{"id":4535,"date":"2021-06-16T20:14:38","date_gmt":"2021-06-16T20:14:38","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=4535"},"modified":"2022-09-26T18:36:58","modified_gmt":"2022-09-26T18:36:58","slug":"hukmu-ya-kukariri-sura-maalum-baada-ya-suratul-fatiha-katika-rakaa-ya-kwanza-na-ya-pili","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/hukmu-ya-kukariri-sura-maalum-baada-ya-suratul-fatiha-katika-rakaa-ya-kwanza-na-ya-pili\/","title":{"rendered":"HUKMU YA KUKARIRI SURA MAALUM BAADA YA SURATUL FATIHA KATIKA RAKAA YA KWANZA NA YA PILI"},"content":{"rendered":"<h3><strong><span style=\"color: #993300;\">HUKMU YA KUKARIRI SURA MAALUM BAADA YA SURATUL FATIHA KATIKA RAKAA YA KWANZA NA YA PILI<\/span><\/strong><\/h3>\n<p><span style=\"color: #008000;\">Suali\u00a0<\/span>:\u00a0Jee yafaa kusoma sura maalum baada ya Suratul fatihah kisha kusoma sura ile ile baada ya fatihah katika rakaa ya pili. Na jee yafaa kudumu kusoma sura maalum baada ya faatihah katika kila swala na katika kila rakaa, na jee swala inaswihi pamoja na kudumu na jambo hilo??<br \/>\n<span style=\"color: #0000ff;\">Jawabu\u00a0:<\/span><\/p>\n<p>Kwanza : Yafaa mwenye kuswali kusoma sura maalum baada ya Suratul Faatihah katika Rakaa ya kwanza, kisha akasoma sura ile ile katika Rakaa ya pili.<br \/>\nNa linaloonesha kufaa kwa jambo hilo ni Hadithi iliyopokelewa na Abu Daud (816) kutoka kwa Mtu mmoja kutoka katika kabila la Juhainah yakwamba<\/p>\n<p dir=\"rtl\" style=\"text-align: right;\"><span style=\"color: #008000;\">\u0633\u064e\u0645\u0650\u0639\u064e \u0627\u0644\u0646\u0651\u064e\u0628\u0650\u064a\u0651\u064e \u0635\u064e\u0644\u0651\u064e\u0649 \u0627\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u064f \u0639\u064e\u0644\u064e\u064a\u0652\u0647\u0650 \u0648\u064e\u0633\u064e\u0644\u0651\u064e\u0645\u064e : \u064a\u064e\u0642\u0652\u0631\u064e\u0623\u064f \u0641\u0650\u064a \u0627\u0644\u0635\u0651\u064f\u0628\u0652\u062d\u0650 ( \u0625\u0650\u0630\u064e\u0627 \u0632\u064f\u0644\u0652\u0632\u0650\u0644\u064e\u062a\u0652 \u0627\u0644\u0652\u0623\u064e\u0631\u0652\u0636\u064f ) \u0641\u0650\u064a \u0627\u0644\u0631\u0651\u064e\u0643\u0652\u0639\u064e\u062a\u064e\u064a\u0652\u0646\u0650 \u0643\u0650\u0644\u0652\u062a\u064e\u064a\u0652\u0647\u0650\u0645\u064e\u0627 \u060c \u0641\u064e\u0644\u064e\u0627 \u0623\u064e\u062f\u0652\u0631\u0650\u064a \u0623\u064e\u0646\u064e\u0633\u0650\u064a\u064e \u0631\u064e\u0633\u064f\u0648\u0644\u064f \u0627\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u0650 \u0635\u064e\u0644\u0651\u064e\u0649 \u0627\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u064f \u0639\u064e\u0644\u064e\u064a\u0652\u0647\u0650 \u0648\u064e\u0633\u064e\u0644\u0651\u064e\u0645\u064e \u0623\u064e\u0645\u0652 \u0642\u064e\u0631\u064e\u0623\u064e \u0630\u064e\u0644\u0650\u0643\u064e \u0639\u064e\u0645\u0652\u062f\u064b\u0627 &#8220;<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\">[Alimsikia Mtume MUHAMMAD \ufdfa akisoma katika Swala ya subhi sura ya (Idha zulzilatil ardhu) katika Rakaa zote mbili sasa sijui kama Mtume \ufdfa alisahau ama alisoma hivyo kwa makusudi]<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #008000;\">Hadithi hii amesema\u00a0Sheikh Albany\u00a0Mungu amrehemu yakwamba ni nzuri katika kitabu cha\u00a0[Swahihu Sunani Abii Daud].<\/span><\/p>\n<p>Amesema\u00a0Sheikh Albany\u00a0Mwenyezi Mungu amrehemu katika kitabu chake &#8220;Swala&#8221; [ukurasa wa 90]<br \/>\n&#8220;Na udhahiri wa hadithi hii ni kwamba mtume MUHAMMAD <span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span> alifanya vile kwa makusudi ili iwe sheria&#8221; .<\/p>\n<p>Na amepokea\u00a0<span style=\"color: #ff6600;\">Imamu Bukhary<\/span>\u00a0(7375)\u00a0na\u00a0<span style=\"color: #ff6600;\">Imamu Muslim\u00a0(813)<\/span>\u00a0Imepokelewa kutoka kwa Aisha radhi za ALLAH ziwe juu yake yakwamba Mtume MUHAMMAD\u00a0<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>:<\/p>\n<p dir=\"rtl\" style=\"text-align: right;\"><span style=\"color: #008000;\">\u0623\u064e\u0646\u0651\u064e \u0631\u064e\u0633\u064f\u0648\u0644\u064e \u0627\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u0650 \u0635\u064e\u0644\u0651\u064e\u0649 \u0627\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u064f \u0639\u064e\u0644\u064e\u064a\u0652\u0647\u0650 \u0648\u064e\u0633\u064e\u0644\u0651\u064e\u0645\u064e \u0628\u064e\u0639\u064e\u062b\u064e \u0631\u064e\u062c\u064f\u0644\u064b\u0627 \u0639\u064e\u0644\u064e\u0649 \u0633\u064e\u0631\u0650\u064a\u0651\u064e\u0629\u064d \u0648\u064e\u0643\u064e\u0627\u0646\u064e \u064a\u064e\u0642\u0652\u0631\u064e\u0623\u064f \u0644\u0650\u0623\u064e\u0635\u0652\u062d\u064e\u0627\u0628\u0650\u0647\u0650 \u0641\u0650\u064a \u0635\u064e\u0644\u064e\u0627\u062a\u0650\u0647\u0650\u0645\u0652 \u0641\u064e\u064a\u064e\u062e\u0652\u062a\u0650\u0645\u064f \u0628\u0650\u0642\u064f\u0644\u0652 \u0647\u064f\u0648\u064e \u0627\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u064f \u0623\u064e\u062d\u064e\u062f\u064c &#8230;. \u0625\u0644\u062e \u0627\u0644\u062d\u062f\u064a\u062b<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\">[Alimtuma mtu kama kiongozi wa kundi la jeshi na alikua akiwasomea watu wake katika Swala zao na alikua akimalizia na (Qul huwa llahu ahad)&#8230;. Mpaka mwisho wa hadith.<\/span><\/p>\n<p>Amesema\u00a0Ibnul Araby\u00a0Mwenyezi Mungu amrehemu akisherehesha hadithi ya Imamu Bukhary:-<br \/>\n&#8220;Na likawa hili ni dalili yakwamba yafaa kukariri sura katika kila rakaa&#8221; imeisha kutoka katika kitabu cha &#8221;\u00a0\u00a0[Ahkaamul Qur&#8217;an] (4\/468)<\/p>\n<p>Pili :Kudumu na kusoma sura maalum baada ya fatihah katika kila Rakaa, na katika kila Swala inafaa na ndio madhehabi ya Wanazuoni wengi.<br \/>\nImekuja katika kitabu cha\u00a0[Mausuuatul fiqhiyyah]\u00a0 (25\/290):<br \/>\n&#8220;Wameenda wanazuoni wengi katika madhehebu ya Hanafi na Shafii na Hanbal yakwamba &#8220;Hakuna tatizo kwa mwenye kuswali kukariri sura katika Qur&#8217;aan aliyoisoma katika rakka ya kwanza&#8221;\u00a0.<\/p>\n<p>Isipokua hata kama jambo hili linafaa,na Swala inaswihi kwalo, na halibatwilishi Swala ila Jambo hili ni kinyume na Sunna, na muongozo uliopangika wa Bwana Mtume MUHAMMAD\u00a0\ufdfa\u00a0na hivyo basi inapendeza na ni bora kwake asome Sura tofauti tofauti kwa kumuiga Bwana Mtume MUHAMMAD\u00a0\ufdfa.