0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

114. Riyadhu Swalihina Mlango wa Kuhimiza kufanya kheri Mwisho wa Umuri Hadithi ya 03


BUSTANI YA WATU WEMA


1463655589


عن عائشةَ رضي اللَّه عنها قالت : ما صَلَّى رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم صلاةً بعْد أَنْ نزَلَتْ علَيْهِ { إذَا جَاءَ نصْرُ اللِّهِ والْفَتْحُ } إلاَّ يقول فيها : « سُبْحانك ربَّنَا وبِحمْدِكَ ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لى »   متفقٌ عليه
وفي رواية الصحيحين عنها : كان رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يُكْثِر أنْ يَقُول فِي ركُوعِه وسُجُودِهِ : « سُبْحانَكَ اللَّهُمَّ ربَّنَا وَبحمْدِكَ ، اللَّهمَّ اغْفِرْ لي »    يتأوَّل الْقُرْآن
{معنى : « يتأوَّل الْقُرُآنَ » أيْ : يعْمل مَا أُمِرَ بِهِ في الْقُــرآنِ في قولِهِ تعالى : {فَسبِّحْ بِحمْدِ ربِّكَ واستَغْفِرْهُ 
وفي رواية لمسلم : كان رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يُكْثِرُ أنْ يَقولَ قبْلَ أَنْ يَمُوتَ : «سُبْحانَكَ اللَّهُمَّ وبِحْمدِكَ ، أسْتَغْفِركَ وأتُوبُ إلَيْكَ » . قالت عائشةُ : قلت : يا رسولَ اللَّه ما هذِهِ الكلِمَاتُ الَّتي أرَاكَ أحْدثْتَها تَقولها ؟ قــال : « جُعِلَتْ لِي علامةٌ في أمَّتي إذا رَأيتُها قُلتُها {إذَا جَاءَ نَصْرُ اللِّهِ والْفَتْحُ } إلى آخر السورة
وفي رواية له : كان رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يُكْثِرُ مِنْ قَوْلِ : « سُبْحانَ اللَّهِ وبحَمْدِهِ . أسْتَغْفِرُ اللَّه وَأَتُوبُ إلَيْه » . قالت : قلت : يا رسولَ اللَّه ، أَرَاكَ تُكْثِرُ مِنْ قَوْل : سُبْحَانَ اللَّهِ وبحمْدِهِ ، أسْتغْفِر اللَّه وأتُوبُ إليْهِ ؟ فقال : « أخْبرني ربِّي أنِّي سَأرَى علاَمَةً فِي أُمَّتي فَإِذَا رأيْتُها أكْثَرْتُ مِن قَوْلِ : سُبْحانَ اللَّهِ وبحَمْدِهِ ، أسْتَغْفِرُ اللَّه وَأتُوبُ إلَيْهِ : فَقَدْ رَأَيْتُها: {إذَا جَاءَ نَصْرُ اللِّهِ والْفَتْحُ } فَتْحُ مَكَّةَ ، { ورأيْتَ النَّاس يدْخُلُونَ فِي دِينِ اللَّهِ أفْوَاجًا ، فَسبحْ بحمْدِ ربِّكَ واسْتَغفِرْهُ إنَّهُ كانَ توَّاباً


Kutoka kwa Bibi ‘Aisha Radhi za Allah ziwe juu yake  amesema: Mtume ﷺ hakuswali Swala yoyote baada ya kuteremka Sura hii [Itakapo kuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ushindi,] Isipokuwa alikuwa akisema: [Kutakasika ni Kwako Mola wetu, Ewe Mola nisamehe.]   [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Na katika Riwaya nyingine ya Swahih Al-Bukhari na Swahih Muslim; Mtume ﷺ alikuwa akikithirisha kusema katika Rukuu yake na sijda yake: [Kutakasika ni kwako Mola wetu, Ewe Mola nisamehe.]      Akiifuata Qur’ani akifanya kama alivyo amrishwa na Qur’ani katika neno lake Mwenyezi Mungu [Zitakase sifa za Mola wako Mlezi, na umwombe msamaha]

Na katika Riwaya nyingine ya Muslim imesema: Mtume alikuwa akikithirisha kusema kabla ya kufa kwake . [Kutakasika ni kwa Mwenyezi Mungu na himdi zote ni Zake, namuomba Msamaha na ninatubia kwakeAsema Aisha:

Nikamuuliza Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nakuona unakithirisha kusema haya maneno  Akajibu:Nimeekewa alama nikiona kwa umma wangu basi niseme maneno hayo [Itakapo kuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ushindi,]  mpaka mwisho wa sura.

Na katika Riwaya nyingine ya Musalim  alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu akikithirisha kusema [Kutakasika ni kwa Mwenyezi Mungu na himdi zote ni Zake, namuomba Msamaha na ninatubia Kwake]  akasema: nikamuuliza nakuona wakitihrisha kusema [Kutakasika ni kwa Mwenyezi Mungu na himdi zote ni Zake, namuomba Msamaha na ninatubia Kwake] akamjibu  [Mola wangu ameniambia  kuwa mimi nitaona alama katika Umma wangu, nitakapoiona nikithirishe kusema: [Kutakasika ni kwa Mwenyezi Mungu na himdi zote ni Zake, namuomba Msamaha na ninatubia Kwake] Nami nimeshaiona: [Itakapo kuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ushindi,] nao ni kukombolewa Makka.  [Na ukaona watu wanaingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundiZitakase sifa za Mola wako Mlezi, na umwombe msamaha; hakika Yeye ndiye anaye pokea toba .]   


 شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله



Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.