BUSTANI YA WATU WEMA
قال العلماء: التوبة واجبة مِنْ كل ذنب. فإن كانت المعصية بين العبد وبين اللَّه تعالى لا تتعلق بحق آدمي فلها ثلاثة شروط
أحدها: أن يقلع عَنْ المعصية
والثاني: أن يندم عَلَى فعلها
والثالث: أن يعزم أن لا يعود إليها أبدا؛
فإن فقد أحد الثلاثة لم تصح توبته
وإن كانت المعصية تتعلق بآدمي فشروطها أربعة: هذه الثلاثة وأن يبرأ مِنْ حق صاحبها. فأن كانت مالا أو نحوه رده إليه، وإن كان حد قذف ونحوه مكنه مِنْه أو طلب عفوه، وإن كانت غيبة استحله مِنْها. ويجب أن يتوب مِنْ جميع الذنوب، فإن تاب مِنْ بعضها صحت توبته عند أهل الحق مِنْ ذلك الذنب وبقى عليه الباقي.
وقد تظاهرت دلائل الكتاب والسنة وإجماع الأمة عَلَى وجوب التوبة
Wanachuoni wamesema: ni wajibu kutubia kwa kila dhambi anayoitenda mtu. na Madhambi yanapokuwa ni baina ya Mwenyezi Mungu ﷻ na mja wake yasiyofungamana na haki ya mwana Aadam, yana shuruti tatu:
1– Ajingoe na ile Dhambi
2– Ajute juu ya kutenda ile Dhambi
3– Aazimie kutoyarudia tena kabisa.
Moja katika shuruti hizo ikikosekana, basi Tawba yake haitosihi.
Na Madhambi yanapofungamana na haki ya mwanadamu, basi Masharti ya Tawba huwa ni nne: ni hizo tatu zilizotangulia
4– Na ya Nne ni: aregeshe haki ya mwenyewe; ikiwa ni mali na mfano wake amrejeshee, ikiwa ni haddi (adhabu) ya kutukana au mfano wake, atammakinisha au amuombe msamaha. Na ikiwa ni kusengenya basi atamuomba amhalalishie.
Na niwajibu mtu kutubia juu dhambi zote. na Akitubia baadhi yake, Tawba yake itasihi kutokana na dhambi ile kwa watu wa haki, na atabakiwa na dhambi nyinginezo.
Na zimekuja Dalili nyingi katika Qur’ani, na Sunna na ijmaa’ ya ummah juu ya uwajibu wa kutubia.
Amesema Mwenyezi mungu ﷻ:
{وتوبوا إِلَى اللَّه جميعا أيها المؤمنون لعلكم تفلحون}
[Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa.] [An Nuur:32]
Na Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ:
{استغفروا ربكم ثم توبوا إليه}
[Na ili mumwombe msamaha Mola wenu Mlezi, kisha mtubie kwake] [Huud:3]
Na Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ:
{يا أيها الذين آمنوا توبوا إِلَى اللَّه توبة نصوحا}
[Enyi mlio amini! Tubuni kwa Mwenyezi Mungu toba iliyo ya kweli!] [Attahrim:8]
شرح مقدمة الباب مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله