{"id":7426,"date":"2021-06-25T13:03:55","date_gmt":"2021-06-25T13:03:55","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=7426"},"modified":"2022-09-14T09:29:08","modified_gmt":"2022-09-14T09:29:08","slug":"ukoo-wa-bwana-mtume-%ef%b7%ba","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/ukoo-wa-bwana-mtume-%ef%b7%ba\/","title":{"rendered":"UKOO WA BWANA MTUME \ufdfa"},"content":{"rendered":"<h3 style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #993300;\"><strong>UKOO WA BWANA MTUME\u00a0\ufdfa<\/strong><\/span><\/h3>\n<hr \/>\n<p><strong><span style=\"font-size: 14pt; color: #000000;\"><span style=\"color: #008000;\">UKOO WA MTUME<\/span>\u00a0<span style=\"color: #008000; font-size: 18.6667px;\">\ufdfa.<\/span><\/span><\/strong><\/p>\n<p><span style=\"font-size: 18pt; color: #000000;\"><span style=\"font-size: 14pt;\">Ukoo wa Mtume wa Allaah <span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>\u00a0unajulikana kwa jina la Ukoo wa Haashim (Bani Haashim), na Haashim huyu ni babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu\u00a0<span style=\"font-size: 18.6667px; color: #008000;\">\ufdfa<\/span>\u00a0aliyekuwa mtu mkarimu sana mwenye kuheshimika miongoni mwa watu wa kabila lake, na kwa ajili hii alipewa yeye jukumu la kuwanywisha na kuwalisha mahujaji waliokuwa wakija kutufu Al-Ka\u2019aba, na hili lilikuwa ni jukumu adhimu sana analopewa mtu mwenye<\/span> <span style=\"font-size: 14pt;\">kuheshimika sana katika watu wa Makkah wakati ule.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size: 14pt; color: #000000;\">Haashim alikuwa mtu wa mwanzo kuwalisha mahujaji chakula maarufu kinachoitwa \u2018Thariyd\u2019, nacho ni mikate mikavu inayokatwakatwa na kuchanganywa na mchuzi wa nyama. Heshima ya chakula hiki katika kuwakaribisha wageni ni mfano wa heshima ya biriani katika jamii yetu.<\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size: 14pt; color: #000000;\">Jina lake hasa lilikuwa ni \u2018Amru, lakini alipewa jina hili la Haashim kwa sababu yeye mwenyewe ndiye aliyekuwa akiikatakata mikate mikavu kwa ajili ya kutayarisha chakula hicho cha \u2018Thariyd\u2019.<\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size: 14pt; color: #000000;\">Na neno \u2018Haashim\u2019 katika lugha ya Kiarabu maana yake ni kitu kikavu kilichokatikakatika.<\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size: 14pt; color: #000000;\">Allaah Anasema juu ya mimea ya ardhi:<\/span><\/p>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"font-size: 14pt; color: #008000;\">{\u0641\u064e\u0623\u064e\u0635\u0652\u0628\u064e\u062d\u064e \u0647\u064e\u0634\u0650\u064a\u0645\u064b\u0627 \u062a\u064e\u0630\u0652\u0631\u064f\u0648\u0647\u064f \u0627\u0644\u0631\u0651\u0650\u064a\u064e\u0627\u062d\u064f}<\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size: 14pt;\"><em><span style=\"color: #0000ff;\">[Mimea Ikawa majani makavu yaliyokatikatika ambayo upepo huyarusha huku na kule]<\/span><\/em>.<\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size: 14pt;\">Al-Kahf \u2013 45<\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size: 14pt;\"><span style=\"color: #000000;\">Imepokelewa kuwa Haashim alipokuwa akienda nchi ya Sham katika safari zake za kibiashara alipita Madina na alipokuwa hapo alimuoa Bibi mmoja aitwae<\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">Salma binti \u2018Amru<\/span> <span style=\"color: #000000;\">anayetokana na kabila la bani Najjar, akakaa naye muda wa siku chache kabla ya kuendelea na safari yake kwenda Sham na kumuacha Bibi Salma kwa wazee wake akiwa na mimba ya<\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">&#8220;Abdul-Muttwallib&#8221;<\/span> <span style=\"color: #000000;\">bila watu wake waliopo Makkah kujua.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size: 14pt;\"><span style=\"color: #000000;\">Wakati<\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">Haashim<\/span> <span style=\"color: #000000;\">alipokuwa safarini, Salma alimzaa &#8220;Abdul-Muttwallib&#8221;, lakini Haashim hakuweza kurudi kwani alifariki dunia akiwa Gaza nchi ya Palastina.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size: 14pt;\"><span style=\"color: #000000;\">&#8220;Abdul-Muttwallib&#8221; alizaliwa katika mwaka wa 497 baada ya Nabii \u2018Isa (Alayhis Salaam) na akapewa jina la<\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">Shaybatul Hamd<\/span> <span style=\"color: #000000;\">kutokana na unywele mmoja wa mvi aliokuwa nao kichwani, kwa sababu neno \u2018Shaybah\u2019 katika lugha ya Kiarabu maana yake ni mvi.<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size: 14pt; color: #000000;\">Bibi Salma aliyekuwa akiishi nyumbani kwa baba yake huko Madina alimlea mwanawe \u2018Abdul-Muttwallib malezi bora.<\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size: 14pt;\">Haashim alikuwa na watoto wa kiume wanne, watatu walikuwa Makkah na mmoja ambaye ni &#8220;<span style=\"color: #ff6600;\">Abdul-Muttwallib<\/span> <span style=\"color: #000000;\">aliyekuwa Madina kwa mama yake, na majina yao ni;<\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">Asad<\/span> <span style=\"color: #000000;\">na<\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">Abu Sayf<\/span> <span style=\"color: #000000;\">na<\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">Nadhlah<\/span> <span style=\"color: #000000;\">na<\/span>\u00a0&#8220;<span style=\"color: #ff6600;\">Abdul-Muttwallib<\/span>, <span style=\"color: #000000;\">na alikuwa na watoto wa kike watano nao ni<\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">Ash-Shifaa<\/span> <span style=\"color: #000000;\">na<\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">Khaalidah<\/span> <span style=\"color: #000000;\">na<\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">Dhaifah<\/span> <span style=\"color: #000000;\">na<\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">Ruqayyah<\/span> <span style=\"color: #000000;\">na<\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">Jannah<\/span>.<\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size: 14pt; color: #000000;\">Jamaa zake walioko Makkah hawakuwa na habari zozote juu ya ndugu yao \u2018Abdul-Muttwallib aliyekuwepo Madina, lakini habari zilimfikia Al Muttwallib ndugu yake Haashim ambaye ni ami yake \u2018Abdul-Muttwallib aliyeifunga safari ya kwenda Madina kumchukua mtoto wa ndugu yake.<\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size: 14pt; color: #000000;\">Al-Muttwallib alilia sana alipomuona \u2018Abdul-Muttwallib, akambeba na kumbusu na kumkumbatia huku akilia kwa furaha, kisha akamtaka ende naye Makkah, lakini \u2018Abdul-Muttwallib alikataa na kumwambia kuwa hawezi kuondoka bila ya ruhusa ya mama yake.<\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size: 14pt; color: #000000;\">Mama yake alikubali baada ya kuombwa sana na kushikiliwa, lakini alipotakiwa na yeye afuatane nao Makkah alikataa na akachagua kubaki kwa wazee wake hapo Madina.<\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size: 14pt; color: #000000;\">Al-Muttwallib aliingia Makkah akiwa amempakia \u2018Abdul-Muttwallib juu ya ngamia na watu walipomuona walikuwa wakisema:<\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size: 14pt; color: #000000;\">\u201cHuyu hapa \u2018Abdul-Muttwallib!\u201d<\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size: 14pt; color: #000000;\">Al-Muttwallib akawa anasema:<\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size: 14pt; color: #000000;\">&#8220;Ole wenu! Huyu ni mwana wa ndugu yangu Haashim.&#8221;<\/span><\/p>\n<p><span style=\"font-size: 14pt;\"><span style=\"color: #000000;\">Akamlea nyumbani kwake mpaka alipokuwa mkubwa, na Al-Muttwallib alipofariki akiwa safarini katika nchi ya<\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">Yemen<\/span> <span style=\"color: #000000;\">mji wa<\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">Radman<\/span>, <span style=\"color: #000000;\">watu wakamchagua \u2018Abdul-Muttwallib kuwa kiongozi wao, akawa anatenda yale wazee wake waliyokuwa wakitenda katika heshima ya kuwalisha na kuwanywisha mahujaji. Alikuwa mkarimu sana na watu wake wakampa jina la &#8220;Al-Fayaadh&#8221; na maana yake ni &#8220;Mkarimu sana&#8221; akapata heshima kubwa sana asiyowahi kupata yeyote katika wazee wake waliotangulia na watu wake wakampenda sana na kumtukuza. [1]<\/span><\/span><\/p>\n<hr \/>\n<p><span style=\"font-size: 12pt;\"><span style=\"color: #0000ff;\">[1]<\/span>\u00a0<span style=\"color: #0000ff;\">Ar-Rahiyq Al-Makhtuum \u2013 uk.40<\/span><\/span><\/p>\n<hr \/>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>UKOO WA BWANA MTUME\u00a0\ufdfa UKOO WA MTUME\u00a0\ufdfa. Ukoo wa Mtume wa Allaah \ufdfa\u00a0unajulikana kwa jina la Ukoo wa Haashim (Bani Haashim), na Haashim huyu ni babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu\u00a0\ufdfa\u00a0aliyekuwa mtu mkarimu sana mwenye kuheshimika miongoni mwa watu wa kabila lake, na kwa ajili hii alipewa yeye jukumu la kuwanywisha na kuwalisha mahujaji waliokuwa [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":15476,"comment_status":"open","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[57],"tags":[],"class_list":["post-7426","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-sera-ya-mtume"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/7426","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=7426"}],"version-history":[{"count":3,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/7426\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":15544,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/7426\/revisions\/15544"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/15476"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=7426"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=7426"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=7426"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}