0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

078. Riyadhu Swalihina Mlango wa Yakini na Kumtegemea Mwenyezu Mungu Hadithi ya 05


BUSTANI YA WATU WEMA


رياض الصالحين


عنْ جَابِرٍ رضي اللَّهُ عنه أَنَّهُ غَزَا مَعَ النَّبِيِّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قِبَلَ نَجْدٍ فَلَمَّا قَفَل رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قَفَل مَعهُمْ ، فأدْركتْهُمُ الْقائِلَةُ في وادٍ كَثِيرِ الْعضَاهِ ، فَنَزَلَ رسولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم، وتَفَرَّقَ النَّاسُ يسْتظلُّونَ بالشجر ، ونَزَلَ رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم تَحْتَ سمُرَةٍ ، فَعَلَّقَ بِهَا سيْفَه ، ونِمْنَا نوْمةً ، فإذا رسولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يدْعونَا ، وإِذَا عِنْدَهُ أعْرابِيُّ فقَالَ : « إنَّ هَذَا اخْتَرَطَ عَلَيَّ سيْفي وأَنَا نَائِمٌ ، فاسْتيقَظتُ وَهُو في يدِهِ صَلْتاً ، قالَ : مَنْ يَمْنَعُكَ منِّي ؟ قُلْتُ : اللَّه ثَلاثاً » وَلَمْ يُعاقِبْهُ وَجَلَسَ .   متفقٌ عليه
وفي رواية : قَالَ جابِرٌ : كُنَّا مع رسول اللِّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم بذاتِ الرِّقاعِ ، فإذَا أتينا على شَجرةٍ ظليلة تركْنَاهَا لرسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، فَجاء رجُلٌ من الْمُشْرِكِين ، وسيف رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم مُعَلَّقٌ بالشَّجرةِ ، فاخْترطهُ فقال : تَخَافُنِي ؟ قَالَ : « لا » قَالَ : فمَنْ يمْنَعُكَ مِنِّي ؟ قال: «اللَّه
وفي رواية أبي بكرٍ الإِسماعيلي في صحيحِهِ : قال منْ يمْنعُكَ مِنِّي ؟ قَالَ : « اللَّهُ » قال: فسقَطَ السَّيْفُ مِنْ يدِهِ ، فأخذ رسَول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم السَّيْفَ فَقال : « منْ يمنعُكَ مِنِّي ؟ » فَقال : كُن خَيْرَ آخِذٍ ، فَقَالَ : « تَشهدُ أنْ لا إلَه إلا اللَّهُ ، وأنِّي رسولُ اللَّه ؟ » قال : لا، ولكِنِّي أعاهِدُك أن لا أقَاتِلَكَ ، ولا أكُونَ مع قوم يقاتلونك ، فَخلَّى سبِيلهُ ، فَأتى أصحابَه فقَالَ : جِئتكُمْ مِنْ عِندِ خيرِ النَّاسِ
قَولُهُ : « قَفَل » أيْ : رجع . و « الْعِضَاهُ » الشَّجر الذي لَه شَوْك . و «السَّمُرةُ » بِفَتْحِ السينِ وضمِّ الْميمِ : الشَّجَرةُ مِن الطَّلْحِ ، وهِي الْعِظَام منْ شَجرِ الْعِضاهِ . و « اخْترطَ السَّيْف » أي : سلَّهُ وهُو في يدِهِ . « صلتاً » أيْ : مسْلُولاً ، وهُو بِفْتح الصادِ وضمِّها


Kutoka kwa  Jaabir Radhi za Allah ziwe juu yake amesimulia kuwa yeye alikwenda kupigana Jihadi sehemu za Najd akiwa pamoja na Mtume ﷺ. aliporejea Mtume ﷺ, alirejea pamoja nao. Ikawakuta katikati ya mchana katika bonde lenye miti mingi ya miba. Mtume akashuka. Wa nao wakaenea (huku na kule) wakitafuta vivuli vya miti. Mtume alishuka chini ya mti wa samura (aina ya mti wenye miba), akautundika upanga wake, tukalala kidogo. Mara ghafla Mtume akatuita, akawa yupo na mbedui, akatuambia: [Mtu huyo kauchomoa upanga wangu nami nimelala, nikaamka nao upo mkononi mwake, akaniuliza: Ni nani atakaye kuhami dhidi yangu? Nikamjibu: [Mwenyezi Mungu mara tatu.] Wala hakumuadhibu, akaketi.       [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Na katika Riwaya nyingine inasema: “Jaabir Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Tulikuwa pamoja na Mtume  huko Dhaatir-Riqaa’, tunapofika kwenye mti wenye kivuli, tulimuachia Mtume . Akaja mtu katika Mushrikina na upanga wa Mtume  umetundikwa kwenye mti. Akauchomoa, akamuuliza: Unaniogopa? Mtume  akamjibu: [Hapana] Akamuuliza: Ni nani atakaye kuhami dhidi yangu? Akamwambia: [Mwenyezi Mungu].

Na katika Riwaya nyingine ya Abuu Bakr Al-Ismaa’iyl katika sahihi yake, imesema: Akamuuliza: Ni nani atakaye kuhami dhidi yangu? Akamwambia: [Mwenyezi Mungu] Upanga ukamuanguka kutoka mkononi mwake. Mtume  akauchukua upanga ule. Akamuuliza: [Ni nani atakaye kuhami dhidi yangu?] Akamjibu: Mbora mwenye kuuchukua. Akamuuliza: [Unashuhudia kuwa hakuna Anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kuwa mimi ni Mtume Wake?] Akajibu: Hapana. Lakini nakuahidi kuwa sitakupiga vita, wala sitokuwa pamoja na watu wanaopigana na wewe. Mtume  akamuacha aende zake. Akawaendea Maswahaba zake, akawaambia: [Nimewajia kutoka kwa mbora wa watu.]


 شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله





Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.