{"id":4634,"date":"2021-06-16T23:11:17","date_gmt":"2021-06-16T23:11:17","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=4634"},"modified":"2023-06-21T12:34:37","modified_gmt":"2023-06-21T12:34:37","slug":"umuhimu-wa-kutafuta-ilimu-ya-dini","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/umuhimu-wa-kutafuta-ilimu-ya-dini\/","title":{"rendered":"UMUHIMU WA KUTAFUTA ILIMU YA DINI"},"content":{"rendered":"<h3 dir=\"LTR\"><span style=\"color: #993300;\"><strong>UMUHIMU WA KUTAFUTA ILIMU YA DINI<\/strong><\/span><\/h3>\n<p>Ilimu ni msingi muhimu katika dini ya Kiislamu. Dini ya Kiislamu imejengwa juu ya Ilimu. Kwasababu Ilimu ndio mwangaza wa kuonyesha njia ya sawa na kuonyesha njia ya mbaya. Aya za kwanza alizo teremshiwa Mtume Muhammad Swalla Llahu \u2018alayhi wasallam zilikuwa ni za kufundisha ilimu, na kuhimiza Waislamu wafanye bidii kutafuta ilimu. Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:<\/p>\n<p dir=\"rtl\" style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">{\u0627\u0642\u0652\u0631\u064e\u0623\u0652 \u0628\u0650\u0627\u0633\u0652\u0645\u0650 \u0631\u064e\u0628\u0651\u0650\u0643\u064e \u0627\u0644\u0651\u064e\u0630\u0650\u064a \u062e\u064e\u0644\u064e\u0642\u064e \u062e\u064e\u0644\u064e\u0642\u064e \u0627\u0644\u0652\u0625\u0650\u0646\u0633\u064e\u0627\u0646\u064e \u0645\u0650\u0646\u0652 \u0639\u064e\u0644\u064e\u0642\u064d \u0627\u0642\u0652\u0631\u064e\u0623\u0652 \u0648\u064e\u0631\u064e\u0628\u0651\u064f\u0643\u064e \u0627\u0644\u0652\u0623\u064e\u0643\u0652\u0631\u064e\u0645\u064f \u0627\u0644\u0651\u064e\u0630\u0650\u064a \u0639\u064e\u0644\u0651\u064e\u0645\u064e \u0628\u0650\u0627\u0644\u0652\u0642\u064e\u0644\u064e\u0645\u0650 \u0639\u064e\u0644\u0651\u064e\u0645\u064e \u0627\u0644\u0652\u0625\u0650\u0646\u0633\u064e\u0627\u0646\u064e \u0645\u064e\u0627 \u0644\u064e\u0645\u0652 \u064a\u064e\u0639\u0652\u0644\u064e\u0645\u0652}<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\"><em>[Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! Ambaye amefundisha kwa kalamu. Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui.]<\/em>\u00a0\u00a0\u00a0[Al-Alaq&#8221;1-5]<\/span><br \/>\nMwenyezi Mungu(Subhaanahu wa Taala)Ametumia katika Aya hizo maneno kama; soma, ilimu, kalamu, kufundisha, yote haya ni kuonyesha umuhimu wa kutafuta ilimu kwa kupitia njia tofauti za kuweza kukufikisha wewe kupata ilimu hio. Katika Aya hizo kuna ishara ya kuonyesha kwanza kabla ya kufanya vitendo vingine ni lazima mwanadamu apate ilimu ili aweze kutekeleza vitendo vyake kwa ujuzi zaidi na maarifa ya kutosha kinyume na mafundisho hayo, basi mwanadamu atafanya mambo kwa ujinga na baada ya kupata faida na mambo hayo, atapata hasara tupu ima kwa kudhuru nafsi yake au jamii kwa jumla.<br \/>\nWajibu wa kutafuta Ilimu kabla ya kila kitu katika Mafundisho ya Qur\u2019ani na Sunna<\/p>\n<p><span style=\"color: #993300;\">KATIKA QUR&#8217;ANI TUKUFU:<\/span><\/p>\n<p>Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala Amesema:<\/p>\n<p dir=\"rtl\" style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">{\u0641\u064e\u0627\u0639\u0652\u0644\u064e\u0645\u0652 \u0623\u064e\u0646\u0651\u064e\u0647\u064f \u0644\u064e\u0627 \u0625\u0650\u0644\u064e\u0670\u0647\u064e \u0625\u0650\u0644\u0651\u064e\u0627 \u0627\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u064f \u0648\u064e\u0627\u0633\u0652\u062a\u064e\u063a\u0652\u0641\u0650\u0631\u0652 \u0644\u0650\u0630\u064e\u0646\u0628\u0650\u0643\u064e \u0648\u064e\u0644\u0650\u0644\u0652\u0645\u064f\u0624\u0652\u0645\u0650\u0646\u0650\u064a\u0646\u064e \u0648\u064e\u0627\u0644\u0652\u0645\u064f\u0624\u0652\u0645\u0650\u0646\u064e\u0627\u062a\u0650 \u06d7 \u0648\u064e\u0627\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u064f \u064a\u064e\u0639\u0652\u0644\u064e\u0645\u064f \u0645\u064f\u062a\u064e\u0642\u064e\u0644\u0651\u064e\u0628\u064e\u0643\u064f\u0645\u0652 \u0648\u064e\u0645\u064e\u062b\u0652\u0648\u064e\u0627\u0643\u064f\u0645\u0652} \u00a0 \u00a0\u0645\u062d\u0645\u062f:19<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\"><em>[Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, na omba maghufira kwa dhambi zako na za Waumini wanaume na Waumini wanawake.]<\/em>\u00a0\u00a0\u00a0[ Mahammad:19]<\/span><br \/>\nAmesema Imam Bukhari katika kitabu chake Sahihi Al-Bukhari: &#8220;Mlango unaozungumzia kusoma ilimu kabla ya maneno na vitendo&#8221; Makusudio ya Imamu Bukhari ni kutafsiri Aya iliyotangulia ya kumaanisha ilimu mwanzo kabla ya vitendo. Ilimu imetangulizwa kwanza kabla ya kusema au kutenda, kwa sababu, ikiwa maneno na vitendo havikujengwa juu ya msingi wa Ilimu, maneno hayo na vitendo hivyo havina faida kwa mwenye kufanya. Khasara yake ni kubwa kuliko faida yake. Ndio Dini ya Kislamu kwanza ikatilia mkazo watu kusoma na kujuwa kabla ya kufanya vitendo.<br \/>\nAmesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:<\/p>\n<p dir=\"rtl\" style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">{\u0625\u0650\u0646\u0651\u064e\u0645\u064e\u0627 \u064a\u064e\u062e\u0652\u0634\u064e\u0649 \u0627\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u064e \u0645\u0650\u0646\u0652 \u0639\u0650\u0628\u064e\u0627\u062f\u0650\u0647\u0650 \u0627\u0644\u0652\u0639\u064f\u0644\u064e\u0645\u064e\u0627\u0621\u064f \u06d7 \u0625\u0650\u0646\u0651\u064e \u0627\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u064e \u0639\u064e\u0632\u0650\u064a\u0632\u064c \u063a\u064e\u0641\u064f\u0648\u0631\u064c} \u00a0 \u00a0 \u0641\u0627\u0637\u0631:28<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\"><em>[Kwa hakika wanao mcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wanazuoni.]\u00a0[Fatir:28]<\/em><\/span><\/p>\n<p>Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala Amesema:<\/p>\n<p dir=\"rtl\" style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">{\u0648\u064e\u062a\u0650\u0644\u0652\u0643\u064e \u0627\u0644\u0652\u0623\u064e\u0645\u0652\u062b\u064e\u0627\u0644\u064f \u0646\u064e\u0636\u0652\u0631\u0650\u0628\u064f\u0647\u064e\u0627 \u0644\u0650\u0644\u0646\u0651\u064e\u0627\u0633\u0650 \u06d6 \u0648\u064e\u0645\u064e\u0627 \u064a\u064e\u0639\u0652\u0642\u0650\u0644\u064f\u0647\u064e\u0627 \u0625\u0650\u0644\u0651\u064e\u0627 \u0627\u0644\u0652\u0639\u064e\u0627\u0644\u0650\u0645\u064f\u0648\u0646\u064e} \u00a0 \u00a0\u0627\u0644\u0639\u0646\u0643\u0628\u0648\u062a:43<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\"><em>[Na hiyo ni mifano tunawapigia watu, na hawaifahamu ila wenye ilimu.]<\/em>\u00a0\u00a0 \u00a0[Al-Ankabut:43]<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #993300;\">KATIKA SUNNA ZA MTUME \ufdfa<\/span><\/p>\n<p>Amesema Mtume\u00a0\ufdfa:<\/p>\n<p dir=\"rtl\" style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">[\u0645\u0646 \u0633\u0644\u0643 \u0637\u0631\u064a\u0642\u0627\u064b \u064a\u0644\u062a\u0645\u0633 \u0641\u064a\u0647 \u0639\u0644\u0645\u0627\u064b \u0633\u0647\u0644 \u0627\u0644\u0644\u0647 \u0644\u0647 \u0628\u0647 \u0637\u0631\u064a\u0642\u0627\u064b \u0625\u0644\u0649 \u0627\u0644\u062c\u0646\u0629] \u00a0 \u00a0<span style=\"color: #ff6600;\"> \u0631\u0648\u0627\u0647 \u0645\u0633\u0644\u0645<\/span><\/span><\/p>\n<p>[Mwenye kufuata njia kwa ajili ya kutafuta Ilimu. Mwenyezi Mungu atafanyia wepesi njia ya kuingia peponi ].\u00a0\u00a0\u00a0[Imepokewa na Muslim]<br \/>\nNa Amesema Mtume\u00a0\ufdfa\u00a0katika Hadithi nyingine:<\/p>\n<p dir=\"rtl\" style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">[\u0645\u064e\u0646\u0652 \u064a\u064f\u0631\u0650\u062f\u0650 \u0627\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u064f \u0628\u0650\u0647\u0650 \u062e\u064e\u064a\u0652\u0631\u064b\u0627 \u064a\u064f\u0641\u064e\u0642\u0651\u0650\u0647\u0652\u0647\u064f \u0641\u0650\u064a \u0627\u0644\u062f\u0651\u0650\u064a\u0646\u0650] \u00a0 \u00a0 <span style=\"color: #ff6600;\">\u00a0\u0631\u0648\u0627\u0647 \u0627\u0644\u0628\u062e\u0627\u0631\u064a \u0648\u0645\u0633\u0644\u0645<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\">[Mwenyezi Mungu akimtakia kheri mja wake humfundisha ilimu ya dini].\u00a0\u00a0<span style=\"color: #008000;\">\u00a0[Imepokewa na Bukhari na Muslim]<\/span><\/span><br \/>\nMuislamu hawezi Kufahamu Qur\u2019an na Sunna za Mtume ila kwa Ilimu. Ni lazima kwanza ajilazimishe na kusoma ili apate ujuzi wa kufahamu. Bila ya kufanya hivyo, atakuwa ni miongoni mwa waliosifiwa na sifa ya ujinga. Ndugu katika Imani, haya ndio mafundisho ya Allah na Mtume wake, yameweka wazi umuhimu wa kusoma kabla ya vitendo. Kwa hivyo, Allah (Subhaanahu wa Taala) hatokubali kwa mja wake ibada au vitendo vilivyo fanywa bila ya ilimu. Kwa sababu hio, ndio Sheria ya Kiislamu ikaamrisha Waislamu kusoma na ikawa hukumu ya kusoma ni wajibu juu ya kila Muislamu.<\/p>\n<p><span style=\"color: #993300;\">MAMBO YANAYO LAZIMU KATIKA KUTAFUTA ILIMU<\/span><\/p>\n<p>Kuwa na Ikhlasi, nayo ni kusoma kwa ajili ya Allah Subhaanahu wa Taala. Muislamu lazima awe na lengo kubwa katika kutafuta ilimu nalo ni kusoma kwa ajili ya kutaka raadhi za Allah Subhaanahu wa Taala. Malengo mengine yanakuja baadae. Lakini, la msingi ni kusoma kwa ajili ya Allah Subhaanahu wa Taala.<br \/>\nKuchunga haki za Mwalimu, kwa kumuheshimu na kumsikiliza vizuri wakati wa kusoma na kuuliza masuali kwa njia ya heshima.<br \/>\nKupanga mikakati ya kusoma, kwa kutanguliza ilimu ambayo ni muhimu sana,kabla ya nyingine, Mfano wa kusoma ilimu ya faradhi kabla ya ilimu ya sunna.<br \/>\nKufanyia kazi ilimu, na kuwa na hisia ya jukumu kubwa ulilo libeba. Na kujuwa ya kwamba utaenda kuulizwa ilimu yako mbele ya Allah. Je ulifanyia nini?<br \/>\nKufundisha watu. Ilimu ni amana kutoka kwa Allah (Subhaanahu wa Taala). Na ili tuweze kutekeleza amana hii kama anavyotaka Mwenyezi Mungu, ni lazima tufanye bidii ya kuwafundisha wengine wasio bahatika kusoma. Amesema Mtume\u00a0\ufdfa:<\/p>\n<p dir=\"rtl\" style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">[\u062e\u064a\u0631\u0643\u0645 \u0645\u0646 \u062a\u0639\u0644\u0645 \u0627\u0644\u0642\u0631\u0627\u0646 \u0648\u0639\u0644\u0645\u0647] \u00a0 \u00a0<span style=\"color: #ff6600;\">\u0623\u062e\u0631\u062c\u0647 \u0627\u0644\u0628\u062e\u0627\u0631\u064a<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\">[Mbora wenu, ni Yule aliye jifunza Qur\u2019ani na akafundisha]. \u00a0<span style=\"color: #008000;\">[ Imepokewa na Bukhari]<\/span><\/span><\/p>\n<p>Kwa hakika, ni jukumu kubwa juu ya wasomi kufanya bidii kuifundisha ilimu waliopewa na Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala.<\/p>\n<p style=\"text-align: center;\"><strong>KWA FAIDA ZAIDI SIKILIZA MADA NA HII NA SHEIKH HAMMAD QASIM<\/strong><audio style=\"display: block; margin: 9px auto;\" src=\"https:\/\/archive.org\/download\/KuhimizaKUtafutaIlimu\/Kuhimiza%20KUtafuta%20Ilimu.mp3\" controls=\"controls\"><\/audio><\/p>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>UMUHIMU WA KUTAFUTA ILIMU YA DINI Ilimu ni msingi muhimu katika dini ya Kiislamu. Dini ya Kiislamu imejengwa juu ya Ilimu. Kwasababu Ilimu ndio mwangaza wa kuonyesha njia ya sawa na kuonyesha njia ya mbaya. Aya za kwanza alizo teremshiwa Mtume Muhammad Swalla Llahu \u2018alayhi wasallam zilikuwa ni za kufundisha ilimu, na kuhimiza Waislamu wafanye [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":21065,"comment_status":"open","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[100],"tags":[],"class_list":["post-4634","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-sehemu-ya-yautangazaji"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4634","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=4634"}],"version-history":[{"count":6,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4634\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":21067,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4634\/revisions\/21067"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/21065"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=4634"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=4634"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=4634"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}