{"id":4835,"date":"2021-06-17T21:19:13","date_gmt":"2021-06-17T21:19:13","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=4835"},"modified":"2023-05-10T08:30:23","modified_gmt":"2023-05-10T08:30:23","slug":"maisha-ya-sayyidna-ali-katika-uhai-wa-mtume-%ef%b7%ba","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/maisha-ya-sayyidna-ali-katika-uhai-wa-mtume-%ef%b7%ba\/","title":{"rendered":"MAISHA YA SAYYIDNA ALI KATIKA UHAI WA MTUME \ufdfa"},"content":{"rendered":"<h4><span style=\"color: #993300;\">MAISHA YAKE KATIKA UHAI WA MTUME\u00a0<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span><\/span><\/h4>\n<p>Mtume\u00a0\ufdfa\u00a0alimuoza \u2018Ali (r.a.) binti yake,\u00a0Fatimah\u00a0(r.a.), katika\u00a0mwaka wa pili wa hijra. Akamtayarishia nguo laini na mto wa ngozi\u00a0ambao uliwekwa majani ndani yake. Na yalikuwa maisha ya \u2018Ali\u00a0(r.a.) na mkewe ni ya kupa nyongo ulimwengu na niya kimaskini na\u00a0ya kusubiri.\u00a0[Al-Murtadha uk. 40]<\/p>\n<p>Ali (r.a.) alikuwa pamoja na Mtume \ufdfa katika vita vya Badri.Na mapambano yake na Al-Walid ibn \u2018Utbah maarufu.<\/p>\n<p>Pia alikuwa\u00a0\u00a0pamoja na Mtume \ufdfa katika vita vya Uhud. Na katika vita vya\u00a0Khandaq, \u2018Ali (r.a.) alipambana na \u2018Amru ibn \u2018Abdu-Wudd ambaye\u00a0akilinganishwa na wapiganaji elfu moja kwa ushujaa wake. \u2018Ali (r.a.)\u00a0alimuua.Na katika vita vya Al-Hudaybiyyah, \u2018Ali (r.a.) alikuwa\u00a0mwandishi wa Waraka wa Sulhu. Na katika vita vya Khaybar, \u2018Ali\u00a0(r.a.) alishika bendera ya jeshi la Walslamu. Na\u00a0akamuu wamwamba\u00a0wa Wayahudi aitwaye Murahhab. Na \u2018Ali (r.a.) aliwahi kuinua lango la ngome moja, ambalo huinuliwa na watu arubaini.\u00a0[Al-Bidayah\u00a0Wan-Nihayah Juz. 7 uk. 225]<\/p>\n<p>Ali (r.a.) hakushiriki katika vita vya Tabuk kwa sababu alimwakilisha\u00a0Mtume \ufdfa kwa Ahli yake katika mji wa Madinah. \u2018Ali (r.a.)\u00a0akamshtakia Mtume \ufdfa kuwa wanafiki wanasema maneno\u00a0mengi kuhusu yeye. Mtume (s.a.w.) akamwambia kwa kumtuliza:<\/p>\n<p dir=\"rtl\" style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">[\u0623\u0644\u0627 \u062a\u0631\u0636\u0649 \u0623\u0646 \u062a\u0643\u0648\u0646 \u0645\u0646\u064a \u0628\u0645\u0646\u0632\u0644\u0629 \u0647\u0627\u0631\u0648\u0646 \u0645\u0646 \u0645\u0648\u0633\u0649 \u060c \u0625\u0644\u0627 \u0623\u0646\u0647 \u0644\u064a\u0633 \u0646\u0628\u064a \u0628\u0639\u062f\u064a]<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\">[Je, wewe huridhiki kuwa daraja yako kwangu mimi ni kama vile\u00a0Harun kwa\u00a0Musa,\u00a0isipokuwa hakuna Mtume baada yangu.]\u00a0 \u00a0 \u00a0[AI-\u00a0Bidayah Wan-Nihayah Juz. 7 uk.\u00a0225]<\/span><\/p>\n<p>Mtume \ufdfa alimpeleka Khalid ibn Al-Walid (r.a.) pamoja na\u00a0Waislamu wengine kwa wakazi wa Yaman awalinganie katika\u00a0Uislamu, wakakaa huko kwa muda wa miezi sita, ila Wayaman\u00a0walikataa Kusilimu. Kisha Mtume \ufdfa akampeleka \u2018Ali (r.a.),\u00a0akawasomea barua ya Mtume \ufdfa . Wakasilimu watu wote wa\u00a0kabila ya Hamadan. \u2018Ali (r.a.) akamuandikia Mtume\u00a0\ufdfa\u00a0kumjulisha kuhusu kusilimu kwao. Khabari hizo zilipomfikia Mtume\u00a0(s.a.w.)\u00a0akasujudu kwa furaha, kisha akainua kichwa chake\u00a0akisema: \u201cAmani iwe juu ya Hamadan, amani iwe juu ya Hamadan.\u201d\u00a0(Zad AI-Ma\u2019ad Juz. 2 uk. 33)<\/p>\n<p>Abu Bakr (r.a.) alipotumwa kuwa amiri wa Hijja na Mtume (s.a.w.) katika mwaka 9H, kisha baadaye akaenda \u2018Ali (r.a.) na aya za Qur\u2019ani kutoka Suratut-Taubah akawasomea watu siku ya kuchinja; basi Abu Bakar (r.a.) aliendelea kuwaongoza watu katika Hijja, ilipofika siku ya kuchinja alisimama \u2018Ali (r.a.) akawasomea watu aya hizo. Kisha akatangaza kuwa kafiri hataingia Peponi, na baada ya mwaka huu si ruhusa kwa mshiriki yeyote kuhiji. Pia hairuhusiwi kutufu uchi kwenye Al-Ka\u2019bah. Na mwenye mkataba wowote na Mtume (s.a.w.) basi utadumu mkataba wake mpaka umalizike muda wake. (Ibn Hisham Juz. 2 uk. 543)<\/p>\n<p>Alipofariki Mtume (s.a.w.) \u2018Ali (r.a.) alimuosha pamoja na \u2018ammi\u00a0yake \u2018Abbas (r.a.) na watoto wa \u2018Abbas: Al-Fadhl na Qutham,\u00a0wakiwa pamoja na Shuqrah mtumwa wa Mtume (s.a.w.) na Usamah\u00a0ibn Zaid, na \u2018Aus ibn Khaulah. Na walisimamia mazishi ya Mtume\u00a0(s.a.w.).<\/p>\n<blockquote><p>*Khulafaau Arrashidun 130-131<\/p><\/blockquote>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>MAISHA YAKE KATIKA UHAI WA MTUME\u00a0\ufdfa Mtume\u00a0\ufdfa\u00a0alimuoza \u2018Ali (r.a.) binti yake,\u00a0Fatimah\u00a0(r.a.), katika\u00a0mwaka wa pili wa hijra. Akamtayarishia nguo laini na mto wa ngozi\u00a0ambao uliwekwa majani ndani yake. Na yalikuwa maisha ya \u2018Ali\u00a0(r.a.) na mkewe ni ya kupa nyongo ulimwengu na niya kimaskini na\u00a0ya kusubiri.\u00a0[Al-Murtadha uk. 40] Ali (r.a.) alikuwa pamoja na Mtume \ufdfa katika vita [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":20191,"comment_status":"open","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[62],"tags":[],"class_list":["post-4835","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-ali-ibn-abi-twalib"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4835","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=4835"}],"version-history":[{"count":7,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4835\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":20195,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4835\/revisions\/20195"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/20191"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=4835"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=4835"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=4835"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}