BUSTANI YA WATU WEMA
عن أنسٍ رضي اللَّه عنه، قال: غَاب عمِّي أَنَسُ بنُ النَّضْرِ رضي اللَّهُ عنه، عن قِتالِ بدرٍ، فقال: يا رسولَ اللَّه غِبْت عن أوَّلِ قِتالٍ قَاتلْتَ المُشرِكِينَ، لَئِنِ اللَّهُ أشْهَدَنِي قتالَ المشركين لَيُرِيَنَّ اللَّهُ ما أصنعُ، فلما كانَ يومُ أُحدٍ انْكشَفَ المُسْلِمُون فقال: اللَّهُمَّ أعْتَذِرُ إليْكَ مِمَّا صنَع هَؤُلاءِ يَعْني أصْحَابَه وأبرأُ إلَيْكَ مِمَّا صنعَ هَؤُلاَءِ يعني المُشْرِكِينَ ثُمَّ تَقَدَّمَ فَاسْتَقْبَلَهُ سعْدُ بْنُ مُعاذٍ، فَقالَ: يا سعْدُ بْنَ معُاذٍ الْجنَّةُ ورَبِّ الكعْبةِ، إِنِى أجِدُ رِيحَهَا مِنْ دُونِ أُحُدٍ. قال سعْدٌ: فَمَا اسْتَطعْتُ يا رسول اللَّه ماصنَعَ، قَالَ أنسٌ: فَوجدْنَا بِهِ بِضْعاً وثمانِينَ ضَرْبةً بِالسَّيفِ، أوْ طَعْنَةً بِرُمْحٍ، أو رمْيةً بِسهْمٍ، ووجدْناهُ قَد قُتِلَ وَمثَّلَ بِهِ المُشرِكُونَ فَما عرفَهُ أَحدٌ إِلاَّ أُخْتُهُ بِبنَانِهِ. ققال أنسٌ: كُنَّا نَرى أوْ نَظُنُّ أنَّ هَذِهِ الآيَة نزلَتْ فيهِ وَفِي أشْباهِهِ: [مِنَ المُؤْمِنِينَ رِجالٌ صدقُوا ما عَاهَدُوا اللَّه علَيهِ] [الأحزاب: 23] إلى آخرها. متفقٌ عليه
Kutoka kwa Anas Radhi za Allah ziwe juu yake amesimulia: Alighibu Ammiy yangu Anas bin Nadhwr Radhi za Allah ziwe juu yake katika Vita vya Badr. Akasema: Ewe Mtume wa Mungu, nilighibu katika vita vya kwanza ulivyopigana na Washirikina. Na apa kwa jina Mwenyezi Mungu Akinijaalia kuhudhuria katika kupigana na washirikina, Atawadhihirishia (washirikina) kile nitakachofanya. vilipofika Vita vya Uhud, Waislamu wakashindwa akasema: Ewe Mola, nakuomba msamaha kwa yale waliyoyafanya hawa (watu wake), na najitenga kwa yale waliyoyafanya hawa (washirikina.) Halafu akasonga mbele, akakutana na Sa’ad bin Mu’aadh, akamwambia: Ewe Sa’d bin Mu’aadh, Pepo! Naapa kwa Mola wa Al-Ka’bah, naisikia harufu yake katika jabali la Uhud. akasema Sa’ad: Sikuweza kufanya namna alivyofanya Ewe Mtume wa Mungu. Anas bin Maalik anaelezea: Tukamkuta amepigwa zaidi ya mapigo themanini ya mapanga, au kudungwa mkuki au kurushia mshale. Tulimkuta ameshauliwa na washirikina na wamemkata pua na masikio yake. Basi hakuna aliyeweza kumtambua isipokuwa dada yake, alimtambua kwa ncha ya vidole vyake. Anas bin Maalik anaeleza: Tulikuwa tukiona au tukidhani kuwa Ayah hii [Suratul Ahzaab: 23.] Ilikuwa imeshuka kwa sababu yake na mfano wake. [Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.] [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله