{"id":4523,"date":"2021-06-16T19:41:58","date_gmt":"2021-06-16T19:41:58","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=4523"},"modified":"2021-10-06T12:37:02","modified_gmt":"2021-10-06T12:37:02","slug":"hukmu-ya-mtu-alie-kula-na-kunywa-akidhani-kuwa-bado-ni-usiku","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/hukmu-ya-mtu-alie-kula-na-kunywa-akidhani-kuwa-bado-ni-usiku\/","title":{"rendered":"HUKMU YA MTU ALIE KULA NA KUNYWA AKIDHANI KUWA BADO NI USIKU"},"content":{"rendered":"<h2>HUKMU YA MTU ALIE KULA NA KUNYWA AKIDHANI KUWA BADO NI USIKU<\/h2>\n<p>Suali :<br \/>\nAl fajiri ya siki ya kwanza ya mwezi wa Ramadhan aliniamsha mke wangu akasema jee unataka\u00a0kunywa maji ?<\/p>\n<p>Na nilipochukua maji kutoka kwake nilimuuliza jee kumeadhiniwa ?<\/p>\n<p>Akasema :hapana na baada ya kunywa maji kwa dakika 15 &#8211; 20 swala ikakimiwa, kwahivyo\u00a0\u00a0nikinywa maji baada ya adhana kwa dakika 5 &#8211; 10 jee nina makosa ?<\/p>\n<p>Jawabu :<br \/>\nAlhamdulillah kwa hakika wamekhtalifiana wanazuoni kuhusu hukmu ya aliyekula au kunywa akidhania kwamba bado ni usiku na bado Al fajiri haijaingia, na vile vile aliyekula au kunywa akidhania kuzama kwa jua kisha ikambainikia kosa lake.<\/p>\n<p>Wanazuoni wengi wanaona yakwamba Saumu yake inaharibika kwa hilo, na inamlazimu yeye kufunga siku moja badala yake.<\/p>\n<p>Na wanaona wanazuoni wengine yakwamba funga yake ni sahihi na yakwamba yeye atakamilisha funga yake wala hatolipa siku ile aliyokula.<\/p>\n<p>Nayo ni kauli ya Mujahid\u00a0na\u00a0Hassan na Twaabiiy,\u00a0na mapokezi kutoka kwa\u00a0Imam Ahmad ,\u00a0na\u00a0amechagua rai hii\u00a0Al Muzany\u00a0katika wanazuoni wa madhehebu ya\u00a0Imam Shafii\u00a0, na Sheykhul\u00a0Islam Ibnu Taymiyah na ameipitisha rai hii\u00a0Sheikh Muhammad Swaleh Al Othaimeen.\u00a0&#8211; Allah\u00a0awarehemu wote.<\/p>\n<p>Amesema\u00a0Sheykhul Islam Ibnu taymiyah\u00a0:<br \/>\n&#8220;Na wale wanaosema hajafungua katika zote (yaani : akikosea au kusahau mwanzo wa mchana au\u00a0mwisho wake ) wamesema hoja yetu ndio yenye nguvu zaidi, na dalili ya\u00a0 Kitabu na Sunna\u00a0juu ya kauli yetu iko wazi zaidi:<\/p>\n<p>kwani Mwenyzi Mungu alietukuka anasema:<\/p>\n<p dir=\"rtl\">{\u0631\u0628\u0646\u0627 \u0644\u0627 \u062a\u0624\u0627\u062e\u0630\u0646\u0627 \u0625\u0646 \u0646\u0633\u064a\u0646\u0627 \u0623\u0648 \u0623\u062e\u0637\u0623\u0646\u0627}<\/p>\n<p><em>[Mola wetu Mlezi! Usituchukulie tukisahau au tukikosea.]\u00a0<\/em>kakusanya baina ya kusahau na kukosea, na kwa sababu atakayefanya yasiyofaa katika Hijja na katika Swala kwa makosa ni kama aliefanya kwa kusahau , na imethibiti katika Sahihi (AlBukhari) yakwamba Maswahaba walifuturu katika zama za Mtume \ufdfa kisha jua likachomoza, na hawakutaja katika hadithi yakwamba wao waliamrishwa kulipa, lakini Hishaam bin Urwah amesema: ni lazima kulipa, na baba yake ni mjuzi kumshinda lakini alikua akisema: Hawalazimiki kulipa na imethibiti katika Sahihi mbili (Bukhari na Muslim)<\/p>\n<p>yakwamba kikundi katika maswahaba walikua wanakula mpaka imdhihirikie mmoja wao uzi mweupe\u00a0kutokana na uzi nyeusi, na akasema Mtume rehma na amani ziwe juu yake<br \/>\nkumwambia mmoja wao hakika<\/p>\n<p dir=\"rtl\">[\u0625\u0646 \u0648\u0633\u0627\u062f\u0643 \u0644\u0639\u0631\u064a\u0636 \u060c \u0625\u0646\u0645\u0627 \u0630\u0644\u0643 \u0628\u064a\u0627\u0636 \u0627\u0644\u0646\u0647\u0627\u0631 \u0648\u0633\u0648\u0627\u062f \u0627\u0644\u0644\u064a\u0644]<\/p>\n<p>[Hakika Mto wako ni mpana, makusudio ya hilo ni uweupe wa mchana na\u00a0na uweusi wa usiku]<\/p>\n<p>Wala haijanukuliwa kwamba Mtume \ufdfa aliwaamrisha kulipa, na hawa walikua wajinga wa hukumu hivyo basi wakakosea, na imethibiti kutoka kwa Umar bin Al Khatwab yakwamba yeye alifungua kisha ikabainika mchana akasema : &#8220;hatulipi kwani sisi hatujakusudia dhambi&#8221;; na imepokelewa kutoka kwake yakwamba alisema: &#8220;tunalipa&#8221; , lakini isnadi ya kwanza ndio iliyothibiti zaidi , na imeswihi kutoka kwake yakwamba yeye alisema: &#8220;hili ni jambo dogo&#8221;; basi wakatafsiri hilo wenye kutafsiri yakwamba yeye alikusudia kuwa hilo la kulipa saumu ni jambo dogo, lakini lafdhi hii haiashirii hilo .<\/p>\n<p>Kwa ujumla : kauli hii (ya kutolipa) ndio yenye athari kubwa na nadharia yenye nguvu zaidi, na\u00a0zaidi na Dalili ya Kitabu , Sunna , na kiasi.&#8221;<\/p>\n<p>Majmuul Fataawa ( 20 \/ 572 , 573 ) .<\/p>\n<p>Na angalia pia\u00a0Al Sharhul Mumti\u00a0\u00a0( 6 \/ 411 )<br \/>\nNa hivyo basi inadhihirika nguvu za dalili za kauli yakwamba Funga yake ni sahihi na wala<\/p>\n<p>hatolipa .<\/p>\n<p>Pamoja na hivyo lau Muislamu atataka kujitoa kwenye shaka na akalipa siku moja mahala pake basi\u00a0atakua amefanya vizuri .<\/p>\n<p>Na ALLAH ni mjuzi zaidi .<\/p>\n<blockquote><p>Chanzo:\u00a0Tovuti ya Fatwa Suali wa Jawabu<\/p><\/blockquote>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>HUKMU YA MTU ALIE KULA NA KUNYWA AKIDHANI KUWA BADO NI USIKU Suali : Al fajiri ya siki ya kwanza ya mwezi wa Ramadhan aliniamsha mke wangu akasema jee unataka\u00a0kunywa maji ? Na nilipochukua maji kutoka kwake nilimuuliza jee kumeadhiniwa ? Akasema :hapana na baada ya kunywa maji kwa dakika 15 &#8211; 20 swala ikakimiwa, [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":9169,"comment_status":"open","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[92],"tags":[],"class_list":["post-4523","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-mlango-wa-saumu-fatawa-sw-2"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4523","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=4523"}],"version-history":[{"count":3,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4523\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":9176,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4523\/revisions\/9176"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/9169"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=4523"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=4523"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=4523"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}