0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

065. Riyadhu Swalihina Mlango wa Kumchunga Mungu Hadithi ya 06

BUSTANI YA WATU WEMA


عَنْ أبي هُريْرَةَ رضي اللَّه عنه أَنَّهُ سمِع النَّبِيَّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يَقُولُ : « إِنَّ ثَلاَثَةً مِنْ بَنِي إِسْرائيلَ : أَبْرَصَ ، وأَقْرَعَ ، وأَعْمَى ، أَرَادَ اللَّهُ أَنْ يَبْتَليَهُمْ فَبَعث إِلَيْهِمْ مَلَكاً ، فأَتَى الأَبْرَصَ فَقَالَ : أَيُّ شَيْءٍ أَحبُّ إِلَيْكَ ؟ قَالَ : لَوْنٌ حسنٌ، وَجِلْدٌ حَسَنٌ ، ويُذْهَبُ عنِّي الَّذي قَدْ قَذَرنِي النَّاسُ ، فَمَسَحهُ فذَهَب عنهُ قذرهُ وَأُعْطِيَ لَوْناً حَسناً . قَالَ : فَأَيُّ الْمالِ أَحَبُّ إِلَيْكَ ؟ قال : الإِبلُ أَوْ قَالَ الْبَقَرُ شَكَّ الرَّاوِي فأُعْطِيَ نَاقَةً عُشرَاءَ ، فَقَالَ : بارَك اللَّهُ لَكَ فِيها
فأَتَى الأَقْرعَ فَقَالَ : أَيُّ شَيْءٍ أَحب إِلَيْكَ ؟ قال : شَعْرٌ حسنٌ ، ويذْهبُ عنِّي هَذَا الَّذي قَذِرَني النَّاسُ ، فَمسحهُ عنْهُ . أُعْطِيَ شَعراً حسناً . قال فَأَيُّ الْمَالِ . أَحبُّ إِلَيْكَ ؟ قال : الْبَقرُ ، فأُعِطيَ بقرةً حامِلاً ، وقَالَ : بَارَكَ اللَّهُ لَكَ فِيهَا
فَأَتَى الأَعْمَى فَقَالَ : أَيُّ شَيْءٍ أَحَبُّ إِلَيْكَ ؟ قال : أَنْ يرُدَّ اللَّهُ إِلَيَّ بَصَري فَأُبْصِرَ النَّاسَ فَمَسَحَهُ فَرَدَّ اللَّهُ إِلَيْهِ بصَرَهُ . قال : فَأَيُّ الْمَالِ أَحَبُّ إِليْكَ ؟ قال : الْغنمُ فَأُعْطِيَ شَاةً والِداً فَأَنْتجَ هذَانِ وَولَّدَ هَذا ، فكَانَ لِهَذَا وَادٍ مِنَ الإِبِلِ ، ولَهَذَا وَادٍ مِنَ الْبَقَرِ ، وَلَهَذَا وَادٍ مِنَ الْغَنَم
ثُمَّ إِنَّهُ أتَى الأْبرص في صورَتِهِ وَهَيْئتِهِ ، فَقَالَ : رَجُلٌ مِسْكينٌ قدِ انقَطعتْ بِيَ الْحِبَالُ في سَفَرِي ، فَلا بَلاغَ لِيَ الْيَوْمَ إِلاَّ باللَّهِ ثُمَّ بِكَ ، أَسْأَلُكَ بِالَّذي أَعْطَاكَ اللَّوْنَ الْحَسَنَ ، والْجِلْدَ الْحَسَنَ ، والْمَالَ ، بَعيِراً أَتبلَّغُ بِهِ في سفَرِي ، فقالَ : الحقُوقُ كَثِيرةٌ . فقال : كَأَنِّي أَعْرفُكُ أَلَمْ تَكُنْ أَبْرصَ يَقْذُرُكَ النَّاسُ ، فَقيراً ، فَأَعْطَاكَ اللَّهُ ، فقالَ : إِنَّما وَرثْتُ هَذا المالَ كَابراً عَنْ كابِرٍ ، فقالَ : إِنْ كُنْتَ كَاذِباً فَصَيَّركَ اللَّهُ إِلى مَا كُنْتَ
وأَتَى الأَقْرَع في صورتهِ وهيئَتِهِ ، فَقَالَ لَهُ مِـثْلَ ما قَالَ لهذَا ، وَرَدَّ عَلَيْه مِثْلَ مَاردَّ هَذَّا ، فَقَالَ : إِنْ كُنْتَ كَاذِباً فَصَيّرَكَ اللهُ إِليَ مَاكُنْتَ
وأَتَى الأَعْمَى في صُورتِهِ وهَيْئَتِهِ ، فقالَ : رَجُلٌ مِسْكينٌ وابْنُ سَبِيلٍ انْقَطَعَتْ بِيَ الْحِبَالُ في سَفَرِي ، فَلا بَلاغَ لِيَ اليَوْمَ إِلاَّ بِاللَّهِ ثُمَّ بِكَ ، أَسْأَلُكَ بالَّذي رَدَّ عَلَيْكَ بصرَكَ شَاةً أَتَبَلَّغُ بِهَا في سَفَرِي ؟ فقالَ : قَدْ كُنْتُ أَعْمَى فَرَدَّ اللَّهُ إِلَيَّ بَصري ، فَخُذْ مَا شِئْتَ وَدعْ مَا شِئْتَ فَوَاللَّهِ ما أَجْهَدُكَ الْيَوْمَ بِشْيءٍ أَخَذْتَهُ للَّهِ عزَّ وجلَّ . فقالَ : أَمْسِكْ مالَكَ فَإِنَّمَا ابْتُلِيتُمْ فَقَدْ رضيَ اللَّهُ عنك ، وَسَخَطَ عَلَى صَاحِبَيْكَ »     متفقٌ عليه


