{"id":4622,"date":"2021-06-16T22:57:33","date_gmt":"2021-06-16T22:57:33","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=4622"},"modified":"2022-02-05T00:35:38","modified_gmt":"2022-02-05T00:35:38","slug":"vipi-tutaanza-malezi-bora-katika-jamii-zetu","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/vipi-tutaanza-malezi-bora-katika-jamii-zetu\/","title":{"rendered":"VIPI TUTAANZA MALEZI BORA KATIKA JAMII ZETU ?"},"content":{"rendered":"<h2><span style=\"color: #993300;\">VIPI TUTAANZA MALEZI BORA KATIKA JAMII ZETU ?<\/span><\/h2>\n<p>Hatua zifuatazo ni muhimu sana kila mmoja wetu azizingatie ili malezi yasiwe ni ya kubahatisha bali malezi yawe ya kitaalamu na kuwe na malengo ya wazi.Kwa hivyo ni muhimu wazazi wasome malezi yenyewe yanavyotakikana Kusomwa. Kusoma vitabu vya malezi na kumsoma Mtume\u00a0\ufdfa\u00a0alivyolea watoto wake na alivyofundisha malezi.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">1.\u00a0<\/span>Kujua namna ya kuchagua mshirika wako katika maisha.Siku zote yataka utazame na kufikiria kuhusu mke au mume mutakayesaidiana naye katika kulea watoto malezi bora.Mtu ambaye mtakuwa na malengo sawa katika malezi ya kufungamanisha kizazi na misingi imara ya Qur\u2019an na Sunnah.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">2.<\/span>\u00a0Kiwango cha maarifa cha mume na mke kiweze kukaribiana ili kuepuka matatizo mbeleni katika kutazama mambo na kuyapima.Mfano viwango vyenu vya masomo viwe vinalingana mfano mwenye shahada ya ndaki na mwenzake awe anakaribia hapo.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">3.<\/span>\u00a0Kuwe na ratiba za malezi na ushirikiano baina ya wanandoa lisiachwe jukumu hili kwa mtu mmoja.Mfano baba akifuatilia masomo basi mama ashughulike kwa kutengeneza mazingira mwafaka ya masomo nyumbani.<br \/>\n<span style=\"color: #ff6600;\">4.<\/span>\u00a0Wazazi wawe mfano mwema kwa watoto wao kwa tabia na wanavyojiweka.Wasitukanane au kutoleana sauti mbele ya watoto wao.Wazazi wawe kielelezo cha kufanya ibada ndani ya nyumba na baba naye ajibidiishe kuswali swala za sunnah ndani ya nyumba yake.Wazazi wasidhihirishe ubaya wao mbele ya watoto.Mfano baba au mama ana udhaifu wa urongo basi asiseme mbele ya watoto au uraibu wa miraa au sigara asiutumie wala kuwatuma watoto.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">5.<\/span>\u00a0Kuweka vikao vya mara kwa mara vya kifamilia ili kupeana nasiha baina ya wazazi na watoto.Wawashirikishe watoto katika baadhi ya mambo mepesi ya nyumabani na kuwataka ushauri kwa mambo hayo.Kuwasikiliza shida zao na mambo yanayowakereketa.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">6.\u00a0<\/span>Wazazi wawe waadilifu katika kuwapenda na kuwahudumia watoto wao.Wasiwabague watoto katika huduma muhimu kiasi cha watoto wenyewe kujua kuwa fulani anapendwa zaidi na wazazi kuliko sisi.Jambo hili hupanda chuki baina ya watoto na linaweza kusababisha maafa makubwa.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">7.<\/span>\u00a0Kufuatilia tabia za watoto wanapokua katika mabadiliko yanayopatikana katika mwili na hisia.Kuwa karibu nao na kuwapa mwongozo wa sawa kama wazazi.Kuwafanya wajue kuwa lengo si kuwanyima uhuru wao bali ni kuwaonyesha ya sawa ambayo yatajenga mustakabali wao.Mfano kumwamrisha mtoto kuswali anapotimu umri wa miaka saba na kumlazimisha anapofikisha miaka kumi na kumuadhibu anapokataa.Kama alivyo sema Bwana Mtume\u00a0\ufdfa:<\/p>\n<p dir=\"rtl\" style=\"text-align: right;\"><span style=\"color: #008000;\">[\u0645\u064f\u0631\u064f\u0648\u0627 \u0623\u064e\u0648\u0652\u0644\u0627\u062f\u064e\u0643\u064f\u0645\u0652 \u0628\u0650\u0627\u0644\u0635\u0651\u064e\u0644\u0627\u0629\u0650 \u0648\u064e\u0647\u064f\u0645\u0652 \u0623\u064e\u0628\u0652\u0646\u064e\u0627\u0621\u064f \u0633\u064e\u0628\u0652\u0639\u0650 \u0633\u0650\u0646\u0650\u064a\u0646\u064e \u060c \u0648\u064e\u0627\u0636\u0652\u0631\u0650\u0628\u064f\u0648\u0647\u064f\u0645\u0652 \u0639\u064e\u0644\u064e\u064a\u0652\u0647\u064e\u0627 \u0648\u064e\u0647\u064f\u0645\u0652 \u0623\u064e\u0628\u0652\u0646\u064e\u0627\u0621\u064f \u0639\u064e\u0634\u0652\u0631\u064d \u060c \u0648\u064e\u0641\u064e\u0631\u0651\u0650\u0642\u064f\u0648\u0627 \u0628\u064e\u064a\u0652\u0646\u064e\u0647\u064f\u0645\u0652 \u0641\u0650\u064a \u0627\u0644\u0652\u0645\u064e\u0636\u064e\u0627\u062c\u0650\u0639\u0650]\u00a0 <span style=\"color: #ff6600;\">\u00a0\u0635\u062d\u062d\u0647 \u0627\u0644\u0623\u0644\u0628\u0627\u0646\u064a \u0641\u064a \u0635\u062d\u064a\u062d \u0623\u0628\u064a \u062f\u0627\u0648\u062f<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\">[Waamrisheni watoto wenu kuswali wanapofika miaka saba,na muwapige wanapoacha Swala wakiwa na umri wa miaka kumi,na muwafarikishe katika malazi]\u00a0\u00a0\u00a0<span style=\"color: #008000;\">[Imesahihiswa na Al-Baniy katika Sunani Abiy Daud]<\/span><\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">8.<\/span>\u00a0Kuweka risala ya pamoja katika kutekeleza haki ya:<\/p>\n<p>\uf0d8\u00a0Mwenyezi Mungu Aliyetukuka.<br \/>\n\uf0d8\u00a0Mtume\u00a0\ufdfa.<br \/>\n\uf0d8\u00a0Wazazi wawili.<br \/>\n\uf0d8\u00a0Nasaba yao.<br \/>\n\uf0d8\u00a0Majirani.<br \/>\n\uf0d8\u00a0Ummah.<br \/>\n\uf0d8\u00a0Nafsi.<br \/>\nHaki zote hizi zataka ziwe katika risala ya pamoja wakubaliane kuwa hizi haki zifahamike na zichungwe.<\/p>\n<p><span style=\"color: #993300;\">VIPI TUTAWAELIMISHA WATOTO WETU KISAWA ?<\/span><\/p>\n<p>\uf0d8\u00a0Kuwafundisha tawhid nako ni kumpwekesha ALLAH (SWT) na kujitahdhirisha na shirk.<br \/>\n\uf0d8\u00a0Kuwahifadhisha kitabu cha ALLAH (SWT) kulingana na uwezo wa akili zao.Baada ya hapo ajue maana yake aweze kuizingatia na kuitumia katika maisha yake.Kwa maana hiyo anafaa kuhifadhi,kufahamu,kuzingatia na kuitumia.<br \/>\n\uf0d8\u00a0Kujua lugha ya kiarabu ambayo ni lugha ya Qur\u2019an na kujifakhiri nayo.<br \/>\n\uf0d8\u00a0Kumfanya mtume\u00a0\ufdfa\u00a0kuwa ndiye kielelezo chema katika maisha ya watoto wetu,kwa kusoma hadithi za mtume na sera yake na kuzifanyia kazi<br \/>\n\uf0d8\u00a0Kuwaheshimu maswahaba wa mtume wote akiwatanguliza makhalifa wanne Abubakar,Omar,Uthman na Ali radhi za Mungu ziwe juu yao wote.<br \/>\n\uf0d8\u00a0Kuwafundisha Fiqh ya ibada zake zote,swalaa,Swaum,Zakat na Hajj<br \/>\n\uf0d8\u00a0kuwafundisha namna ya kufikiria na kupanua uwezo wao wa kutoa masuluhisho.<br \/>\nBaada ya kuweka misingi hii imara unaweza kumpeleka shule yenye nidhamu ili kukuza misingi uliyoijenga.Mfano ni shule za mseto zenye masomo ya dini na kisekula akapate maarifa ya kilimwengu pasi na kusahau akhera yake.<\/p>\n<p>TAHADHARI!!!<br \/>\nUKIWEZA KUJIEPUSHA NA ANASA NYUMBANI KWAKO ITASAIDIA SANA KATIKA MALEZI YA WATOTO WAKO.<br \/>\nJAZAKALLAH KHEIR.<\/p>\n<p>Sheikh Abuu Hamza<\/p>\n<p>Mombasa-Kenya<\/p>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>VIPI TUTAANZA MALEZI BORA KATIKA JAMII ZETU ? Hatua zifuatazo ni muhimu sana kila mmoja wetu azizingatie ili malezi yasiwe ni ya kubahatisha bali malezi yawe ya kitaalamu na kuwe na malengo ya wazi.Kwa hivyo ni muhimu wazazi wasome malezi yenyewe yanavyotakikana Kusomwa. Kusoma vitabu vya malezi na kumsoma Mtume\u00a0\ufdfa\u00a0alivyolea watoto wake na alivyofundisha malezi. [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":9029,"comment_status":"open","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[101],"tags":[],"class_list":["post-4622","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-sehemu-ya-tarbiya"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4622","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=4622"}],"version-history":[{"count":5,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4622\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":12945,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4622\/revisions\/12945"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/9029"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=4622"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=4622"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=4622"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}