BUSTANI YA WATU WEMA
عن جابرٍ رضي اللَّه عنه أَنْ رسولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم أَمَر بِلَعْقِ الأَصابِعِ وَالصحْفةِ وقال: « إِنَّكُــم لا تَدْرُونَ في أَيِّهَا الْبَرَكَةَ » رواه مسلم
وفي رواية لَهُ : « إِذَا وَقَعتْ لُقْمةُ أَحدِكُمْ فَلْيَأْخُذْهَا فَلْيُمِطْ مَا كَانَ بِهَا مِنْ أَذًى ، وَلْيَأْكُلْهَا ، وَلا يَدَعْهَا لَلشَّيْطانِ ، وَلا يَمْسَحْ يَدَهُ بِالْمَندِيلِ حَتَّى يَلْعَقَ أَصَابِعهُ ، فَإِنَّهُ لا يدْرِي في أَيِّ طَعَامِهِ الْبَركَةَ
وفي رواية له : « إِنَّ الشَّيْطَانَ يَحْضُرُ أَحَدكُمْ عِنْدَ كُلِّ شَيءٍ مِنْ شَأْنِهِ حَتَّى يَحْضُرَهُ عِنْدَ طَعَامِهِ ، فَإِذَا سَقَطَتْ مِنْ أَحَدِكُمْ اللُّقْمَةُ فَلْيُمِطْ مَا كَان بِهَا منْ أَذًى، فَلْيأْكُلْها ، وَلا يَدَعْهَا لِلشَّيْطَانِ
Kutoka kwa Jaabir Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume ﷺ ameamrisha kulamba vidole na sahani, akasema: [Ninyi hamjui ni wapi penye baraka.] [Imepokewana Muslim]
Na katika Riwaya nyingine ya Muslim imesema:
[Linapoanguka tonge la chakula la mmoja wenu, aliokote na aondoe taka iliyoingia na alile, wala asimuachie shetani, wala asiupanguse mkono wake kwa kitambaa mpaka avilambe kidole vyake; kwani hajui ni katika chakula kipi kuna baraka.]
Na Riwaya nyingine tena ya Muslim imesema:
[Hakika shetani anahudhuria katika kila jambo la mmoja wenu hata anahudhuria kwenye chakula chake. Basi linapoanguka tonge la chakula la mmoja wenu, aondoe sehemu iliyoingia taka na alile,wala asimuachie shetani.]