوَ العَاصي
Kutoka kwa Mama wa Waumini Ummu Salamah Hind bint Abu Umayyah Hudhayfah (Radhi za Allah ziwe juu yake ya kutoka kwa Mtume ﷺ amesema: [Hakika mutatawaliwa na viongozi, (baadhi ya mambo yao ) mtayajua (kwa kuwa yameafikiana na sheria) na mengine mtayachukia (kwa kuwa hayaafikiani na sheria) Basi atakayechukia huyo amesalimika, (hana dhambi) lakini atakae ridhia na akafwata (huyo atakuwa na madambi)] (Maswahaba) Wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Je, tupigane nao? Akasema: [La (Msipigane nao) iwapo watasimamisha Swala miongoni mwenu.] [Imepokewa na Muslim]
Maana yake: Mwenye kuchukia kwa moyo wake na asiweze kukanya kwa Mkono wake wala kwa Ulimi wake basi amesalimika na Madhambi na ametekeleza wadhifa wake, na Mwenye kukanya kwa vile anavyo weza basi amesalimika na Madhambi,na mwenye kuridhia na vitendo vyao na akawafuata basi huyo ndie mkosefu
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله