{"id":25380,"date":"2025-12-02T10:31:00","date_gmt":"2025-12-02T10:31:00","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=25380"},"modified":"2025-12-03T11:55:09","modified_gmt":"2025-12-03T11:55:09","slug":"hali-ya-vikosi-hivi-ilikuwa-kama-ifuatavyo","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/hali-ya-vikosi-hivi-ilikuwa-kama-ifuatavyo\/","title":{"rendered":"HALI YA VIKOSI HIVI ILIKUWA KAMA IFUATAVYO"},"content":{"rendered":"<p>Hali ya Vikosi Hivi Ilikuwa kama Ifuatavyo:<br \/>\n<span style=\"color: #333300;\"><strong>1) Kikosi cha Saifu Al-Bahri,<\/strong><\/span> Mnamo mwezi wa Ramadhani mwaka wa 1 A.H., sawa na mwaka 623 C.E, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) alimpa uongozi wa kikosi hiki <span style=\"color: #ff6600;\">Hamza bin Abdi Al-Muttalib<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) na aliongoza watu thelathini katika Muhajirina. Alitumwa akazuie msafara wa kibiashara wa Makuraishi uliokuwa ukitoka Sham. Katika msafara huo alikuwemo<span style=\"color: #ff6600;\"> Abu Iahli bin Hisham,<\/span> akiwaongoza watu mia tatu. Walipofika <span style=\"color: #ff6600;\">Saiful-al-Bahri<\/span> kwa upande wa Al-Idhi, wakakutana na wakapanga safu kwa ajili ya vita. Majdy bin Amru A-Juhani alikuwa ni rafiki wa makundi yote mawili, akawazuia kupigana. Hii ilikuwa ndiyo bendera ya kwanza ya vita iliyotungikwa na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>), ilikuwa nyeupe na alikabidhiwa Aba Marthad Kanazi bin Huswaini Al-Ghanawy kuibeba.<br \/>\n<span style=\"color: #993300;\"><strong>2) Kikosi cha Rabighi:<\/strong><\/span> Katika mwezi wa Shawwal mwakail A.H, mwafaka na mwezi wa April mwaka wa 623 C.E. Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) alimpeleka <span style=\"color: #ff6600;\">Ubaida bin al-Harith bin Abdul Muttalib<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) akiongoza Muhujiriml sitini wakiwa na farasi, njiani wakakutana na <span style=\"color: #ff6600;\">Abu Sufyani<\/span> akiwa<br \/>\nanaongoza kikosi cha watu mia -mbili katika jangwa la Rabighi. Makundi mawili haya yalitupiana mishale, lakini havikutokea vita. Katika kikosi hiki walijiunga watu wawili na Uislamu kutoka katika Jeshi la Makka; nao ni <span style=\"color: #ff6600;\">Al-Miqdadi bin Amri Al-Bahrani<\/span>, na <span style=\"color: #ff6600;\">Utba bin Al-Maaziny.<\/span> Walitoka pamoja na maka\ufb01ri, ili hiyo ndiyo iwe njia ya kufika kwa Waislamu. Bendera ya Ubaida (Radhi za Allah ziwe juu yake) ilikuwa nyeupe na mbebaji wake alikuwa ni&#8217; <span style=\"color: #ff6600;\">Mistani bin Athatha bin Al-Muttahb bin Abdil Mana\ufb01<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake).<br \/>\n<span style=\"color: #993300;\"><strong>3) Kikosi cha Al-Kharar,<\/strong><\/span> katika mwezi wa Dhulqa\u2019duh mwaka wa 1 wa A.H. sawasawa na mwezi Mei mwaka 623 C .E. Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) alimpeleka tena <span style=\"color: #ff6600;\">Sa\u2019ad bin Abi Waqqasi<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) akiwaongoza watu ishirini kwa leng la kuuzuia msafara wa kibiashara wa Makuraishi na akachukua<br \/>\nahadi kutoka kwake kuwa asivuke Al-Kharrazi. Wakatoka hali ya kwenda usiku na wakiji\ufb01cha mchana. Walifika AL-Kharrazi asubuhi ya Alkhamisi, na wakakuta kuwa msafara umekwishapita kutoka siku iliyopita. Bendera ya Sa&#8217;ad (Radhi za Allah ziwe juu yake) ilikuwa nyeupe na mbebaji alikuwa ni Al-Miqdadi bin Amri (Radhi za Allah ziwe juu yake).<br \/>\n<span style=\"color: #993300;\"><strong>4) Ghazwa Al-Abwa,<\/strong><\/span> au Waddan: Katika mwezi wa Safar mwaka wa 2 A.H sawa na mwezi Agosti mwaka 623 C.E. Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) alitoka yeye mwenyewe baada ya kumfanya <span style=\"color: #ff6600;\">Sa&#8217;ad bin Ubada<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) kuwa Khalifa wa Madina, akiongoza kikosi cha watu sabini katika Muhajirina, alikwenda kwa madhumuni ya kuuzuia msafara wa biashara, mpaka wakafika Waddani bila kukutana na upinzani wowote.<br \/>\nKatika vita hivi Mtume (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) alifunga mkataba wa kusaidiana na <span style=\"color: #ff6600;\">Amru bin Makhashi Ad-Damari;<\/span> aliyekuwa<br \/>\nkiongozi na Bwana wa Banu Dumari katika zama zake.<br \/>\nMkataba ulikuwa kama ifuatavyo:-<br \/>\nWaraka huu kutoka kwa Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) kwenda kwa Banu Dhamrah,<br \/>\nkuw amani ya mali zao na maisha yao. Kwamba wana haki ya kunusuriwa kwa atakaye wakusudia kwa<br \/>\nubaya, isipukuwa watakapoipiga vita Dini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t); na kuwa Mtume (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) atakapowaita kwa ajili ya kumnusuru watamwitikia. (1)<\/p>\n<p>Hivi ndivyo vita vya kwanza alivyopigana Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>).<\/p>\n<p>Mtume (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) alikaa nje ya Madina kwa siku kumi na tano, bemdera yak\u00e9 ihikuwa nygupe na mchukuzi wa bendera hiyo alikuwa ni Hamza bin Abdil Muttalib (Radhi za Allah ziwe juu yake).<br \/>\n<span style=\"color: #993300;\"><strong>5) Vita vya Buwat;<\/strong><\/span> Ilipo\ufb01ka Rabiul Awwal mnamo mwaka wa 2 wa A.H. sawa na Septemba mwaka 623 C.E. Radhi za Allah ziwe juu yake wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) alitoka akiongoza watu mia mbili katika Masahaba wake ili kuuvamia msafara wa biashara wa Makuraishi, akiwemo <span style=\"color: #ff6600;\">Umayya bin Khalaf, Jumahi<\/span> na watu wengine mia moja katika Makuraishi, wakiwa na ngamia elfu mbili na mia tano. Ali\ufb01ka Buwat kwa upande wa Ridawi na<br \/>\nhakukutana na upinzani wowote. Katika vita hivi uongozi wa Madina alimwachia <span style=\"color: #ff6600;\">Sa&#8217;ad bin Muadhi<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake). Bendera yake ilikuwa nyeupe na mchukuzi wa bendera hiyo alikuwa ni Sa&#8217;ad bin Abu Waqqas (Radhi za Allah ziwe juu yake).<br \/>\n<span style=\"color: #993300;\"><strong>6) Vita vya Safwan;<\/strong><\/span> Ilipofika Rabiul Awwal mwaka wa 2 C.E. sawa na mwezi Septemba mwaka 623 C.E., <span style=\"color: #ff6600;\">Kurzi bin Jabir A17 Fihry<\/span> alifanya mashambulizi akiwa na askari wachache ka\ufb01ka kikosi cha Mushirikina katika eneo la malisho ya wanyama wa Madina na akanyang&#8217;anya baadhi ya mifugo. Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) alitoka akiwa na watu sabini katika Masahaba wake ili kumfukuza. Ali\ufb01ka mpaka katika jangwa<br \/>\nlinaloitwa Safwan katika upande wa Badri, lakini Kurzi na wenzake hawakupatikana, na akarejea bila kupigana vita. Vita hivi vinajulikana kwa jina la vita vya <span style=\"color: #ff6600;\">Badri vya kwanza,<\/span> na katika vita hivi uongozi wa Madina alipewa Zaid bin Haritha (Radhi za Allah ziwe juu yake), bendera ilikuwa nyeupe na mchukuzi wake alikuwa ni Ali bin Abu Twalib (Radhi za Allah ziwe juu yake).<br \/>\n<span style=\"color: #993300;\"><strong>7) Vita vya Dhil Ushairah;<\/strong><\/span> Katika mwezi wa Jumadal-al-Ula na Jumada-al-Akhirah mwaka wa 2 wa AH. sawa na Novemba na Desemba mwaka 623 C.E. Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) alitoka akiongoza watu mia moja na khamsini 150 na wengine wanasema kuwa walikuwa ni watu mia mbili 200 katika Muhajirina, waliotoka kwa hiari zao bila ya mtu yeyote kulazimishwa. Walitoka wakiwa na ngamia thalathini walokuwa wakiwapanda kwa zamu, na walitoka kwa lengo la kuingilia kati msafara wa biashara uliokuwa ukielekea Sham. Walikuwa wamekwisha pata khabari kupitia wapelelezi wake waliokuwa Makkah kuwa ndani ya msafara huo mna mali za Makuraishi. Alipofika mahali paitwapo <span style=\"color: #ff6600;\">Dhil Ushairah<\/span> akapata khabari kuwa msafara Umekwishapita siku nyingi. Msafara huo ndiyo uliosababisha vita vya Badri Kuu.<br \/>\nKulingana na mapokeo ya Ibn Ishaq, Mtume (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) alitoka mwishoni mwa Jamada-al-Ula, na kurejea mwanzoni mwa Jamadal Akhirah. Huenda hii ndiyo ikawa sababii ya watu wa somo la Sira kutofautiana katika kuainisha mwezi wa vita hivi.<br \/>\nKatika vita hivi Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) alifunga mkataba wa kutofanyiana uadui na <span style=\"color: #ff6600;\">Banu Mudliji<\/span> na washirika wao katika <span style=\"color: #ff6600;\">Banu Dhumra.<\/span> Uongozi wa Madina katika vita hivi alipewa <span style=\"color: #ff6600;\">Abu Salama bin Abdil Assad Al-Makhzoumy<\/span> (r.a). Bendera katika vita hivi ilikuwa ni nyeupe<br \/>\nna mbebaji wake alikuwa ni Hamza bin Abdil A1-Muttalib<br \/>\n(Radhi za Allah ziwe juu yake.)<br \/>\n<span style=\"color: #993300;\"><strong>8) Kikosi cha Nakhlah:<\/strong><\/span> Katika Mwezi wa Rajab mwaka wa pili AH. sawa na Januari mwaka 624 C.E. Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) alimpeleka <span style=\"color: #ff6600;\">Abdallah bin Jahshi Al- Assad<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake), kwenye mji wa <span style=\"color: #ff6600;\">Nakhlah<\/span> akiwa anawaongoza watu kumi na wawili 12 katika Muhajirina, kila watu wawili<br \/>\nwalipokezana kumpanda ngamia mmoja.<\/p>\n<p>Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa amemuandikia barua na akamuamrisha kuwa\u00bb asiisome mpaka aenda mwendo wa siku mbili, kisha aisome. Kisha Abdullah akaenda baada ya siku mbili akaisoma, akakuta maneno yafuatayo: <span style=\"color: #0000ff;\">\u201dUtakapoyangalia maandishi yangu haya nenda mpaka Nakhlah kati ya Makka na Taif, ukatishe msafara wa biashara wa Makuraishi na kusanya khabari zao.\u201d<\/span> Akasema: &#8220;Nimesikia na nimetii.