0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

111. Riyadhu Swalihina Mlango wa Mujahada Hadithi ya 17


BUSTANI YA WATU WEMA


1463655589


عن عن سعيدِ بنِ عبدِ العزيزِ، عن رَبيعةَ بنِ يزيدَ، عن أَبِي إدريس الخَوْلاَنيِّ، عن أَبِي ذَرٍّ جُنْدُبِ بنِ جُنَادَةَ، رضي اللَّهُ عنه، عن النَّبِيِّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم فيما يَرْوِى عَنِ اللَّهِ تباركَ وتعالى أنه قال: «يا عِبَادِي إِنِّي حَرَّمْتُ الظُّلْمَ عَلَى نَفْسِي وَجَعَلْتُهُ بَيْنَكُمْ مُحَرَّماً فَلاَ تَظالمُوا، يَا عِبَادِي كُلُّكُم ضَالٌّ إِلاَّ مَنْ هَدَيْتُهُ، فَاسْتَهْدُوني أهْدكُمْ، يَا عِبَادي كُلُّكُمْ جائعٌ إِلاَّ منْ أطعمتُه، فاسْتطْعموني أطعمْكم، يا عبادي كلكم عَارٍ إلاَّ مِنْ كَسَوْتُهُ فَاسْتَكْسُوني أكْسُكُمْ، يَا عِبَادِي إنَّكُمْ تُخْطِئُونَ بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَأَنَا أغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعاً، فَاسْتَغْفِرُوني أغْفِرْ لَكُمْ، يَا عِبَادِي إِنَّكُمْ لَنْ تَبْلُغُوا ضُرِّي فَتَضُرُّوني، وَلَنْ تَبْلُغُوا نَفْعِي فَتَنْفَعُوني، يَا عِبَادِي لَوْ أَنَّ أوَّلَكُمْ وآخِركُمْ، وَإنْسَكُمْ وَجِنَّكُمْ كَانُوا عَلَى أتقَى قلبِ رجلٍ واحدٍ منكم ما زادَ ذلكَ فِي مُلكي شيئاً، يا عِبَادِي لو أَنَّ أوَّلكم وآخرَكُم وإنسَكُم وجنكُمْ كَانوا عَلَى أفْجَرِ قَلْبِ رَجُلٍ وَاحِدٍ مِنْكُمْ مَا نَقَصَ ذَلِكَ مِنْ مُلْكِي شَيْئاً، يَا عِبَادِي لَوْ أَنَّ أَوَّلَكُمْ وَآخِركُمْ وَإنْسَكُمْ وَجِنَّكُمْ، قَامُوا فِي صَعيدٍ وَاحدٍ، فَسألُوني فَأعْطَيْتُ كُلَّ إنْسانٍمَسْألَتَهُ، مَا نَقَصَ ذَلِكَ مِمَّا عِنْدِي إِلاَّ كَمَا َيَنْقُصُ المِخْيَطُ إِذَا أُدْخِلَ البَحْرَ، يَا عِبَادِي إنَّما هِيَ أعْمَالُكُمْ أُحْصِيهَا لَكُمْ، ثُمَّ أوَفِّيكُمْ إيَّاهَا، فَمَنْ وَجَدَ خَيْراً فَلْيَحْمِدِ اللَّه، وَمَنْ وَجَدَ غَيْرَ ذَلِكَ فَلاَ يَلُومَنَّ إلاَّ نَفْسَهُ».

قَالَ سعيدٌ: كان أبو إدريس إذا حدَّثَ بهذا الحديث جَثَا عَلَى رُكبتيه.    رواه مسلم

وروينا عن الإمام أحمد بن حنبل رحمه اللَّه قال: ليس لأهل الشام حديث أشرف من هذا الحديث


Kutoka kwa Said bin Abdulaziz amepokea kutoka kwa Rabia bin Yazid kutoka Idriis Al Khawlaani kutoka kwa Abuu Dharr, Jundub bin Junaadah Radhi za Allah ziwe juu yake amepokea kutoka kwa Mtume katika aliyopokea kutoka kwa Mola wake Anasema: [Enyi waja Wangu, hakika Nimeharamisha dhulma, na Nimeijaalia ni haramu miongoni mwenu; kwa hivyo msidhulumiane. Enyi waja Wangu, nyote mmepotea isipokuwa Niliyemuongoza, kwa hivyo Niombeni uongofu Nami Nitawaongoa. Enyi waja Wangu, nyote mna njaa isipokuwa niliyemlisha, kwa hivyo niombeni chakula Nami Nitawalisha. Enyi waja Wangu, nyote mpo uchi isipokuwa Niliyemvisha, kwa hivyo niombeni Niwavishe, Nami Nitawavisha. Enyi waja Wangu, nyinyi mnakosea usiku na mchana, Nami Nasamehe dhambi zote; kwa hivyo niombeni msamaha Nami Nitawasamehe. Enyi waja Wangu, nyinyi hamuwezi kunidhuru wala hamuwezi kuninufaisha. Enyi waja Wangu, lau wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, wanadamu wenu na majini wenu wangalikuwa sawa na moyo wa mchaji Mwenyezi Mungu mno miongoni mwenu, basi hilo halingenizidishia chochote katika Ufalme Wangu. Enyi waja Wangu, lau wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, wanaadam wenu na majini wenu wangalikuwa sawa na moyo wa mtu muovu mno miongoni mwenu, basi hilo lisingalipunguza chochote katika Ufalme Wangu. Enyi waja Wangu, lau wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, wanaadam wenu na majini wenu wangesimama katika uwanja mmoja, wakaniomba; Nami Nikampa kila mmoja ombi lake, isingalipungua chochote katika Nilichowapa isipokuwa ni kama vile sindano iliyochovywa baharini inavyopunguza maji. Enyi waja Wangu, hakika Nimezidhibiti ‘amali zenu, kisha Nitawalipa; atakayekuta kheri amuhimidi Mwenyezi Mungu, na atakayekuta kinyume chake basi asilaumu isipokuwa ailaumu nafsi yake.]

Asema Sa’ad: (ambaye ni mpokezi wa Hadithi hii) amesema: Abuu Idriys alikuwa, anapohadithia Hadithi hii, akikaa kwa kupiga magoti.    [Imepokewa na Muslim]


 شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله



Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.