<\/p>\n<p>Anasema\u00a0Sheikh Ibnu Uthaymeen\u00a0ALLAH amrehemu:<br \/>\n&#8220;Na mkabala wa jambo hili ni kwamba jambo linaweza kua linafaa lakini haliwi sheria:<br \/>\nKisa cha mtu ambae mtume alimtuma kama kiongozi wa jeshi , basi alikua akiwaswalisha watu wake na katika kusoma kwake alikua akmalizia na (Qul huwa llahu ahad) , waliporudi wakamuelezea Mtume \ufdfa kuhusu jambo hilo Mtume\u00a0\ufdfa akasema &#8220;Muulizeni kwanini alikua akifanya hivyo&#8221;? Akasema : Hakika sura hii ni sifa ya Al Rahmaan na mimi napenda kuisoma sura hii Mtume\u00a0\ufdfa akasema &#8221; Mwambieni yakwamba ALLAH anampenda&#8221; kwahivyo mtume akalikiri tendo lake hili , nalo ni yeye kumalizia kisomo chake katika swala na (Qul huwa llahu ahad) Lakini Mtume \ufdfa hakulifanya jambo hili kwamba ni sheria ; kwani hata yeye Mtume \ufdfa alikua hamalizi kisomo chake katika swala na Qul huwa llahu ahad na wala hakuamrisha umma wake kufanya hivyo.&#8221;<\/p>\n<p>Inabainika kutokana na jambo hili yakwamba kuna matendo ambayo inafaa kuyafanya lakini sio sheria ,kwa maana yakwamba mwanadamu akikifanya kitendo hicho hakemewi , na pia hawezi kuambrishwa kukifanya kitendo hicho &#8221;<br \/>\nImeisha kutoka katika kitabu cha\u00a0[Majmu&#8217;u Fataawa Ibni Uthaymeen] (17\/252)<br \/>\nNa ALLAH ndio mjuzi zaidi.<\/p>\n<p>Kwa kifupi : inafaa kwa mwenye kiswalia kusoma sura maalum baada ya Faatihah katika Rakaa ya kwanza na kusoma sura ile ile katika Rakaa ya pili na hivyo hivyo kudumu na kusoma sura maalum baada ya Faatihah katika kila Rakaa , na katika swala zote lakini linalopendeza na lililo bora kwake : ni kusoma sura tofauti tofauti , kwa kumuiga bwana Mtume MUHAMMAD <span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>.<\/p>\n<blockquote><p><span dir=\"RTL\">Chanzo ni Fatwa ya Sheikh Swaleh Al Munajjid*\u00a0<\/span><\/p>\n<p>Na kufanya Tarjam na Ustadh Fadhil Muhammad<\/p><\/blockquote>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>HUKMU YA KUKARIRI SURA MAALUM BAADA YA SURATUL FATIHA KATIKA RAKAA YA KWANZA NA YA PILI Suali\u00a0:\u00a0Jee yafaa kusoma sura maalum baada ya Suratul fatihah kisha kusoma sura ile ile baada ya fatihah katika rakaa ya pili. Na jee yafaa kudumu kusoma sura maalum baada ya faatihah katika kila swala na katika kila rakaa, na [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":15967,"comment_status":"open","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[90],"tags":[],"class_list":["post-4535","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-mlango-wa-swala-fatawa-sw"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4535","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=4535"}],"version-history":[{"count":5,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4535\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":16100,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4535\/revisions\/16100"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/15967"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=4535"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=4535"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=4535"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}