Abuu Hurayrah Radhi za Allah ziwe juu yake kuwa amemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema: [Watu watatu katika wana Israil Mwenyezi Mungu Alitaka kuwapa mtihani  Mwenye ukoma, mwenye kunyonyoka nywele (kipara) na kipofu. Akawapelekea Malaika. Akamwendea mwenye ukoma. Akamuuliza: “Kitu gani unachokipenda zaidi?” Akamjibu: “Napenda niwe na rangi nzuri, ngozi nzuri na niondokewe na hali hii ambayo watu wananidharau.” Yule Malaika akampangusa, ukoma ukamuondokea na akapewa rangi na ngozi nzuri. Akamuuliza: “Unapenda mali gani?” Akajibu: “Ngamia.”. Au alisema: Ng’ombe, (mpokezi amekuwa na mashaka kama ni ng’ombe au ngamia). Akapewa ngamia mwenye mimba (karibu na kuzaa). Akamuombea: “Mwenyezi Mungu Akubariki”.

Akamuendea mwenye upara. Akamuuliza: “Kitu gani unachokipenda zaidi?” Akamjibu: “Nywele nzuri, na niondokewe na hali hii ambayo watu wananidharau.” Akampangusa, akaondokewa na upara na akawa na nywele nzuri. Akamuuliza: “Unapenda mali gani?” Akamjibu: “Ng’ombe.” Akapewa ng’ombe mwenye mimba. Akamuombea: “Mwenyezi Mungu Akubarikie.” Akamuendea kipofu akamuuliza: “Kitu gani unachonapenda zaidi?” Akamjibu: “Napenda Mwenyezi Mungu Anirudishie macho yangu ili nione watu.” Akampangusa. Mwenyezi Mungu Akamrudishia macho yake. Akamuuliza. “Unapenda mali gani?” Akamjibu: “Mbuzi.” Akapewa mbuzi mwenye mtoto. Wale wenye ngamia na Ng’ombe wanyama wao wakazaa, na mwenye mbuzi nae akazalisha. Mmoja wao akawa na bonde lililojaa Ngamia, na mwengine ana bonde lililojaa Ng’ombe na huyu ana bonde lililojaa Mbuzi. Kisha, akamuendea mwenye ukoma katika sura yake na umbile lake (kama siku ile aliyokutana nae kwanza). Akamwambia: “Mimi ni masikini, rizki imenikatikia safarini, sina njia leo, (sina matumaini) isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu kisha kwako. Nakuomba kwa Ambaye Amekupa rangi nzuri, ngozi nzuri na mali, unipe Ngamia ili nimalize safari yangu.” Akamjibu: “Haki zipo nyingi (nina majukumu mengi, kwa hiyo siwezi kukusaidia). Akamwambia: “Kana kwamba nakujua, si ulikuwa na ukoma na watu wanakudharau na ulikuwa fukara, na Mwenyezi Mungu Akakupa?” Akamwambia: “Mali hii nimerithi kutoka kwa mababu na mababu.” Akamwambia: “Ikiwa unasema uongo, Mwenyezi Mungu Akurudishe kama ulivyokuwa.” Akamuendea mwenye upara katika sura yake na umbile lake (kama siku ile aliyokutana naye kwa mara ya kwanza). Akamwambia kama alivyomwambia wa mwanzo. Naye akamrudishia jibu kama alivyomrudishia wa mwanzo. Akamwambia: “Ikiwa unasema uongo, Mwenyezi Mungu Akurudishe kama ulivyokuwa.” Akamuendea kipofu katika sura yake na umbile lake (kama siku ile aliyokutana naye kwa mara ya kwanza). Akamwambia: “Mimi ni masikini, rizki imenikatikia safarini, sina njia leo, (sina matumaini) isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu kisha kwako. Nakuomba kwa Ambaye Amekurudishia macho yako, unipe mbuzi ili nimalizie safari yangu.” Akamjibu: “Kwa hakika nilikuwa kipofu, Mwenyezi Mungu Akanirudishia kuona kwangu. Chukua unachotaka, na wacha unachotaka. Wa-Allaahi sikufanyia uzito kwa kitu ulichokichukua kwa Ajili ya Mwenyezi Mungu.” Akamwambia “Zuia mali yako. Hakika mumepewa mtihani. Hakika Mwenyezi Mungu Ameshakuridhia na Amewaghadhibikia wenzio wawili.]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim]


 شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.