BUSTANI YA WATU WEMA
عنْ أنسٍ رضيَ اللَّهُ عنه قال : قال : رسولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : « مَنْ قَالَ يعنِي إذا خَرَج مِنْ بيْتِهِ : بِسْم اللَّهِ توكَّلْتُ عَلَى اللَّهِ ، ولا حوْلَ ولا قُوةَ إلاَّ بِاللَّهِ ، يقالُ لهُ هُديتَ وَكُفِيت ووُقِيتَ ، وتنحَّى عنه الشَّيْطَانُ » رواه أبو داودَ والترمذيُّ ، والنِّسائِيُّ وغيرُهمِ : وقال الترمذيُّ حديثٌ حسنٌ ، زاد أبو داود : « فيقول : يعْنِي الشَّيْطَانَ لِشَيْطانٍ آخر : كيْفَ لك بِرجُلٍ قَدْ هُدِيَ وَكُفي وَوُقِى»؟
Kutoka kwa Anas Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mweneyzi Mungu ﷺ : [Atakayesema anapotoka Nyumbani kwake. Kwa jina la Mwenyezi Mungu nimemtegea Mwenyezi Mungu, hakuna hila (ya kuepuka maasi) wala nguvu (ya kufanya ‘Ibaada) ila kwa msaada wa Mwenyezi Mungu. Ataambiwa: Umeshaongozwa, umeshatoshelezwa, na umeshakingwa, na shawani hujitenga naye.] [Imepokewa na Abuu Dawud, na At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy na wengineo. At-Tirmidhiy amesema: Hadiyth hii ni Hasan]
na Abuu Dawud ameongezea: [shetani humueleza shatani mwenzie: Utamuwezaje mtu aliyeongozwa, akatoshelezwa na akakingwa?]