KINGA YA MUISLAMU
Amesema Mtume ﷺ Mwenye kusema:
سُبْحَانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ
[Ametakasika Allaah na sifa njema zote ni zake]
kwa siku mara mia, atafutiwa madhambi yake hata kama yalikuwa mfano wa povu la bahari. [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
Na Mtume ﷺ amesema : “Atakaye sema:
[ لا إله إلا وحده لا شريك لهُ ، لهُ الملك ، ولهُ الحمدُ ، وهو على كل شيء قدير عشر مرات ]
[Hapana mola apasae kuabudiwa kwahaki ila Allaah hali ya kuwa peke yake hana mshirika ni wake Ufalme na ni zake kila sifa njema na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza.] mara kumi, ni kama (thawabu za mtu) aliyewacha huru nafsi nne katika wana wa Ismail. [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
Na amesema Mtume ﷺ Kuna maneno mawili ni mepesi mno juu ya ulimi, mazito mno katika mizani, yanapendeza mno mbele ya Rahmani (Mwenye kurehemu) nayo ni :
[ سبحان الله وبحمده سبحان الله العظيم ]
[Ametakasika Allaah na sifa njema zote ni zake, ametakasika Allaah aliye Mtukufu] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
Na amesema Mtume ﷺ Kusema kwangu:
[ سبحان الله ، والحمد لله ،ولا إله إلا الله ، والله أكبر ]
[Ametakasika Allaah na sifa njema zote ni za Allaah na hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Allaah, na Allaah ni Mkubwa]
ni bora kwangu kuliko kila kilichoangaziwa na jua. [Imepokewa na Muslim.]
Na amesema Mtume ﷺ: [Hivi anashindwa mmoja wenu kuchuma kila siku thawabu elfu? Mtu mmoja miongoni mwa waliokaa akamuuliza “Atachuma vipi mmoja wetu thawabu elfu? Akamjibu ﷺ Aseme :
سُبْحَانَ اللهِ
[Ametakasika Allaah]
……. Mara mia moja, basi ataandikiwa thawabu elfu moja, au atafutiwa madhami elfu moja. [Imepokewa na Muslim.]
Na Mtume ﷺ amesema : Atakaesema:
سُبْحَانَ اللهِ العَظِيمِ وبِحَمْدِهِ
[Ametakasika Allaah aliye Mtukufu na sifa njema zote ni zake]
.. hupandiwa mtende peponi [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy na Al-Haakim.]
Na amesema Mtume ﷺ [Ewe Abdalla Bin Qays, hivi nikufahamishe (nikuonyeshe) hazina miongoni mwa hazina za pepo? Nikamwambia: Ndio Ewe Mtume wa Allaah. Akaniambia: ‘Sema:
لا حول ولا قوة إلا بالله
[Hakuna uwezo wala nguvu ila za Allaah] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
Na akasema Mtume ﷺ [Bora ya maneno kwa Allaah ni manne :
[سُبْحَانَ اللهِ، والْحَمْدُ للهِ، لاَ إِلَهَ إَلاَّ اللهُ واللهُ أَكْبَرُ وَلاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إلاَّ باللهِ]
[Ametakasika Allaah na sifa njema ni za Allaah na hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Allaah , na Allaah ni Mkubwa]
…. Si vibaya kuanza kwa lolote katika haya. [Imepokewa na Muslim.]
Alikuja mtu mmoja wa shamba kwa Mtume ﷺ akamwambia, nifundishe maneno nitakayoyasema. Mtume ﷺ akamwambia : Sema:
لاَ إِلهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، اللهُ أَكْبَرُ كَبيراَ والْحَمْدُ للهِ كَثيراً، سُبْحَانَ اللهِ رَبِّ العَالَمينَ، لاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ باللهِ العَزيزِ الْحَكِيمِ
[Hapana mola apasae kuabudiwa kwahaki ila ni Allaah hali ya kuwa peke yake wala hana mshirika wake, Allaah ni Mkubwa tena sana, na sifa njema zote ni za Allaah tena nyingi sana. Ametakasika Allaah mola wa viumbe vyote, hapana uwezo wala nguvu ila ni za Allaah , Mwenye Kutukuka Mwingi wa Hekima]
yule mtu kisha akasema “Haya ni ya Allaah ni yapi yangu? Mtume akamwambia, Sema:
اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي، وارْحَمْنِي، واهْدِنِي، وارْزُقْنِي
[Ewe Allaah nisameh na unirehemu na uniongoze na uniruzuku] [Imepokewa na Muslim.]
Alikuwa mtu akisilimu, mtume anamfundisha kuswali kisha anamuamrisha kuomba kwa matamshi haya:
اللَّهُمَّ اغْفِرِ لِي، وارْحَمْنِي، واهْدِنِي، وعَافِنِي وارْزُقْنِي
[Ewe Allaah nisamehe na unirehemu na uniongoze na unipe afya njema na uniruzuku] [Imepokewa na Muslim.]
Bora ya dua ni mtu kusema:
[الْحَمْدُ للهِ]
[Kila sifa njema ni za Allaah]
na bora ya utajo (uradi) ni mtu kusema:
لاَ إِلَه إِلاَّ اللهُ
[Hapana mola apasae kuabudiwa kwahaki ila ni Allaah.] [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy na Ibnu Maajah na Al-Haakim]
Mema yasiokwisha ni :
سُبْحَانَ اللهِ، والْحَمْدُ للهِ،لاَ إِلَهَ إَلاَّ اللهُ واللهُ أَكْبَرُ وَلاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إلاَّ باللهِ
[Ametakasika Allaah na sifa njema zote ni za Allaah, hapana mola apasae kuabudiwa kwahaki ila ni Allaah, na Allaah ni Mkubwa, nahakuna uwezo wala nguvu ila za Allaah.] [Imepokewa na Ahmad.]