باب الدعاء للميت بعد دفنه والقعود عند قبره ساعة للدُّعاء له والاستغفار والقراءة
عن أَبي عَمْرو وقيل: أَبُو عبد اللَّه، وقيل: أَبو لَيْلى عُثْمَانُ بن عَفَّانَ رضي اللَّه عنه قَالَ: كانَ النَّبيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم إِذَا فرَغَ مِن دَفْنِ المَيِّتِ وقَفَ علَيهِ، وقال: “استغفِرُوا لأخِيكُم وسَلُوا لَهُ التَّثبيتَ فإنَّهُ الآنَ يُسأَلُ “. رواه أَبُو داود
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
161. MLANGO WA KUMUOMBEA DUA MAITI BAADA YA KUMZIKA, KUKETI KABURINI MWAKE KWA MDA ILI KUMUOMBEA DUA NA KUMUOMBEA ISTIGHFARI NA KUSOMA (QUR’ÂN)
Imepokewa na Abû ‘Amri, pia huitwa Abû ‘Abdillâh, na pia anajulikana kama Abû Lailâ, ‘Uthmân bin ‘Affân (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Mtume ﷺ alikuwa anapomaliza kumzika maiti husimama na akasema: “Muombeeni istighfari ndugu yenu na mumuombee uthibitisho, hakika yeye hivi sasa anaulizwa.” [ Imepokewa na Abû Dâwûd ].