{"id":4285,"date":"2021-06-16T08:21:36","date_gmt":"2021-06-16T08:21:36","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=4285"},"modified":"2021-10-06T12:36:41","modified_gmt":"2021-10-06T12:36:41","slug":"itikadi-ya-mashia-kuhusu-kuzuru-najaf-na-karbalaa-2","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/itikadi-ya-mashia-kuhusu-kuzuru-najaf-na-karbalaa-2\/","title":{"rendered":"ITIKADI YA MASHIA KUHUSU KUZURU NAJAF NA KARBALAA"},"content":{"rendered":"<h3><span style=\"color: #993300;\">NI IPI ITIKADI YA MASHIA KUHUSU NAJAF NA KARBALAA, NA JE, KUNA FADHLA GANI KATIKA KUZURU SEHEMU HIZO ?<\/span><\/h3>\n<p>Mashia wanaitakidi sehemu yalipo makaburi ya watu waliodai kuwa ni Maimamu wao, au ambao ni Maimamu kweli, kwa sehemu hizo ni sehemu takatifu, hivyo Al-Kuufa ni haram (sehemu takatifu), pia Karbalaa ni haram, na Qumm nayo ni haram.<\/p>\n<p>Na wanayo riwaya wanayodai kuwa imepokelewa kwa As-Swaadiq kwamba, Allaah Anayo haram Yake ambayo ni Makkah, na Mtume Wake anayo haram yake ambayo ni Madiynah, na Amiyrul-Muuminiyna (\u00b4Aliy) anayo haram yake ambayo ni Al-Kuufah, na sisi tunayo haram yetu ambayo ni Qumm.<\/p>\n<p>Na Kar-balaa kwa Mashia ni bora kuliko Al-Ka\u00b4abah. Imekuja katika Kitabu \u2018Bihaarul-Anwaar\u2019 kutoka kwa Abu \u00b4Abdillaah kwamba kasema:<\/p>\n<p>&#8220;Hakika Allaah Aliiteremshia Al-Ka\u00b4abah wahyi (ufunuo) lau kama si udongo wa Karbalaa nisingelikufanya bora, na lau kama si mwili wa yule aliyeko katika udongo wa Karbalaa nisingekuumba, wala nisingeumba nyumba ambayo kwayo umejifakharisha, basi tulia na uwe ni Mkia dhalili na si mwenye kibri kwa ardhi ya Karbalaa, la sivyo nitakutupa katika Jahannam.&#8221;(1)<\/p>\n<p>Bali Raafidhwah wanaona kuzuru kaburi la Husayn huko Karbala ni bora kuliko nguzo ya tano ya Uislamu (Hijjah)!!<\/p>\n<p>Amesema Al-Majlisiy katika kitabu chake \u2018Bihaarul-Anwaar\u2019 kutoka kwa Bashiyr Ad-Dahaan amesema: &#8220;Nilimuuliza Abu \u00b4Abdillaah: \u201cEndapo itanipita Hijjah kisha nikaenda katika kaburi la Husayn? Akasema: Vizuri sana ewe Bashiyr, Muumini yeyote atakaeliendea kaburi la Husayn hali ya kutambua haki yake, katika siku ambayo si siku ya \u2018Iyd, basi huandikiwa thawabu za Hijjah 20 na \u00b4Umrah 20 zenye kukubaliwa, na thawabu za kushiriki katika vita 20 vya Jihaad pamoja na Mtume au Imamu muadilifu, na atakayeliendea siku ya \u00b4Arafah hali ya kujua haki zake basi huandikiwa thawabu za Hijjah 1000 na \u00b4Umrah 1000 zenye kukubaliwa, na thawabu za kupigana Jihaad 1000 pamoja na Mtume au Imamu muadilifu.<\/p>\n<p>Pia katika kitabu hicho hicho wametaja kwamba wanaozuru kaburi la Husayn huko Karbalaa ni watu safi, na wanaokuwa wamesimama \u00b4Arafah ni watoto wa Zinaa!!<\/p>\n<p>Imepokewa toka kwa \u00b4Aliy bin Asbaatw kwamba kapokea toka kwa Abu \u00b4Abdillaah kuwa kasema: \u201cHakika Allaah Mtukufu Anaanza kuwatazama wanaozuru kaburi la Husayn usiku wa kuamkia \u00b4Arafah. Akasema: Nikamuuliza, kabla hajawatazama walioko katika kisimamo cha \u00b4Arafah? Akasema: Ndio, nikamuuliza, kwanini iwe hivyo? Akasema: \u201cKwa sababu katika watu walioko \u00b4Arafah mna watoto wa zinaa tofauti na wale walioko Karbalaa hakuna mtoto wa zinaa kati yao.&#8221;(2)<\/p>\n<p>Bali kiongozi wao mkuu (wa hivi sasa) \u00b4Aliy As-Sistaaniy katika kitabu chake \u2018Minhaajus-Swaalihiyn\u2019 amefadhilisha kuswali katika makaburi kuliko kuswali katika Misikiti!!<\/p>\n<p>Kasema katika mas-alah nambari 562: \u201cInapendeza kuswali katika makaburi ya Maimamu (\u00b4Alayhimus-Salaam) bali imesemekana kuwa ni bora kuliko kuswali Misikitini, na imepokewa kwamba kuswali katika kaburi la Imamu \u00b4Aliy bin Abi Twaalib (\u2018Alayhis Salaam) ina ubora wa Swalah laki mbili.\u201d(3)<\/p>\n<p>Bali Shaykh wao \u2018Abbaas Al-Kaashaaniy katika kitabu chake \u2018MaswaabiyhulJinaan\u2019 kapituka mipaka katika kuitukuza Karbalaa mpaka akasema: &#8220;Hapana shaka kwamba Karbalaa ndio sehemu takatifu zaidi katika Uislamu, na imepewa utukufu ambao haikupewa sehemu yoyote ardhini, na hii ni kwa mujibu wa dalili nyingi zilizopokewa kuhusu jambo hili, hivyo ikafanywa ndio ardhi ya Allaah iliyotukuzwa na kubarikiwa, na ni ardhi iliyonyenyekea, na ni ardhi iliyoteuliwa na ndio haram ya Allaah yenye baraka na amani, na ndio haram ya Mtume, na ndio kitovu cha Uislamu, na ni katika sehemu ambazo Allaah Anapenda kuombwa na kuabudiwa katika sehemu hizo, na ndio ardhi ambayo udongo wake ni tiba, hakika sifa hizi na nyinginezo zilizopo katika ardhi ya Karbalaa, hazipatikani katika sehemu yoyote ardhini, hata katika AlKa\u00b4abah.&#8221;(4)<\/p>\n<p>Vilevile imekuja katika kitabu \u2018Al-Mazaar\u2019 cha Muhammad An-Nu\u2019umaan, wenyewe wanamuita \u2018Ash-Shaykhul-Mufiyd\u2019 akielezea ubora wa Masjid AlKuufah: Imepokewa toka kwa Abu Ja\u2019afar Al-Baaqir amesema: &#8220;Lau watu wangejua fadhila zinazopatikana katika Masjid Al-Kuufah basi wangeliuandalia matumizi na vipandwa kutoka sehemu mbalimbali ili kuuendea, hakika Swalah ya faradhi katika Msikiti huo ni sawa na Hijjah, na Swalah ya Sunnah ni sawa na `Umrah.&#8221;(5)<\/p>\n<p>Vilevile imekuja katika kitabu hicho hicho katika mlango aliyouita \u2018Yasemwayo wakati wa kusimama katika kaburi\u2019 kwamba mwenye kumzuru Husayn anatakiwa kuashiria kwa mkono wake wa kuume, na aseme katika du\u00b4aa ndefu kabisa, miongoni mwake maneno yafuatayo: &#8220;Nimekujia kukuzuru, nikitaraji uthibitishwe unyayo wangu, na nina yaqini kwamba Allaah Mtukufu Anawaondolea waja Wake matatizo yao kupitia kwenu, na kwa sababu yenu anateremsha Rahma, na kupitia nyinyi anaizuia ardhi isiwadidimize watu wake, na kupitia nyinyi kayathibitisha majabali yake. Ninamuelekea Mola wangu kupitia kwenu ili mnikidhie haja zangu, na mnisamehe madhambi yangu.&#8221; (6)<\/p>\n<p>Hebu tazama ndugu msomaji jinsi watu hawa walivyotumbukia katika ushirikina, kwa kumuomba asiyekuwa Allaah awakidhie haja zao, na kuomba kusamehewa madhambi yao kwa asiyekuwa Allaah, vipi wamefikia katika hali hii, na ilihali Allaah Anasema:<\/p>\n<p><em>[Hakuna anayesamehe madhambi ila Allaah.]\u00a0<\/em> [Al-\u00b4Imraan 03: 135].<\/p>\n<p>Tunamuomba Allaah Atukinge na ushirikina. *<\/p>\n<blockquote><p>\u00a0<em>1)\u00a0Bihaarul-Anwaar 10\/107.<\/em><\/p>\n<p><em>2)\u00a0Bihaarul-Anwaar cha Al-Majlisiy 85\/98.<\/em><\/p>\n<p><em>3)\u00a0Minhaajus-Swalihiyn cha As-Sistaaniy 1\/187.<\/em><\/p>\n<p><em>4)\u00a0Maswaabiyhul-Jinaan cha \u00b4Abbaas Al-Kaashaaniy uk. 360.<\/em><\/p>\n<p><em>5)\u00a0Kitaabul-Mazaar cha Shaykh Al-Mufiyd uk. 20.<\/em><\/p>\n<p><em>\u00a06)\u00a0Kitaabul-Mazaar cha Shaykh Al-Mufiyd uk. 99.<\/em><\/p>\n<p><em>* MIONGONI MWA ITIKADI ZA MASHIA \u2018Abdullaah Bin Muhammad As- Salafiy Uk \/ 32-33<\/em><\/p><\/blockquote>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>NI IPI ITIKADI YA MASHIA KUHUSU NAJAF NA KARBALAA, NA JE, KUNA FADHLA GANI KATIKA KUZURU SEHEMU HIZO ? Mashia wanaitakidi sehemu yalipo makaburi ya watu waliodai kuwa ni Maimamu wao, au ambao ni Maimamu kweli, kwa sehemu hizo ni sehemu takatifu, hivyo Al-Kuufa ni haram (sehemu takatifu), pia Karbalaa ni haram, na Qumm nayo [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":10740,"comment_status":"open","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[81],"tags":[],"class_list":["post-4285","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-itikadi-za-mashia"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4285","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=4285"}],"version-history":[{"count":3,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4285\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":10762,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4285\/revisions\/10762"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/10740"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=4285"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=4285"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=4285"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}