0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

127. Riyadhu Swalihina Mlango wa Ubainifu wa Njia nyingi za Kheri Hadithi ya 11

BUSTANI YA WATU WEMA


عن أَبِي هريرة رضي اللَّه عنْهُ عن النبي صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال : « لَقَد رأَيْتُ رَجُلاً يَتَقَلَّبُ فِي الْجنَّةِ فِي شَجرةٍ قطَعها مِنْ ظَهْرِ الطَّريقِ كَانَتْ تُؤْذِي الْمُسلِمِينَ » . رواه مسلم

وفي رواية : « مرَّ رجُلٌ بِغُصْنِ شَجرةٍ عَلَى ظَهْرِ طرِيقٍ فَقَالَ : واللَّهِ لأُنَحِّينَّ هذا عنِ الْمسلِمِينَ لا يُؤْذِيهُمْ ، فأُدْخِلَ الْجَنَّةَ
وفي رواية لهما : « بيْنَما رجُلٌ يمْشِي بِطريقٍ وجد غُصْن شَوْكٍ علَى الطَّرِيقِ ، فأخَّرُه فشَكَر اللَّهُ لَهُ ، فغَفر لَهُ


Kutoka kwa Abuu Hurayrah  Radhi za Allah ziwe juu yake amepokea kutoka kwa Mtume  Amesema: [Kwa hakika nilimuona mtu akitembea Peponi kwa sababu ya mti alioukata katikati ya njia uliokuwa ukiwaudhi Waislaamu.]      [Imepokewa na Muslim]

Na katika Riwaya nyingine inasema: [Mtu mmoja alipita katikati ya tawi la mti uliokuwa katikati ya njia, akasema: Wa-Allaahi nitaliondoa tawi hili lisiwaudhi Waislaamu. basi Akaingizwa Peponi].

Na Riwaya nyingine ya Bukhari na Muslim imesema: [Mtu mmoja alipokuwa akitembea njiani, akakuta tawi la mti wenye miba njiani, akaliweka nyuma. Mwenyezi Mungu Akamjazi na Akamghufuria.]


 شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله



Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.