{"id":5646,"date":"2021-06-21T22:03:12","date_gmt":"2021-06-21T22:03:12","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=5646"},"modified":"2022-08-25T19:49:56","modified_gmt":"2022-08-25T19:49:56","slug":"sharti-za-kusihi-adhana","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/sharti-za-kusihi-adhana\/","title":{"rendered":"SHARTI ZA KUSIHI ADHANA"},"content":{"rendered":"<h3><span style=\"color: #993300;\">SHARTI ZA KUSIHI ADHANA<\/span><\/h3>\n<p>Ili adhana iweze kusihi na kuzingatiwa kisheria kuwa ni adhana kumeshurutizwa kupatikana sharti zifuatazo:-<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">1.<\/span>\u00a0Muadhini awe ni Muislamu, mwanamume, mwenye akili.<\/p>\n<p>Haisihi Adhana ya Kafiri na wala haikubaliwi Adhana yake,na vile vile haisihi Adhana ya Mwanamke na Mtoto ndogo asiefikisha miaka ya kuweza kupambanuwa.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">2.<\/span>\u00a0Adhana ilingane na mpango uliowekwa.<\/p>\n<p>Ni sharti matamko ya adhana yaletwe kwa mtungo na utaratibu wake kama yalivyopokewa kutoka kwa Bwana Mtume\u00a0<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>.<\/p>\n<p>Hii ni kwa sababu kuacha utaratibu kunatuhumisha kufanya mchezo na kupunguza uzito wa tangazo hili la kuingia kwa wakati wa swala.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">3.<\/span>\u00a0Iwe ni yenye kufuatanishwa, kusiwe na mwanya mrefu baina ya maneno yake.<\/p>\n<p>Ni sharti upatikane mfululizo baina ya matamko ya adhana, kiasi cha kutopatikana mwanya mkubwa baina ya tamko la kwanza na lile la linalofuatia.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">4.<\/span>\u00a0Iwe ni pale unapoingia wakati wa Swala.<\/p>\n<p>Na hili linatokana na kauli ya Bwana Mtume\u00a0\ufdfa:<\/p>\n<p dir=\"rtl\" style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">[\u0648\u0625\u0630\u0627 \u062d\u0636\u0631\u062a \u0627\u0644\u0635\u0644\u0627\u0629 \u0641\u0644\u064a\u0624\u0630\u0646 \u0644\u0643\u0645 \u0623\u062d\u062f\u0643\u0645]\u00a0 \u00a0<span style=\"color: #ff6600;\"> \u0645\u062a\u0641\u0642 \u0639\u0644\u064a\u0647<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\">[Itakapohudhuria swala, basi na akuadhinieni mmoja wenu].\u00a0 \u00a0\u00a0<span style=\"color: #008000;\">[Imepokewa na Bukhari na Muslim]<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">5.\u00a0<\/span>Iwe ni kwa Lugha ya Kiarabu<\/p>\n<p>Ni sharti matamko yote ya adhana yaletwe kwa lugha ya Kiarabu kama yalivyopokelewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu<span style=\"color: #008000;\">\u00a0\ufdfa<\/span>.<\/p>\n<p>Haijuzu kutolewa adhana kwa lugha nyingine yo yote isiyo Kiarabu, kwani hiyo haitakuwa adhana bali tarjamah (tafsiri ya neno kwa neno) ya adhana<\/p>\n<p><span style=\"color: #993300;\"><strong>TANBIHI<\/strong>:<\/span><\/p>\n<p>Haikusuniwa adhana kwa jamaa ya wanawake, kwa sababu ya fitina inayoweza kupatikana kutokana na kusikilizika sauti zao na wanamume.<\/p>\n<p>Iliyosuniwa kwao ni Iqaama tu, kwa sababu hekima yake ni kuwainua waliohudhuria swala kuswali. Na haina kuinua sauti kama ilivyo kwa adhana.<\/p>\n<hr \/>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>SHARTI ZA KUSIHI ADHANA Ili adhana iweze kusihi na kuzingatiwa kisheria kuwa ni adhana kumeshurutizwa kupatikana sharti zifuatazo:- 1.\u00a0Muadhini awe ni Muislamu, mwanamume, mwenye akili. Haisihi Adhana ya Kafiri na wala haikubaliwi Adhana yake,na vile vile haisihi Adhana ya Mwanamke na Mtoto ndogo asiefikisha miaka ya kuweza kupambanuwa. 2.\u00a0Adhana ilingane na mpango uliowekwa. Ni sharti [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":14705,"comment_status":"open","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[69],"tags":[],"class_list":["post-5646","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-mlango-wa-swala"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/5646","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=5646"}],"version-history":[{"count":5,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/5646\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":14739,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/5646\/revisions\/14739"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/14705"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=5646"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=5646"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=5646"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}