BUSTANI YA WATU WEMA
عَنْ أَبَي عَمروٍ جَرير بنِ عبدِ اللَّه ، رضي اللَّه عنه ، قال : كُنَّا في صَدْر النَّهارِ عِنْد رسولِ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم فَجاءهُ قوْمٌ عُرَاةٌ مُجْتابي النِّمار أَو الْعَباءِ . مُتَقلِّدي السُّيوفِ عامَّتُهمْ ، بل كلهم مِنْ مُضرَ ، فَتمعَّر وجهُ رسولِ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، لِما رَأَى بِهِمْ مِنْ الْفَاقة ، فدخلَ ثُمَّ خرج ، فَأَمر بلالاً فَأَذَّن وأَقَامَ ، فَصلَّى ثُمَّ خَطبَ ، فَقالَ : {يَا أَيُّهَا الناسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الذي خلقكُمْ مِنْ نَفْسٍ وَاحِدةٍ } إِلَى آخِرِ الآية: { إِنَّ اللَّه كَانَ عَليْكُمْ رَقِيباً} ، وَالآيةُ الأُخْرَى الَّتِي في آخر الْحشْرِ : { يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمنُوا اتَّقُوا اللَّه ولْتنظُرْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمتْ لِغَدٍ} تَصدٍََّق رَجُلٌ مِنْ دِينَارِهِ مِنْ دِرْهَمهِ مِنْ ثَوْبِهِ مِنْ صَاع بُرِّه مِنْ صَاعِ تَمرِه حَتَّى قَالَ : وَلوْ بِشقِّ تَمْرةٍ فَجَاءَ رَجُلٌ مِنْ الأَنْصَارِ بِصُرَّةٍ كادتْ كَفُّهُ تَعجزُ عَنْهَا ، بَلْ قَدْ عَجزتْ ، ثُمَّ تَتابَعَ النَّاسُ حَتَّى رَأَيْتُ كَوْميْنِ مِنْ طَعامٍ وَثيابٍ ، حتَّى رَأَيْتُ وجْهَ رسولِ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، يَتهلَّلُ كَأَنَّهُ مذْهَبَةٌ ، فقال رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : « مَنْ سَنَّ في الإِسْلام سُنةً حَسنةً فَلَهُ أَجْرُهَا، وأَجْرُ منْ عَملَ بِهَا مِنْ بَعْدِهِ مِنْ غَيْرِ أَنْ ينْقُصَ مِنْ أُجُورهِمْ شَيءٌ ، ومَنْ سَنَّ في الإِسْلامِ سُنَّةً سيَّئةً كَانَ عَليه وِزْرها وَوِزرُ مَنْ عَمِلَ بِهَا مِنْ بعْده مِنْ غَيْرِ أَنْ يَنْقُصَ مِنْ أَوْزارهمْ شَيْءٌ » رواه مسلم
Kutoka kwa Abuu ‘Amru Jariyr bin ‘Abdillaah Radhi za Allah ziwe juu yake amesema kwamba: Tulikuwa pamoja na Mtume ﷺ katikati ya mchana. Mara wakaja watu waliokuwa Uchi wamevaa nguo za sufi, na majoho, (za kupasukapasuka) panga zao zikiwa zinagusa chini. Wote walikuwa wanatoka kabila ya Mudhar, bali wote walikuwa ni kutoka kabila la Mudhar. Uso wa Mtume ﷺ ulibadilika kwa kuwaona hawa watu katika hali hii ya shida na njaa. Akaingia nyumbani kwake kisha akatoka. Alimuamuru Bilaal Radhi za Allah ziwe juu yake akaadhini kisha akakimu, kisha (Mtume ﷺ) aliswalisha na kuwahutubia watu (baada ya Swala,) akasema: [Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni.]
Na akasoma aya nyingine ambayo ipo mwisho wa Suratu Al-Hashr: [Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kila nafsi iangalie inayo yatanguliza kwa ajili ya Kesho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari ya mnayo yatenda.]
(Baada ya hayo akasema) Mtu natoe sadaka katika dinari yake, dirhamu yake, nguo yake, Pishi yake ya ngano, Pishi yake ya tende, mpaka akasema: “Hata kama mtu atatoa kipande cha tende.” Mtu mmoja wa ki Answaar (aliposikia haya) alikuja na mzigo uliomuelemea kuubeba. halafu Wengine wakamfuata (kwa kuleta sadaka zao) mpaka nikaona mirundiko miwili ya Vyakula na nguo. Nikauona uso wa Mtume ﷺ unang’aa kama kwamba ni dhahabu. Mtume ﷺ akasema : [Atakae weka katika Uislamu mwenendo nzuri atapata ujira wake ya na ujira (thawabu) atakaetenda kitendo hicho baada yake bila ya wao kupunguziwa chochote katika ujira wao. Na atakeweka mwendo mbaya, atapata madhambi zake na dhambi za atakaetenda baada yake bila ya wao kupunguziwa chochote katika dhambi zao.] [Imepokewa na Muslim]
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله