{"id":4369,"date":"2021-06-16T10:16:48","date_gmt":"2021-06-16T10:16:48","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=4369"},"modified":"2022-03-03T12:21:33","modified_gmt":"2022-03-03T12:21:33","slug":"je-yesu-na-issa-a-s-ni-mtu-mmoja","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/je-yesu-na-issa-a-s-ni-mtu-mmoja\/","title":{"rendered":"JE YESU NA ISSA (A.S) NI MTU MMOJA??"},"content":{"rendered":"<h2><span style=\"color: #993300;\">JE YESU NA ISSA (A.S) NI MTU MMOJA?<\/span><\/h2>\n<p>Mwanadamu anapoongozwa na uoga, mara nyingi hutoka katika mipangilio sahihi<\/p>\n<p>na kuchukua muda wake mwingi akijaribu kubuni njia na mikakati ya kumkinga<\/p>\n<p>asipoteze alichonacho na waliomzunguka. Kwa hivyo hujifanya kama ni tofauti na<\/p>\n<p>wale wanaomsikiza kiakili, katika kuelewa na kwa njia hii hubuni uwongo wa<\/p>\n<p>kumdumisha katika biashara ya pekee anayoijua yeye.<\/p>\n<p>Waislamu hatukuamriwa kudharau, kuchukia au kubagua mtu yeyote kwa misingi<\/p>\n<p>ya rangi, awe mke au mume kuwa tukuza Manabii hadi kiwango cha kusema<\/p>\n<p>ili kujifurahisha tu kwa muda kuwa Yesu, Issa na Jesus ni watu tofauti, bali Quran<\/p>\n<p>imetuamuru hivi:<\/p>\n<p>\u201cSema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na tuliyoteremshiwa sisi, na<\/p>\n<p>aliyoteremshiwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaqub na wajukuu zao na<\/p>\n<p>aliyopewa Musa na Issa na Manabii wengine kutoka kwa Mola wao. Hatubagui<\/p>\n<p>baina yao hata mmoja na sisi ni wenyekevu kwake.\u201d\u00a0(TMQ 3:84)<\/p>\n<p>Sisi waislamu hatuna tabia ya baadhi ya wakristo kubagua Manabii, bali<\/p>\n<p>tunawaamini, kuwataja kwa heshima yao pamoja na kuwahami kutokana na wale<\/p>\n<p>ambao wana itikadi mbaya. Lakini kila wakati waislamu wanapokuja pamoja ili<\/p>\n<p>waishi kwa undugu wa kibinadamu na wakristo, wako wanaotafuna changarawe<\/p>\n<p>za fitna eti Yesu, Issa na Jesus ni watu tofauti!<\/p>\n<p>Katika kurasa hizi hatulengi kuunga wala kupinga wale wakristo wanaosema Yesu<\/p>\n<p>mwana wa maryamu ndiye mungu, mwana wa mungu au zote (mungu tena<\/p>\n<p>mwana wa mungu) bali ni kukupeni mwelekeo ulio sahihi kwa atakaye maana,<\/p>\n<p>hakuna kulazimisha mtu katika dini\u00a0(Quran 2:256)<\/p>\n<p>Ulimwengu umeweka vitu vinavyoitwa International Standards na huwezi kuleta<\/p>\n<p>chochote kinyume chake, na kuwa umekileta na kinatumika sio dalili kuwa uko<\/p>\n<p>sawa, bali wale waasisi wa ubaya huo wanafurahi kukuona ukididimia kwenye<\/p>\n<p>lindi la upotovu.<\/p>\n<p>Ni habari za kuaminika kuwa kuna vitu vinne kisheria ya uandishi havifanyiwi<\/p>\n<p>tafsiri na utaona katika ramani ya biblia yako jina la mto Yordani halijafanyiwa<\/p>\n<p>tafsiri, mto Nile, Tigris, Euphrates na mingineyo imebakia na jina asilia. Jina la<\/p>\n<p>mto au jina la nchi, jina la mtu au mlima haliwezi kufanyiwa tafsiri lakini kwa<\/p>\n<p>hawa ndugu wakristo katika Biblia yao majina ya watu yamefanyiwa tafsiri eti<\/p>\n<p>Yesu ni Kiswahili na Jesus ni Kizungu lakini lugha yake ya asili usiijue?<\/p>\n<p>Wengi hawajui kuwa jina \u201cIssa\u201d ni jina la ki israeli na kama waeza kufuatilia hebu<\/p>\n<p>tafuta maana na namna jina hili linavyosomwa \u201cESSAU\u201d na sina shaka utafahamu<\/p>\n<p>Kwa sababu ya kudumisha utengano na maelewano, sote twajua kuwa \u201cIssa\u201d<\/p>\n<p>ndiye huyo \u201cYesu\u201d kama vile mkate ndio \u201cBread\u201d<\/p>\n<p>Quran na Biblia zimetuonyesha kuwa Mama Maryamu a.s. alizaa mtoto wa<\/p>\n<p>kiume aliyetahiriwa siku ya nne kama ilivyo desturi ambaye alitukuzwa mno na<\/p>\n<p>Mola s.w.t.<\/p>\n<p>1. Quran 3:45\u00a0\u2013 Malaika waliotumwa kwa Mama Maryam.<\/p>\n<p>2. Luka 1:26\u00a0\u2013 Mwezi wa sita Malaika Gabriel alitumwa kwa Maryam.<\/p>\n<p>3. Quran 3:47\u00a0\u2013 Maryam ni Bikra hajui Mume.<\/p>\n<p>4. Luka 1:34\u00a0\u2013 Maryam ni bikra hajui mume.<\/p>\n<p>Quran inamtambua Yesu kuwa ni mwana wa Maryam sawa na andiko la Biblia,<\/p>\n<p>sasa vipi mtu aseme Yesu na Issa ni tofauti?<\/p>\n<p>1. Quran 3:45\u00a0\u2013 Jina lake ni Issa mwana wa Maryam.<\/p>\n<p>2. Marko 6:3\u00a0\u2013 Yesu, mwana wa Maryam.<\/p>\n<p>Kuna katika wakristo wanaodhani kuwa kwa mujibu wa Quran mwana wa<\/p>\n<p>Maryam hakufanya miujiza na wakawadanganya wakristo hivyo lakini Quran<\/p>\n<p>yaonyesha baadhi ya miujiza yake japokuwa wanadamu hawataki kuukubali<\/p>\n<p>1. Quran 3:49\u00a0\u2013 Isa mwana wa Maryam aliwaponya baadhi ya vipofu, wenye<\/p>\n<p>ukoma, na kufufua baadhi ya waliokufa kwa idhni ya Mwenyezi Mungu.<\/p>\n<p>2. Yohana 11:38 \u2013 44\u00a0\u2013 yesu amuomba Mwenyezi Mungu amfufue lazaro ili<\/p>\n<p>wale wa Izraeli wajue kuwa Yesu alitumwa na Mungu. Kando na kumfufua<\/p>\n<p>Lazaro, aliwaponya viwete, vipofu, mabubu n.k.<\/p>\n<p>Ili kutukinga na shirki, Quran ikatuonyesha kuwa mfano wake Yesu ni kama Adam<\/p>\n<p>a.s. wote waliumbwa kwa udongo na Mola s.w.t na hawastahiki kuabudiwa kwa<\/p>\n<p>vyovyote na yeyote.<\/p>\n<p>1. Quran 3:59\u00a0\u2013 Issa ana asili kutokana na Adam.<\/p>\n<p>2. Mathayo 26:64\u00a0\u2013 Yesu ni mwana wa Adam.<\/p>\n<p>3. Mathayo 19:27\u00a0\u2013 Yesu ni mwana wa Adam.<\/p>\n<p>Kihakika ni masikitiko kwa baadhi ya wakristo kudai leo eti wa Izraeli hawamjui<\/p>\n<p>Yesu ilhali Maryam aliyemzaa ametokana na wana wa Izraeli. Sasa wewe mkenya<\/p>\n<p>utamjua Yesu kulikoni mama yake?<\/p>\n<p>1. Quran 3:49\u00a0\u2013 Issa ni mtume kwa wana wa Izraeli tu.<\/p>\n<p>2. Quran 61:6\u00a0\u2013 Issa ni mtume kwa wa izraeli tu.<\/p>\n<p>3. Mathayo 10:5\u00a0\u2013 Yesu atuma wanafunzi wake kwa kabila za wa Izraeli.<\/p>\n<p>4. Mathayo 10:23\u00a0\u2013 Wao wanafunzi hawataimaliza miji ya Izraeli<\/p>\n<p>5. Mathayo 15:21\u00a0\u2013 26 \u2013 Yesu ametumwa kwa wa Izraeli pekee.<\/p>\n<p>6. Matendo 2:22\u00a0\u2013 Yesu amedhihirishwa kwenu (Waizraeli) na Mungu.<\/p>\n<p>7. Matendo 5:31\u00a0\u2013 Yesu ameleta toba kwa waizraeli tu.<\/p>\n<p>8. Matendo 11:19\u00a0\u2013 wanafunzi walifundisha habari za Yesu kwa waizraeli tu.<\/p>\n<p>9. Yohana 17:9\u00a0\u2013 Yesu anawaombea hao, haombei ulimwengu.<\/p>\n<p>Kama \u201cIssa\u201d, \u201cYesu\u201d naye hawezi kuokoa na hajui siku ya Qiyama na hawezi<\/p>\n<p>kufanya lolote ila aamriwe na Mungu.<\/p>\n<p>1. Quran 31:34\u00a0\u2013 habari za kiama ni zake Mola tu.<\/p>\n<p>2. Taurati 32:39\u00a0\u2013 Mwenyezi Mungu tu ndiye anayeokoa.<\/p>\n<p>3. Yohana 5:30\u00a0\u2013 Yesu hawezi kufanya lolote ila aamriwe.<\/p>\n<p>4. Mathayo 20:20\u00a0\u2013 Yesu asema uzima wa milele watapewa waliowekewa<\/p>\n<p>tayari na Mola.<\/p>\n<p>5. Yohana 14:28\u00a0\u2013 Mungu ni mkuu kuliko Yesu mwana wa Maryam.<\/p>\n<p>Quran imesimama msimamo mmoja na ndio mwafaka wa jamhuri ya Maulamaa<\/p>\n<p>kuwa mwana wa Maryam hakufa msalabani.<\/p>\n<p>1. Quran 4:157\u00a0\u2013 hakufa msalabani, ila wao wanafuata dhana.<\/p>\n<p>Ikiwa Yesu alikufa msalabani na ndiye Mungu wa baadhi ya wakristo basi<\/p>\n<p>yasikitisha kwa kuwa yaonyesha udhaifu wa Mungu huyu hata auwawe na viumbe<\/p>\n<p>vyake. Kwa hakika maandiko ya Biblia yameachana sana kuhusu kifo cha Yesu<\/p>\n<p>msalabani na ni vigumu kwetu kuamini na mifano ni mingi tu: &#8211;<\/p>\n<p>1. Mathayo 27:27\u00a0\u2013 Yesu kavishwa vazi jekundu.<\/p>\n<p>2. Marko 15:16\u00a0\u2013 Yesu kavishwa vazi la rangi ya zambarau.<\/p>\n<p>3. Marko 15:25\u00a0\u2013 saa tatu asubuhi Yesu amesulubiwa.<\/p>\n<p>4. Yohana 19:14\u00a0\u2013 Saa sita Yesu yuko mahakamani.<\/p>\n<p>5. Mathayo 27:3\u00a0\u2013 5: Je Yuda alijinyonga?<\/p>\n<p>6. Matendo 1:18\u00a0\u2013 20: Au Yuda alianguka akapasuka tumbo?<\/p>\n<p>Ikiwa wafuasi wa Yesu ni wakristo (Christians) Je Yesu mwenyewe alikuwa na dini<\/p>\n<p>gani na je jina la mtu laweza kuwa dini ya watu?<\/p>\n<p>1. Quran 61:14\u00a0\u2013 Mtume Issa alikuwa na wanafunzi wake.<\/p>\n<p>2. Mathayo 10:2\u00a0\u2013 Majina ya wanafunzi wa Yesu.<\/p>\n<p>Kama ni kweli kuwa Yesu aliyezaliwa na Maryam ni Mungu na kuwa anao ndugu<\/p>\n<p>zake kama munavyotuonyesha basi mna bahati kuwa mungu mwenye ndugu na<\/p>\n<p>ukoo. Sisi waislamu hatuna.<\/p>\n<p>Mathayo 1:1<\/p>\n<p>Uislamu umetuonyesha kuwa baada ya kumzaa \u201cIssa\u201d, Maryam hakuolewa,<\/p>\n<p>hakuingiliwa na mtu yeyote hadi alipokufa, yaani ndiye mwanamke pekee aliyezaa<\/p>\n<p>pasina kuingiliwa na akafa bila kuingiliwa.<\/p>\n<p>Yesu alifundisha njia ya Mungu akisema \u201cutuongoze katika njia iliyonyooka.\u201d<\/p>\n<p>1. Mathayo 6:9<\/p>\n<p>2. Luka 20:21<\/p>\n<p>Kasema kuwa kuna utatu ni kumtukana Mola, ni kumtukana Nabii Yesu, Yesu ni<\/p>\n<p>mtume tu.<\/p>\n<p>1. Yohana 17:3<\/p>\n<p>2. Yohana 5:30<\/p>\n<p>3. Yohana 7:16 \u2013 18<\/p>\n<p>4. Marko 12:28 \u2013 31<\/p>\n<p>5. Mathayo 4:10 \u2013\u00a0\u201cHuo utatu watoka wapi hali Yesu mwenyewe<\/p>\n<p>alimuabudu Mola, vipi wewe unamuabudu Yesu na udai kuwa Nabii Isaya<\/p>\n<p>alihakikisha, hali Isaya alisema \u201ctumepewa mtoto mwanamume\u201d vipi<\/p>\n<p>Mungu awe mtoto tena wa \u201ckiume\u201d kumbuka kuwa Mola hana mfano<\/p>\n<p>wowote.