{"id":4619,"date":"2021-06-16T22:55:25","date_gmt":"2021-06-16T22:55:25","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=4619"},"modified":"2021-12-20T16:09:48","modified_gmt":"2021-12-20T16:09:48","slug":"mbinu-za-malezi-sheikh-abuu-hamza","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/mbinu-za-malezi-sheikh-abuu-hamza\/","title":{"rendered":"MBINU ZA MALEZI- Sheikh Abuu Hamza"},"content":{"rendered":"<h3><span style=\"color: #993300;\"><strong>MBINU ZA MALEZI<\/strong><\/span><\/h3>\n<p>Malezi \u00a0yana mbinu \u00a0maalumu \u00a0ambazo yataka \u00a0tuzifahamu, ili tuweze kuwalea \u00a0watoto wetu \u00a0kwa njia za kisawa. Mbinu hizi zinabadilika \u00a0kulingana \u00a0na mabadiliko ya kitaaluma yanavyobadilika kwa kasi sana.Pamoja na \u00a0athari ya tamaduni zinazotufikia kupitia mitandao mbalimbali. Kwa hivyo kuna dharura ya kuzifahamu \u00a0mbinu hizi haswa ukizingatia kuwa kuna athari \u00a0ya utandawazi \u00a0katika ulimwengushi \u00a0au ulimwengu wa kijiji kimoja.Mambo yafuatayo ni muhimu yazingatiwe:<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">1. <\/span>Kwanza mbinu ya kuwa wewe ni kiigizo \u00a0chema kwa \u00a0namna unavyomlea mtoto au jinsi jamii inavyokutazama \u00a0wewe \u00a0pamoja na mambo unayoyatenda \u00a0kuliko unayoyasema. Kwa hivyo kuwa mfano mwema ni muhimu sana katika malezi.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">2.<\/span> Pili \u00a0ni mbinu ya mawaidha mazuri \u00a0na kumuelekeza mtoto wako mara kwa mara katika njia iliyonyooka.Kutoa mwongozo wa kimaisha kwa unayemlea ni jambo muhimu sana.Hivi kwamba akue akijua mwelekeo unaoutaka wewe kama mlezi wake.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">3.<\/span> Tatu mbinu ya kumpendezesha \u00a0na kumwonesha \u00a0uzuri wa lile unalotaka \u00a0alifanye, vipi lina athari \u00a0na maisha yake na kumwonesha \u00a0vipi atafaulu akifuata \u00a0yale unayomfahamisha.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">4.<\/span> Nne mbinu ya kumtahadharisha na kumwonesha \u00a0madhara na hasara atakazopata katika maisha yake na ubaya wa tabia ile mbaya unayomkataza.Kwa mfano madhara ya kutohifadhi wakati, kukhalifu ahadi, kutokuwa na uaminifu katika maisha yake pamoja na tabia mbaya nyingi.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">5.<\/span> Tano ni mbinu ya kupigia mtoto wako mifano hai \u00a0ili aweze kutofautisha baina ya faida na hasara za tabia mbalimbali.Mfano Amati mwalimu mwanachuoni wa kike ambaye mpaka leo yupo katika \u00a0uhai na amefundisha \u00a0Qur\u2019an miaka 110.Huu ni mfano hai katika nchi ya Kenya mwanamke mshela atumia umri wake wote katika kufundisha dini.Hivi ndivyo jinsi tunavyopaswa kujitolea kwa manufaa ya jamii.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">6.<\/span> Sita ni mbinu ya kutumia \u00a0visa vilivyotokea katika kurekebisha tabia fulani. Utoaji wa visa ni mbinu muhimu sana katika kulea mtoto.Kwani waliotangulia walipatikana na mambo mengi ambayo lau watoto wetu watakuwa wakihadithiwa watapata mazingatio mengi sana.Mfano wa kile kisa cha yule mwanamume aliyeuwa watu 99 kisha akarudi kwa ALLAH(S.W.T) kumtaka msamaha.Akakutana na msomi aliyemshauri \u00a0atoke katika mji ule anaoishi aende katika mji wa watu wazuri.Kisa ni kirefu lakini faida yake ni kuwa, mwisho ALLAH(S.W.T) akamsamehe.Mazingatio tunayoyapata ni kuwa hatupaswi kukata tamaa na rehma ya ALLAH (S.W.T).<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">7.\u00a0<\/span> Mbinu ya saba ni ya kumzowezesha mtoto kukariri jambo mpaka akazowea \u00a0kama alivyofundisha Mtume \ufdfa\u00a0 Swala juu ya mimbari na kama alivyofundisha Sayyidna Uthman b.Affan (R.A) namna Mtume alivyochukua Udhu.Jambo likirudiwarudiwa linabaki kwenye fahamu ya mtoto.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">8.<\/span>\u00a0Mbinu ya nane ni ya kufaidika na matokeo fulani kisha ukatumia fursa ile kurekibisha kosa au kutilia nguvu fikra fulani kwa kutumia matokeo fulani.Mfano kumsisitiza mtoto afanye bidii ya kuhifadhi Qur\u2019an baada ya kumwona mwenzake akiswalisha msikitini na mengine mengi.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">9.<\/span> Mbinu ya tisa ni kujaribu \u00a0kukuza fikra ya mtoto na kuifungamanisha na utumiaji wa busara katika maisha ya wanadamu.Akue akijua kuwa katika maisha kuna mambo mengi yanayohitaji hekima na busara pasi na kutumia nguvu kukabiliana nayo.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">10.<\/span> Mbinu ya kumi ni kujaribu kukusanya \u00a0mazoezi uliyoyapata \u00a0kulingana \u00a0na tajriba yako katika kutaamaliana \u00a0na binadamu wengine.Mtoto wako awe karibu na wewe katika kuona ni jinsi gani unataamaliana na watu.Akiona tabia fulani inajirudiarudia hutakuwa na haja ya kumwambia afanye bali atafanya mwenyewe kwa sababu amekuwa akikuona jinsi gani unavyotaamaliana na watu.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">11.<\/span> Kumi na moja ni mbinu ya kutumia mazungumzo mazuri katika kutafuta usawa wa jambo.Na vilevile kukinaisha watu \u00a0katika kutazama mambo na vishawishi tofauti katika maisha.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">12.<\/span> Kumi na mbili ni kujaza nafasi au pengo kwa \u00a0kutumia fursa inapojitokeza \u00a0au kubuni nafasi ya kurekibisha jambo kwa njia ya hekima na busara.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">13.<\/span> Kumi na tatu ni kuangalia jinsi watu wanavyosuhubiana katika safari na kutazama \u00a0vitendo vyao katika safari hizo kwani \u00a0mara nyingi watu wanafahamika na kudhirika jinsi walivyo wakati wakiwa kwenye safari.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">14.<\/span> Mbinu ya Kumi na nne ni yakuadhibu \u00a0na hii yafaa itumike ya mwisho \u00a0baada ya kutofanya kazi mbinu zote kumi na tatu zilizotangulia.Mbinu hii yafaa itumike kwa uwangalifu mno na adhabu iwe ya kipimo na iambatane na kosa mara tu linapofanyika.Kwa mfano ni makosa kwa mzazi kumwadhibu mtoto wake leo kwa kosa alilotenda wiki iliyopita.Changamoto ni kuwa wazazi wengi hawajui mbinu hizi,wao hupindukia katika kutesa na kuadhibu tu.<\/p>\n<p>Hivyo basi ni muhimu sana kuzingatia mbinu hizo ili zirahisishe malezi haswa katika ulimwengu huu wa utandawazi.<\/p>\n<p>Makala yameandikwa na: Sheikh Abu hamza<\/p>\n<p>Kusahihishwa kilugha na: Ustadh Ali Juma<\/p>\n<p>Makala yanaendelea\u2026<\/p>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>MBINU ZA MALEZI Malezi \u00a0yana mbinu \u00a0maalumu \u00a0ambazo yataka \u00a0tuzifahamu, ili tuweze kuwalea \u00a0watoto wetu \u00a0kwa njia za kisawa. Mbinu hizi zinabadilika \u00a0kulingana \u00a0na mabadiliko ya kitaaluma yanavyobadilika kwa kasi sana.Pamoja na \u00a0athari ya tamaduni zinazotufikia kupitia mitandao mbalimbali. Kwa hivyo kuna dharura ya kuzifahamu \u00a0mbinu hizi haswa ukizingatia kuwa kuna athari \u00a0ya utandawazi \u00a0katika [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":12287,"comment_status":"open","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[101],"tags":[],"class_list":["post-4619","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-sehemu-ya-tarbiya"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4619","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=4619"}],"version-history":[{"count":6,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4619\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":12289,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4619\/revisions\/12289"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/12287"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=4619"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=4619"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=4619"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}