{"id":4847,"date":"2021-06-17T21:31:35","date_gmt":"2021-06-17T21:31:35","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=4847"},"modified":"2023-05-10T08:16:17","modified_gmt":"2023-05-10T08:16:17","slug":"kusilimu-kwa-umar-ibn-al-khattwab-r-a","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/kusilimu-kwa-umar-ibn-al-khattwab-r-a\/","title":{"rendered":"KUSILIMU KWA &#8216;UMAR IBN AL KHATTWAB (R.A.)"},"content":{"rendered":"<h4><span style=\"color: #993300;\">KUSILIMU KWA \u2018UMAR IBN AL KHATTWAB (R.A.)<\/span><\/h4>\n<p>Alipotumilizwa Mtume\u00a0\ufdfa\u00a0na kutangaza Uislamu kwa watu, basi waliingia wenye kuingia katika Uislamu. Na miongoni mwao katika\u00a0jamii yake ni dada yake \u2018Umar (r.a.) ambaye ni Fatimah na mtoto\u00a0wa Ammi yake ambaye ni shemeji yake Sa\u2019id ibn Zaid, na Nu\u2019aym\u00a0ibn Abdullah; na wengine kutoka katika Bani Adiy. Ama \u2018Umar (r.a.)\u00a0wakati huo alikuwa hajasilimu, na alikuwa mwenye kushikamana na\u00a0itikadi yake ya kijahilia, akifanya uadui wa kuupinga Uislamu jambo\u00a0ambalo alilolitoa kutoka kwa mjomba wake Abu Jahl. Na alikuwa\u00a0katika watu ambao wanapinga kuendelea kwa Uislamu, na akiwaudhi\u00a0ambao wameingia katika Uislamu na kuwapiga watumwa na\u00a0madhaifu kati yao.<\/p>\n<p>Na Mtume\u00a0\ufdfa\u00a0alikuwa amemuomba\u00a0Mwenyezi Mungu amuongoze \u2018Umar katika Uislamu. Amepokea\u00a0Tirmidhi kutoka kwa ibn \u2018Umar (r.a.) kwamba Mtume\u00a0\ufdfa\u00a0amesema:<\/p>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">[\u0627\u0644\u0644\u0647\u0645 \u0623\u0639\u0632 \u0627\u0644\u0625\u0633\u0644\u0627\u0645 \u0628\u0623\u062d\u0628 \u0647\u0630\u064a\u0646 \u0627\u0644\u0631\u062c\u0644\u064a\u0646 \u0625\u0644\u064a\u0643]<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\">[Ewe Mola upe nguvu Uislamu kupitia kwa mmoja\u00a0unayempenda zaidi katika watu wawili hawa]<\/span>\u00a0\u2018Umar ibn AI-Khattab\u00a0au Abu Jahl ibn Hisham. Ikawa apendwaye zaidi na Mwenyezi Mungu\u00a0ni \u2018Umar.\u00a0[At- Tirmidhi Juz.2\/209]<\/p>\n<p>Alitoka \u2018Umar (r.a.) siku moja huku akishika upanga wake,\u00a0akikusudia kwenda kumuuwa Mtume\u00a0\ufdfa. Akakutana njiani na\u00a0Nu\u2019aym ibn \u2018Abdullah\u00a0(r.a.), wakajadiliana, akageuza safari yake\u00a0akaelekea hadi nyumbani kwa shemeji yake\u00a0Sa\u2019id ibn Zaid\u00a0akiwa\u00a0pamoja na mkewe\u00a0Fatimah (r.a.), ambaye ni dada yake \u2018Umar (r.a.).\u00a0Akawapata wanasoma ukurasa ambao ndani yake kuna Surat Twahaa.<\/p>\n<p>Akawapiga na kuwajeruhi mpaka wakasema:\u00a0\u201cNdio tumesilimu na\u00a0tumemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, fanya utakalo.\u201d\u00a0Baada ya kusikia maneno hayo \u2018Umar akaathirika, akautaka ule\u00a0ukurasa ambao walikuwa wakiusoma, dada yake akakataa kumpa\u00a0akamwambia: \u201cSisi tunachelea kukupa huo ukurasa.\u201d Akajibu \u2018Umar\u00a0kumwambia dada yake: \u201cUsiogope\u201d na akaapa kuwa hatafanya\u00a0ubaya. Akatumai dada yake kuwa huenda akasilimu akamwambia:\u00a0\u201cEwe kaka yangu hakika wewe ni najisi kwa ajili ya shirki yako, na\u00a0huu ukurasa hauguswi ila na aliyetahirika.\u201d\u00a0Akaenda \u2018Umar kuoga\u00a0kisha dada yake akampa ule ukurasa, akausoma. Kisha akasema:\u00a0\u201cNi uzuri ulioje wa maneno haya!\u201d Kisha akaenda mpaka kwenye\u00a0nyumba ya Al-Arqam ibn Al-Arqam, huko Safaa ambako ni makao ya\u00a0Mtume\u00a0\ufdfa\u00a0na Masahaba wake. Alipowasili \u2018Umar (r.a.) akasema\u00a0kumwambia Mtume \ufdfa\u00a0\u201cEwe Mtume wa Allah nimekujia nipate\u00a0kumwamini Allah na Mtume Wake pamoja na yale yaliokuja kutoka\u00a0kwa Allah.\u201d<\/p>\n<p>Mtume\u00a0\ufdfa\u00a0akapiga Takbir ambayo iliwajulisha watu wa nyumba ile kuwa \u2018Umar amesilimu. Alisilimu \u2018Umar baada ya Hamzah kwa\u00a0siku tatu, mwishoni mwa Mwezi wa Mfungo Tatu mwaka wa sita\u00a0kutoka kutumilizwa Mtume\u00a0\ufdfa\u00a0 Na \u2018Abdullah Ibn Mas\u2019ud\u00a0alikuwa akisema:\u00a0\u201cHatukuwa tukiweza kusali Al-Ka\u2019ba mpaka\u00a0aliposilimu \u2018Umar ibn AI-Khattab, aliposilimu aliwapiga vita\u00a0Maquraish mpaka akaweza kusali kwenye Al-Ka\u2019ba na tukasali\u00a0pamoja naye.\u201d<\/p>\n<p>Na imepokewa kuwa Mtume\u00a0\ufdfa\u00a0alitoka siku moja na Masahaba\u00a0zake katika safu mbili, Umar (r.a.) akiwa mbele ya safu moja na\u00a0Hamzah (r.a.) akiwa mbeie ya safu hiyo nyingine mpaka wakaingia\u00a0msikitini, \u2018Umar na Hamzah wakafika kwa Maquraish. Maquraish\u00a0wakawaangalia na kupatwa na huzuni ambayo haijawahi kuwapata.\u00a0Mtume\u00a0\ufdfa\u00a0akamwita \u2018Umar kuanzia siku hiyo Al-Faruq.<\/p>\n<p>Pamoja na kuwa \u2018Umar (r.a.) alikuwa ni mtu mwenye utisho na ni\u00a0mwamba, pia hakuwa mwenye kunusurika na mateso ya Ma\u2019quraish\u00a0mpaka wakaweza kumshambulia wakawa wanampiga nave\u00a0akiwapiga, mpaka \u2018Umar (r.a.) akachoka kupigana nao na akakaa\u00a0chini, wakamsimamia Maquraish na kumpiga kichwani na huku<\/p>\n<p>akiwaambia: \u201cFanyeni mtakacho, naapa kwaMwenyezi Mungu, lau\u00a0si si walstamu tungekuwa idadi yetu mia tatu, hakika si si\u00a0tungewaachia nyinyi huu mji au nyinyi mungetuachia sisi .\u201d\u00a0[Sirat\u00a0Ibn Hisham 1\/474]<\/p>\n<blockquote><p>*Al Khulafaau Arrashidun 59-61<\/p><\/blockquote>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>KUSILIMU KWA \u2018UMAR IBN AL KHATTWAB (R.A.) Alipotumilizwa Mtume\u00a0\ufdfa\u00a0na kutangaza Uislamu kwa watu, basi waliingia wenye kuingia katika Uislamu. Na miongoni mwao katika\u00a0jamii yake ni dada yake \u2018Umar (r.a.) ambaye ni Fatimah na mtoto\u00a0wa Ammi yake ambaye ni shemeji yake Sa\u2019id ibn Zaid, na Nu\u2019aym\u00a0ibn Abdullah; na wengine kutoka katika Bani Adiy. Ama \u2018Umar (r.a.)\u00a0wakati [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":20175,"comment_status":"open","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[64],"tags":[],"class_list":["post-4847","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-umar-ibn-al-khattab"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4847","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=4847"}],"version-history":[{"count":5,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4847\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":20182,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4847\/revisions\/20182"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/20175"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=4847"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=4847"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=4847"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}