باب مَا يقول إِذَا لبس ثوباً جديداً أَوْ نعلاً أَوْ نحوه
عن أَبي سعيد الخُدْري رضيَ اللَّه عنه قَالَ: كانَ رسُولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم إِذَا اسْتَجَدَّ ثَوْباً سمَّاهُ باسْمِهِ عِمامَةً، أَوْ قَمِيصاً، أَوْ رِدَاءً يقُولُ: “اللَّهُمَّ لكَ الحَمْدُ أَنْتَ كَسَوْتَنِيهِ، أَسْأَلُكَ خَيْرَهُ وَخَيْرَ مَا صُنِع لَهُ، وأَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّهِ وشَرِّ مَا صُنِعَ لَهُ”
رواهُ أَبو داود، والترمذي وَقالَ: حديث حسن
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
125. MLANGO WA ANAYOSEMA ANAYEVAA NGUO MPYA, AU VIATU NA MFANO WAKE
Imepokewa na Abû Sa‘îd al-Khudry (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Alikuwa Mtume ﷺ anapovaa nguo mpya huitaja nguo hiyo kwa jina lake, ima iwe ni kilemba, kanzu au kishali. Kisha akiomba: “Allâhumma lakalhamdu Anta kasawtanîhi, as-aluka khairahû wa khaira mâ suni‘a lahû wa a-ûdhu bika min sharrihî wa sharri mâ suni‘a lahû.” [Ewe Mola shukrani ni Zako Wewe Ndiwe Ulienivisha nguo hii. Nakuomba kheri yake na kheri iliyotengenezewa nguo hii. Na najilinda Kwako kutokana na shari yake na shari iliyotengenezewa nguo hii._” [ Imepokewa na Abû Dâwûd na Tirmidhy, na amesema: Hadîth hii ni Hasan.]