0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

081. Riyadhu Swalihina Mlango wa Yakini na Kumtegemea Mwenyezi Mungu Hadithi ya 08


BUSTANI YA WATU WEMA


 رياض الصالحين


عنْ أبي بَكْرٍ الصِّدِّيق رضي اللَّه عنه عبدِ اللَّه بنِ عثمانَ بنِ عامِرِ بنِ عُمَرَ ابن كعب بن سعد بْنِ تَيْمِ بْن مُرَّةَ بْنِ كَعْبِ بْن لُؤيِّ بْنِ غَالِب الْقُرَشِيِّ التَّيْمِيِّ رضي اللَّه عنه وهُو وأبُوهُ وَأُمَّهُ صحابَةٌ ، رضي اللَّه عنهم قال : نظرتُ إلى أقْدَامِ المُشْرِكِينَ ونَحنُ في الْغَارِ وهُمْ علَى رؤوسنا فقلتُ : يا رسولَ اللَّهِ لَوْ أَنَّ أحَدَهمْ نَظرَ تَحتَ قَدميْهِ لأبصرَنا فقال: « مَا ظَنُّك يا أبا بكرٍ باثْنْينِ اللَّهُ ثالثُِهْما »     متفقٌ عليه


Kutoka kwa Abuu Bakr As-Swidiyq, Abdullaah ‘Uthmaan bin ‘Aamir bin ‘Umar bin Ka’ab bin Sa’ad bin Taym bin Murrah bin Ka’ab bin Lu-ayy bin Ghaalib Al-Qurashiy At-Taymiy Radhi za Allah ziwe juu yake yeye, baba yake na mama yake wote ni maswahaba Radhi za Allah ziwe juu yao amesema: Niliitazama miguu ya mshirikina nasi tupo pangoni nao wapo juu yetu (wanatutafuta ili watuue). Nikamwambia:, Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu lau mmoja wao atautazama chini ya mguu wake atatuona! Akasema: [Ewe Abuu Bakar, unadhaniaje watu wawili ambao watatu wao ni Mwenyezi Mungu ?]   [Imepokewa na Bukhari na Muslim]


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.