<\/p>\n<p>Yesu mwenyewe alisema waache wafu wazike wafu wao, tena angoje wafe ili<\/p>\n<p>awahubirie, kuongea na wafu huu si ushetani!utafute jina Issa kwa Biblia na hao<\/p>\n<p>waandishi wa biblia wamesema katika dibaji ya union version 1952 kuwa:-<\/p>\n<p>\u2026Hio kazi yenyewe haikuwa rahisi. Matumizi mbali mbali yametokea katika<\/p>\n<p>Janibu mbali mbali za nchi hii. Kwa mfano ilikuwa hapana budi kufikiri kwamba<\/p>\n<p>hilo jina la Mungu katika agano la kale litaandikwa \u201cJehova Mwenyezi Mungu<\/p>\n<p>au Bwana Mungu\u2026pia maendelezo ya majina yote ya watu nay a mahali ilikuwa<\/p>\n<p>lazima yafikiriwe tena na mengine kutengenezwa. Jambo hili lilikuwa kazi<\/p>\n<p>kubwa sana kwa sababu yako majina zaidi 3500. Tena jina la kitabu chenyewe<\/p>\n<p>lilifikiriwa, kama kiitwe \u201cMaagano mapya\u201d au agano jipya.<\/p>\n<p>Ndugu msomaji, bado wataka kuona neno \u201cIssa\u201d katika Biblia? Hizi ndizo taratibu<\/p>\n<p>ya Iman kama ilivyoeleza Quran:<\/p>\n<p>\u201cHiki ni kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake, ni muongozo kwa wacha<\/p>\n<p>Mungu ambao huyaamini mambo ya ghaib na hudumisha sala na hutoa katika<\/p>\n<p>vile tulivyowapa.\u201d\u00a0(TMQ 2:2 \u2013 3)<\/p>\n<p>Naye Yesu akasema:<\/p>\n<p>\u201csi kila mtu aniambiaye Bwana, bwana, atakayeingia katika ufalme wa<\/p>\n<p>mbinguni, bali ni Yule afanyaye mapenzi ya baba yangu aliye mbinguni.\u201d<\/p>\n<p>(Mathayo 7:21)<\/p>\n<p>Amua, utamuita \u201cYesu simba\u201d au utafanya mapenzi ya Mungu?<\/p>\n<p>Imetayarishwa na<\/p>\n<p>Adam Ambetsa<\/p>\n<p>Tel No: 0723 \u2013 174 154<\/p>\n<p>Mombasa.<\/p>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>JE YESU NA ISSA (A.S) NI MTU MMOJA? Mwanadamu anapoongozwa na uoga, mara nyingi hutoka katika mipangilio sahihi na kuchukua muda wake mwingi akijaribu kubuni njia na mikakati ya kumkinga asipoteze alichonacho na waliomzunguka. Kwa hivyo hujifanya kama ni tofauti na wale wanaomsikiza kiakili, katika kuelewa na kwa njia hii hubuni uwongo wa kumdumisha katika [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":9239,"comment_status":"open","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[85],"tags":[],"class_list":["post-4369","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-itikadi-za-wakiristo"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4369","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=4369"}],"version-history":[{"count":4,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4369\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":13095,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4369\/revisions\/13095"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/9239"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=4369"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=4369"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=4369"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}