{"id":4719,"date":"2021-06-17T15:45:02","date_gmt":"2021-06-17T15:45:02","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=4719"},"modified":"2021-12-10T20:48:27","modified_gmt":"2021-12-10T20:48:27","slug":"kutahadhari-na-uchawi-na-uganga","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/kutahadhari-na-uchawi-na-uganga\/","title":{"rendered":"KUTAHADHARI NA UCHAWI NA UGANGA"},"content":{"rendered":"<h3><span style=\"color: #800000;\">KUTAHADHARI NA UCHAWI NA UGANGA<\/span><\/h3>\n<p>Ndugu Muislamu katika Makala haya tutaelezea hukumu ya uchawi na uganga katika uislamu pia tutatoa tahadhari kwa watu kwenda kwa waganga na wapiga ramli na pia tuwabainishie hatari za waganga katika umma tutahimiza kuchukua sababu za kisheria.<br \/>\nNi kweli usiofichika ya kwamba watu wanapitia mitihani mbali mbali, kwa mfano mitihani ya kiuchumi, ya kiafya na pia ya kijamii na mitihani mingineo. Kwa hivyo kukabiliana na mitihani hii ni lazima sheria ichungwe na sababu za kisheria zifuatwe katika kutatua matatizo yoyote yanayomkabili Muislamu popote alipo hafai kwenda kinyume na sheria.<br \/>\nNdugu Muislamu hakika katika mitihani waliopewa watu leo, waume kwa wake, wakubwa kwa wadogo, isipokuwa walio rehemewa na Mwenyezi Mungu ni kwenda kwa waganga na watu wa ramli wanaokula mali ya watu kwa batili.<br \/>\nUnaweza kumuona kiongozi amefungamanishwa na mganga hafanyi jambo lolote isipokuwa kwa ushauri wake hata kama ushauri huo utaenda kinyume na dini ya kiislamu, na anahisi ndani ya moyo wake ya kwamba huyo mganga ndiye anayempa uongozi na anaweza kuuchukua uongozi huo.na Kusahau kabisa kuwa Mwenyezi Mungu (Subhanahu wa Ta&#8217;aala) Ndie mmiliki wa kila kitu,Mwenyezi Mungu Anasema:<\/p>\n<p dir=\"rtl\" style=\"text-align: right;\"><span style=\"color: #008000;\">\u0642\u064f\u0644\u0650 \u0627\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u064f\u0645\u0651\u064e \u0645\u064e\u0627\u0644\u0650\u0643\u064e \u0627\u0644\u0652\u0645\u064f\u0644\u0652\u0643\u0650 \u062a\u064f\u0624\u0652\u062a\u0650\u064a \u0627\u0644\u0652\u0645\u064f\u0644\u0652\u0643\u064e \u0645\u064e\u0646 \u062a\u064e\u0634\u064e\u0627\u0621\u064f \u0648\u064e\u062a\u064e\u0646\u0632\u0650\u0639\u064f \u0627\u0644\u0652\u0645\u064f\u0644\u0652\u0643\u064e \u0645\u0650\u0645\u0651\u064e\u0646 \u062a\u064e\u0634\u064e\u0627\u0621\u064f \u0648\u064e\u062a\u064f\u0639\u0650\u0632\u0651\u064f \u0645\u064e\u0646 \u062a\u064e\u0634\u064e\u0627\u0621\u064f \u0648\u064e\u062a\u064f\u0630\u0650\u0644\u0651\u064f \u0645\u064e\u0646 \u062a\u064e\u0634\u064e\u0627\u0621\u064f \u06d6 \u0628\u0650\u064a\u064e\u062f\u0650\u0643\u064e \u0627\u0644\u0652\u062e\u064e\u064a\u0652\u0631\u064f \u06d6 \u0625\u0650\u0646\u0651\u064e\u0643\u064e \u0639\u064e\u0644\u064e\u0649\u0670 \u0643\u064f\u0644\u0651\u0650 \u0634\u064e\u064a\u0652\u0621\u064d \u0642\u064e\u062f\u0650\u064a\u0631\u064c \u00a0 \u00a0 \u00a0\u0622\u0644 \u0639\u0645\u0631\u0627\u0646:26<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\"><em>[Sema ewe Mwenyezi Mungu Mfalme wa wafalme Unampa ufalme unaye mtaka na unampokonya ufalme unayemtaka na unamtukuza unayemtaka na Unamdhalilisha unayemtaka katika mkono wako kuna kheri. Hakika yako wewe juu ya kila kitu ni muweza]\u00a0<\/em>\u00a0\u00a0\u00a0[Al-Imraan: 26]<\/span><\/p>\n<p>Utaona mfanyabiashara hanunui wala hauzi isipokuwa kwa ushauri wa mganga ambaye amefungamanisha moyo wake na mganga huyo na hufanya lolote atakaloambiwa na mganga namna litakavyokuwa jambo lile.<br \/>\nUtapata mke anaetaka kumtawala mumewe kwa kiasi ambacho mume yule hatatamani mke mwengine isipokuwa yeye ataenda mke yule kwa mganga mchafu na atataka usaidizi, akisahau kuwa Mwenyezi Mungu ndie ambaye amejaalia mapenzi ya dhati baina ya mume na mke hii ndio hali yetu waja wa Mwenyezi Mungu isipokuwa aliyerehemewa na Mwenyezi Mungu.<br \/>\nNdugu katika imani ni vyema kila Muislamu kujuwa Hukmu ya kufanya hivyo,na kwamba Mwenyezi Mungu Amebainisha wazi katika Qur\u2019an tukufu kwamba kujifundisha uchawi ni ukafiri.<br \/>\nMwenyezi Mungu (Subhanahu wa Ta&#8217;aala)<\/p>\n<p dir=\"rtl\" style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">{\u0648\u064e\u0645\u064e\u0627 \u064a\u064f\u0639\u064e\u0644\u0651\u0650\u0645\u064e\u0627\u0646\u0650 \u0645\u0650\u0646\u0652 \u0623\u064e\u062d\u064e\u062f\u064d \u062d\u064e\u062a\u0651\u064e\u0649\u0670 \u064a\u064e\u0642\u064f\u0648\u0644\u064e\u0627 \u0625\u0650\u0646\u0651\u064e\u0645\u064e\u0627 \u0646\u064e\u062d\u0652\u0646\u064f \u0641\u0650\u062a\u0652\u0646\u064e\u0629\u064c \u0641\u064e\u0644\u064e\u0627 \u062a\u064e\u0643\u0652\u0641\u064f\u0631\u0652} \u0627\u0644\u0628\u0642\u0631\u0629:102<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\"><em>[Na hawamfundishi yoyote mpaka waseme hakika yetu sisi ni fitna usikufuru ]<\/em>\u00a0\u00a0[Al-Baqara: 102]<\/span><br \/>\nNa vile vile Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Amesema:<\/p>\n<p dir=\"rtl\" style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">{\u0648\u064e\u0644\u064e\u0627 \u064a\u064f\u0641\u0652\u0644\u0650\u062d\u064f \u0627\u0644\u0633\u0651\u064e\u0627\u062d\u0650\u0631\u064f \u062d\u064e\u064a\u0652\u062b\u064f \u0623\u064e\u062a\u064e\u0649\u0670} \u00a0 \u00a0 \u0637\u0647:69<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\"><em>[Na mchawi hafanikiwi popote afikapo.]\u00a0<\/em>\u00a0 \u00a0[Twaha: 69].<\/span><\/p>\n<p>Na amesema Mtume\u00a0\ufdfa:<\/p>\n<p dir=\"rtl\" style=\"text-align: right;\"><span style=\"color: #008000;\">\u0627\u062c\u062a\u0646\u0628\u0648\u0627 \u0627\u0644\u0633\u0628\u0639 \u0627\u0644\u0645\u0648\u0628\u0642\u0627\u062a))\u060c \u0642\u0627\u0644\u0648\u0627: \u064a\u0627 \u0631\u0633\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0644\u0647\u060c \u0648\u0645\u0627 \u0647\u0646\u061f \u0642\u0627\u0644: ((\u0627\u0644\u0634\u0631\u0643 \u0628\u0627\u0644\u0644\u0647\u060c \u0648\u0627\u0644\u0633\u062d\u0631\u060c \u0648\u0642\u062a\u0644 \u0627\u0644\u0646\u0641\u0633 \u0627\u0644\u062a\u064a \u062d\u0631\u0645 \u0627\u0644\u0644\u0647 \u0625\u0644\u0627 \u0628\u0627\u0644\u062d\u0642\u060c \u0648\u0623\u0643\u0644 \u0627\u0644\u0631\u0628\u0627\u060c \u0648\u0623\u0643\u0644 \u0645\u0627\u0644 \u0627\u0644\u064a\u062a\u064a\u0645\u060c \u0648\u0627\u0644\u062a\u0648\u0644\u064a \u064a\u0648\u0645 \u0627\u0644\u0632\u062d\u0641\u060c \u0648\u0642\u0630\u0641 \u0627\u0644\u0645\u062d\u0635\u0646\u0627\u062a \u0627\u0644\u0645\u0624\u0645\u0646\u0627\u062a \u0627\u0644\u063a\u0627\u0641\u0644\u0627\u062a \u00a0 \u00a0 \u00a0 \u00a0\u0645\u062a\u0641\u0642 \u0639\u0644\u064a\u0647<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\">[Jiupusheni na mambo saba yanayoangamiza, wakasema maswahaba: Ni yapi, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema Mtume \ufdfa: Kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na uchawi, na kuuwa nafsi aliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu ila kwa haki, na kula Ribaa, na kula mali ya yatima, na kukimbia vitani,(katika jihadi) na kuwasingizia kuwa wamezini wanawake waliojihifadhi walioghafilika tena waumini].\u00a0\u00a0<span style=\"color: #008000;\">[Imepokewa na Bukhari na Muslim]<\/span><\/span><br \/>\nAsema Aisha:Watu walimuuliza Mtume\u00a0\ufdfa\u00a0kuhusu uganga akasema: [Hao si chochote. Wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika hao wanazungumzia mambo mara nyingine kisha yanatokea kweli. Akasema Mtume\u00a0\ufdfa:<\/p>\n<p dir=\"rtl\" style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">[\u062a\u0650\u0644\u0652\u0643\u064e \u0627\u0644\u0652\u0643\u064e\u0644\u0650\u0645\u064e\u0629\u064f \u0627\u0644\u0652\u062d\u064e\u0642\u0651\u064f \u064a\u064e\u062e\u0652\u0637\u064e\u0641\u064f\u0647\u064e\u0627 \u0627\u0644\u0652\u062c\u0650\u0646\u0651\u0650\u064a\u0651\u064f \u060c \u0641\u064e\u064a\u064e\u0642\u0652\u0630\u0650\u0641\u064f\u0647\u064e\u0627 \u0641\u0650\u064a \u0623\u064f\u0630\u064f\u0646\u0650 \u0648\u064e\u0644\u0650\u064a\u0651\u0650\u0647\u0650 \u060c \u0648\u064e\u064a\u064e\u0632\u0650\u064a\u062f\u064f \u0641\u0650\u064a\u0647\u064e\u0627 \u0645\u0650\u0627\u0626\u064e\u0629\u064e \u0643\u064e\u0630\u0652\u0628\u064e\u0629\u064d]\u00a0 \u00a0 \u00a0\u0631\u0648\u0627\u0647 \u0645\u0633\u0644\u0645<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\">[Hilo ni neno la haki analolichukua jinni kisha akalitia katika sikio la rafiki yake naye kwa upande wake akachanganya neno hilo na maneno mia ya uongo].\u00a0 \u00a0 \u00a0<span style=\"color: #008000;\"> [Imepokewa na Muslim]<\/span><\/span><br \/>\nNa katika hadithi nyingine za kukataza uchawi na uganga. Mtume<br \/>\n\ufdfa:\u00a0amesema:<\/p>\n<p dir=\"rtl\" style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">[\u0645\u064e\u0646\u0652 \u0623\u064e\u062a\u064e\u0649 \u0643\u064e\u0627\u0647\u0650\u0646\u064b\u0627\u060c \u0623\u064e\u0648\u0652 \u0639\u064e\u0631\u0651\u064e\u0627\u0641\u064b\u0627\u060c \u0641\u064e\u0635\u064e\u062f\u0651\u064e\u0642\u064e\u0647\u064f \u0628\u0650\u0645\u064e\u0627 \u064a\u064e\u0642\u064f\u0648\u0644\u064f\u060c \u0641\u064e\u0642\u064e\u062f\u0652 \u0643\u064e\u0641\u064e\u0631\u064e \u0628\u0650\u0645\u064e\u0627 \u0623\u064f\u0646\u0652\u0632\u0650\u0644\u064e \u0639\u064e\u0644\u064e\u0649 \u0645\u064f\u062d\u064e\u0645\u0651\u064e\u062f\u064d \u0635\u0644\u0649 \u0627\u0644\u0644\u0647 \u0639\u0644\u064a\u0647 \u0648\u0633\u0644\u0645] \u00a0 \u0631\u0648\u0627\u0647 \u0623\u062d\u0645\u062f<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\">[Atakayeenda kwa mganga au mchawi akamuuliza na akamuamini kwa atakayosema basi amekufuru aliyoteremshiwa Mtume Muhammad rehma na amani zimfikie].\u00a0 \u00a0 \u00a0<span style=\"color: #008000;\"> [Imepokewa na Ahmad]<\/span><\/span><br \/>\nHadithi hii tukufu inatufundisha kwamba mtu yoyote atakaye kwenda kwa mganga kumuuliza kitu na akamuamini kwa atakayomwambia basi ametoka kabisa katika dini ya Uislamu. Ama hukumu ambayo inatakiwa aichukue kiongozi kwa atakayepatikana anafanya uchawi ni kukatwa shingo yake na kuuwawa kama ilivyothibiti katika maneno ya Maswahaba Mwenyezi Mungu awawie radhi; Tahadhari tunayoitoa ni kwamba haifai kwa Muislamu kuchukua hatua mikononi mwake isije ikaleta balaa na fujo miongoni mwa watu.<\/p>\n<p><span style=\"color: #993300;\">MADHARA YA WACHAWI NA WAGANGA KATIKA UMMA<\/span><\/p>\n<p>Baadhi ya madhara ya waganga na wachawi katika umma. Madhara hayo ni kama yafuatayo;<br \/>\n<span style=\"color: #ff6600;\">1.<\/span> Kufutika imani za wanaokwenda kwa waganga na kuwaamini kwa watakayo ambiwa kama ilivyo katika hadithi ya Mtume\u00a0\ufdfa\u00a0tuliyoitaja.<br \/>\n<span style=\"color: #ff6600;\">2.<\/span> Kukithiri vifo na au kuona makaburi yanafukuliwa au kuona baadhi ya viungo vya wanadamu kwa hawa waganga baada ya kuwaamrisha wafuasi wao wawaletee.<br \/>\n<span style=\"color: #ff6600;\">3.<\/span> Kuenea zina na machafu baina ya watu kwani ni wangapi katika waganga hufanya zina na wake za watu na wakaharibu ndoa za watu na wakafungua milango mikubwa ya shari.<br \/>\n<span style=\"color: #ff6600;\">4.<\/span> Kula mali za watu kwa njia ya batili kinyume na haki, kwani kila anachochukua mganga ni kwa kazi yake mbovu na anakula uchafu. Mtume\u00a0\ufdfa\u00a0amekataza kula thamani ya mbwa na mahari ya mzinifu na chumo la mganga.<br \/>\n<span style=\"color: #ff6600;\">5.<\/span> Kuwapoteza watu na kuwafanya watu kuwa na tabia mbaya na kuwazuia wao kutekeleza maamrisho ya Dini, kwani kuna wengine huacha swala zote au baadhi yake na wengine huzuiliwa kuoga janaba na wengine huzuiliwa kufanya mema bali huamrishwa kufanya mabaya.<br \/>\n<span style=\"color: #ff6600;\">6.<\/span> Kumkasirisha Mwenyezi Mungu na kusababisha adhabu yake. Alisema Zainab binti Jahshi kumwambia Mtume\u00a0\ufdfa:<\/p>\n<p dir=\"rtl\" style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">[\u0623\u064e\u0646\u064e\u0647\u0652\u0644\u0650\u0643\u064f \u0648\u064e\u0641\u0650\u064a\u0646\u064e\u0627 \u0627\u0644\u0635\u0651\u064e\u0627\u0644\u0650\u062d\u064f\u0648\u0646\u064e \u0642\u064e\u0627\u0644\u064e \u00ab \u0646\u064e\u0639\u064e\u0645\u0652 \u0625\u0650\u0630\u064e\u0627 \u0643\u064e\u062b\u064f\u0631\u064e \u0627\u0644\u0652\u062e\u064e\u0628\u064e\u062b\u064f]\u00a0 \u00a0 \u00a0 \u0631\u0648\u0627\u0647 \u0645\u0633\u0644\u0645<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\">[Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Je tunaweza kuangamizwa na kati yetu kuna watu wema? Akasema Mtume \ufdfa: Ndio, ukikithiri uchafu].\u00a0 \u00a0<span style=\"color: #008000;\"> [Imepokewa na Muslim]<\/span><\/span><\/p>\n<p>Na je kuna wachafu zaidi kuliko waganga waovu?.<br \/>\n<span style=\"color: #ff6600;\">7.<\/span> Kupata hasara duniani na kesho akhera.Amesema Mwenyezi Mungu (Subhanahu wa Ta&#8217;aala)<\/p>\n<p dir=\"rtl\" style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">{\u0648\u064e\u0644\u064e\u0627 \u064a\u064f\u0641\u0652\u0644\u0650\u062d\u064f \u0627\u0644\u0633\u0651\u064e\u0627\u062d\u0650\u0631\u064f \u062d\u064e\u064a\u0652\u062b\u064f \u0623\u064e\u062a\u064e\u0649\u0670} \u0637\u0647:69<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\"><em>[Na mchawi hafanikiwi popote afikapo.]\u00a0<\/em>\u00a0\u00a0[Twaha: 69].<\/span><\/p>\n<p>Asema\u00a0Sheikhul Islaam Ibn Taimia\u00a0Mwenyezi Mungu Amrehemu \u00abHivi ndivyo ilivyo.\u00a0Hakika ufuatiliaji unaonesha kwamba watu wakitegemea nyota hawafaulu. Si duniani bali vile vile kesho akhera.\u201d<br \/>\nHayo ndiyo baadhi ya madhara yanayopatikana kutoka kwa waganga waovu.<br \/>\nKwa hivyo, ni lazima ewe Muislamu kuelekea kwa Mwenyezi Mungu na watu wakumbushane kwamba jambo la kwenda kwa waganga na kuangaliliwa ni jambo baya na halifai. Jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu ni Mfalme na Mwenye kumiliki kila kitu, hana wa kumzuwia anapo toa. Ametuamrisha Mola Wetu tutakapo kuwa na tatizo lolote tumuombe Yeye na tumtake Yeye msaada, na yafaa tumtegemee yeye katika kila kitu na tuchukue sababu za kisheria katika kufikia tunayoyakusudia na miongoni mwa sababu hizo ni kumuomba Mwenyezi Mungu dua. Kwa hivyo, atakaemuomba kwa nia njema hakika Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa amali ya anayeomba. Mwenyezi Mungu yuko karibu na hujibu maombi na yeye ndiye anayeruzuku ndege porini na samaki baharini.Amesema Mwenyezi Mungu (Subhanau wa Ta&#8217;aala)<\/p>\n<p dir=\"rtl\" style=\"text-align: right;\"><span style=\"color: #008000;\">\u0627\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u064f \u0627\u0644\u0651\u064e\u0630\u0650\u064a \u062e\u064e\u0644\u064e\u0642\u064e \u0627\u0644\u0633\u0651\u064e\u0645\u064e\u0627\u0648\u064e\u0627\u062a\u0650 \u0648\u064e\u0627\u0644\u0652\u0623\u064e\u0631\u0652\u0636\u064e \u0648\u064e\u0623\u064e\u0646\u0632\u064e\u0644\u064e \u0645\u0650\u0646\u064e \u0627\u0644\u0633\u0651\u064e\u0645\u064e\u0627\u0621\u0650 \u0645\u064e\u0627\u0621\u064b \u0641\u064e\u0623\u064e\u062e\u0652\u0631\u064e\u062c\u064e \u0628\u0650\u0647\u0650 \u0645\u0650\u0646\u064e \u0627\u0644\u062b\u0651\u064e\u0645\u064e\u0631\u064e\u0627\u062a\u0650 \u0631\u0650\u0632\u0652\u0642\u064b\u0627 \u0644\u0651\u064e\u0643\u064f\u0645\u0652 \u06d6 \u0648\u064e\u0633\u064e\u062e\u0651\u064e\u0631\u064e \u0644\u064e\u0643\u064f\u0645\u064f \u0627\u0644\u0652\u0641\u064f\u0644\u0652\u0643\u064e \u0644\u0650\u062a\u064e\u062c\u0652\u0631\u0650\u064a\u064e \u0641\u0650\u064a \u0627\u0644\u0652\u0628\u064e\u062d\u0652\u0631\u0650 \u0628\u0650\u0623\u064e\u0645\u0652\u0631\u0650\u0647\u0650 \u06d6 \u0648\u064e\u0633\u064e\u062e\u0651\u064e\u0631\u064e \u0644\u064e\u0643\u064f\u0645\u064f \u0627\u0644\u0652\u0623\u064e\u0646\u0652\u0647\u064e\u0627\u0631\u064e \u0648\u064e\u0633\u064e\u062e\u0651\u064e\u0631\u064e \u0644\u064e\u0643\u064f\u0645\u064f \u0627\u0644\u0634\u0651\u064e\u0645\u0652\u0633\u064e \u0648\u064e\u0627\u0644\u0652\u0642\u064e\u0645\u064e\u0631\u064e \u062f\u064e\u0627\u0626\u0650\u0628\u064e\u064a\u0652\u0646\u0650 \u06d6 \u0648\u064e\u0633\u064e\u062e\u0651\u064e\u0631\u064e \u0644\u064e\u0643\u064f\u0645\u064f \u0627\u0644\u0644\u0651\u064e\u064a\u0652\u0644\u064e \u0648\u064e\u0627\u0644\u0646\u0651\u064e\u0647\u064e\u0627\u0631\u064e \u00a0 \u00a0 \u00a0\u0625\u0628\u0631\u0627\u0647\u064a\u0645:32-34<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\"><em>[Mwenyezi Mungu ambaye ameumba mbingu na ardhi na ameteremsha maji kutoka mbinguni akatoa kutokana na maji hayo matunda hali ya kuwa ni riziki kwenu na Amewadhalilishia meli ili itembee baharini kwa amri Yake na Akawadhalilishia mito na akawadhalilishia jua na mwezi zinazotembea na akawadhalilishia usiku na mchana na akawapa kila mnachoomba na endapo mutazihesabu neema za Mwenyezi Mungu hamuwezi kuzidhibiti hakika mwanadamu ni dhalimu aliye mkufuru Mwenyezi Mungu. ]<\/em>\u00a0[Ibrahiim:32-34]<\/span><\/p>\n<p dir=\"LTR\" style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #993300;\"><em>\u00a0SIKILIZA MADA HII NA SHEIKH SHADDADI ALI\u00a0<\/em><\/span><\/p>\n<p><audio style=\"display: block; margin: 9px auto;\" src=\"https:\/\/archive.org\/download\/KUTAHADHARINAWACHAWINAWAGANGA\/KUTAHADHARI%20NA%20WACHAWI%20NA%20WAGANGA.mp3\" controls=\"controls\"><\/audio><\/p>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>KUTAHADHARI NA UCHAWI NA UGANGA Ndugu Muislamu katika Makala haya tutaelezea hukumu ya uchawi na uganga katika uislamu pia tutatoa tahadhari kwa watu kwenda kwa waganga na wapiga ramli na pia tuwabainishie hatari za waganga katika umma tutahimiza kuchukua sababu za kisheria. Ni kweli usiofichika ya kwamba watu wanapitia mitihani mbali mbali, kwa mfano mitihani [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":12092,"comment_status":"open","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[96],"tags":[],"class_list":["post-4719","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-sehemu-ya-imani"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4719","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=4719"}],"version-history":[{"count":4,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4719\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":12094,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4719\/revisions\/12094"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/12092"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=4719"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=4719"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=4719"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}