&#8221; Akawaeleza wenzake khabari hiyo, nakuwa yeye hawalazimishi kwa hiyo mwenye kupenda kufa shahidi (kufa katika vita vya kuitetea Dini ya Mwenyezi Mungu) na asimame, na mwenye kuichukia arudi. Ama mimi nina simama, wakasimama wote, isipokuwa <span style=\"color: #ff6600;\">Sa\u2019ad bin Abi Waqqas<\/span><br \/>\n(Radhi za Allah ziwe juu yake) <span style=\"color: #ff6600;\">na Utba bin Ghazwan<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) walimpoteza ngamia wao ambaye walikuwa wanapokezana kumpanda, wakabakia nyuma wakimtafuta.<br \/>\n<span style=\"color: #ff6600;\">Abdullah bin Jahshi<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) alikwenda mpaka aka\ufb01ka Nakhlah, ukapita msafara wa biashara wa Makuraishi ukiwa umebeba zabibu, ngozi na biashara zingine. Katika msafara huo alikuwepo Amri bin Al-Hadhramy, \u2019Uthman na Nawfal, watoto wawili wa <span style=\"color: #ff6600;\">Abdill-ah bin Al-Mughira,<\/span> na Al-Hakam bin<br \/>\nKisan, huru wa <span style=\"color: #ff6600;\">Banu Al-Mughirab<\/span> Waislamu wakashauriana na wakasema: &#8220;Sisi tumo katika siku ya mwisho ya mwezi wa Rajab, mwezi mtukufu, iwapo tutapigana nao tutakuwa tumevunja heshima ya mwezi mtukufu na iwapo tutawaacha, usiku huu wataingia Haram.\u201d Waliamua kupigana nao na <span style=\"color: #ff6600;\">Amri bin Al-Hadhrami<\/span> aliuawa kwa kupigwa mshale. Wakamteka <span style=\"color: #ff6600;\">\u2019Uthmani na Al-Hakam.<\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">Nawfal<\/span> aliponyoka.<br \/>\nKisha waka\ufb01ka na ule msafara na wale mateka wawili mpaka Madina, wakiwa wametenga katika mali hiyo khumsi (moja ya tano). Na hili ndilo likawa fungu la khumsi ya kwanza kutolewa katika Uislamu. Wakawa ni watu wa kwanza kuuawa katika Uislamu na wakawa ni mateka wawili wa mwanzo katika Uislamu.<br \/>\nMtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) alishutumu lile ambalo walilolifanya na akasema: <span style=\"color: #0000ff;\">&#8220;Sikuwaamrisha kupigana katika mwezi mtukufu\u201d,<\/span> akasimamisha kufanya jambo lolote kuhusu mali ya msafara na wale mateka wawili. Mushirikina walipata sababu ya kuwatuhumu Waislamu kuwa wao wamehalalisha yale ambayo Ameyaharamisha Mwenyezi Mungu. Maneno mengi ya hapa na pale yalizungumzwa<br \/>\nmpaka wahyi ukashuka uliotoa jawabu ambalo lilionyesha kwamba vitendo vya Mushirikina vilikuwa vibaya sana kuliko vitendo vya Waislamu :<\/p>\n<h4 style=\"text-align: right;\"><span style=\"color: #008000;\">\u064a\u064e\u0633\u06e1\u0640\u0654\u064e\u0644\u064f\u0648\u0646\u064e\u0643\u064e \u0639\u064e\u0646\u0650 \u0671\u0644\u0634\u0651\u064e\u0647\u06e1\u0631\u0650 \u0671\u0644\u06e1\u062d\u064e\u0631\u064e\u0627\u0645\u0650 \u0642\u0650\u062a\u064e\u0627\u0644\u0656 \u0641\u0650\u064a\u0647\u0650\u06d6 \u0642\u064f\u0644\u06e1 \u0642\u0650\u062a\u064e\u0627\u0644\u065e \u0641\u0650\u064a\u0647\u0650 \u0643\u064e\u0628\u0650\u064a\u0631\u065e\u06da \u0648\u064e\u0635\u064e\u062f\u0651\u064c \u0639\u064e\u0646 \u0633\u064e\u0628\u0650\u064a\u0644\u0650 \u0671\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u0650 \u0648\u064e\u0643\u064f\u0641\u06e1\u0631\u064f\u06e2 \u0628\u0650\u0647\u0650\u06e6 \u0648\u064e\u0671\u0644\u06e1\u0645\u064e\u0633\u06e1\u062c\u0650\u062f\u0650 \u0671\u0644\u06e1\u062d\u064e\u0631\u064e\u0627\u0645\u0650 \u0648\u064e\u0625\u0650\u062e\u06e1\u0631\u064e\u0627\u062c\u064f \u0623\u064e\u0647\u06e1\u0644\u0650\u0647\u0650\u06e6 \u0645\u0650\u0646\u06e1\u0647\u064f \u0623\u064e\u0643\u06e1\u0628\u064e\u0631\u064f \u0639\u0650\u0646\u062f\u064e \u0671\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u0650\u06da \u0648\u064e\u0671\u0644\u06e1\u0641\u0650\u062a\u06e1\u0646\u064e\u0629\u064f \u0623\u064e\u0643\u06e1\u0628\u064e\u0631\u064f \u0645\u0650\u0646\u064e \u0671\u0644\u06e1\u0642\u064e\u062a\u06e1\u0644\u0650\u06d7\u00a0<\/span><\/h4>\n<p>\u201d<span style=\"color: #0000ff;\">Wanakuuliza juu ya kupigana vita katika mwezi mtakatifu. Sema: Kupigana vita wakati huo ni dhambi kubwa. Lakini kuzuilia watu wasende katika Njia ya Mwenyezi Mungu na kumkanusha Yeye, na kuzuilia watu wasende kwenye Msikiti Mtakatifu na kuwatoa watu wake humo, ni makubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Na fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa.<\/span>\u201d (2:217)<br \/>\nKwa hakika wahyi huu umeweka wazi, kuwa mzozo ambao ulizushwa na Mushirikina ili kuleta mashaka katika mwendo wa wapiganaji Waislamu, mzozo huo hauna sababu yoyote ya kukubalika, kwani mambo yote matukufu na matakatifu yalikwisha vunjwa katika kuupiga vita Uislamu na kuwakandamiza waumini wake. Hivi Waislamu hawakuwa wakiishi katika mji mtukufu wa Makka? wakati walipoamua kuwanyang\u2019anya mali zao na kutaka kumnuuwa Mtume wao?;<br \/>\nSasa ni jambo gani ambalo limeyarejeshea haya mambo utukufu wake ghafla?; kukawa kuyavunja kwake ni fedheha?.<br \/>\nKwa hakika madai ya Mushirikina ni madai yaliyojengwa juu ya ubaya na uchafu. Baada ya hapo, Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) aliwaachia huru wale mateka wawili na akalipa fidia kwa mawalii wa wale watu wawili waliouliwa. (2)<br \/>\nHivyo ndivyo vikosi vya uchunguzi na vita vilivyotokea kabla ya Badri, haukutokea uporaji wa mali wala uuaji katika vita hivyo isipokuwa baada ya yale ambayo waliyatenda Mushirikina katika uongozi wa <span style=\"color: #ff6600;\">Kurzi bin Iabir Al-Fihry. <\/span>Utakuta mwanzo wa yote hayo unatokana na Mushirikina pamoja na yale ambayo walikuwa wameyafanya kabla ya hapo.<br \/>\nBaada ya kutokea yaliyotokea katika kikosi cha <span style=\"color: #ff6600;\">Abdillah bin Jahshi<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) ilithibiti khofu ya Mushirikina, na wakaiona hatari ya kweli ikiwakabili. Wakajiingiza katika lile ambalo walikuwa wanaogopa kujihusisha nalo na wakajua kwamba Madina iko katika ulinzi madhubuti, na inafatilia harakati zao zote za biashara na kwamba Waislamu walikuwa na uwezo wa kwenda takriban umbali wa maili mia tatu, wakauwa watu na kuwateka wengine, na kuzichukua mali zao, na wakarudi hali ya kuwa wako salama wakiwa na ngawira.<\/p>\n<p>Mushirikina walihisi kuwa biashara yao ya Sham iko hatarini. Badala ya kuzinduka na kuacha upotevu na kuishika njia ya wema na utulivu kama walivyofanya<span style=\"color: #ff6600;\"> Juhaina<\/span> na <span style=\"color: #ff6600;\">Banuu Dhumra<\/span>, wao wakaongeza chuki na ghadhabu. Wakashikilia vigogo na wakubwa wao wengine juu ya yale ambayo walikuwa<br \/>\nwanakamiwa na wanatishwa kwayo huko nyuma. Miongoni mwa hayo ni kuwateketeza Waislamu katika mji wao, na huku ndiko kurukwa na akili ambako kuliwaleta Badri ili kupigana na Waislamu.<br \/>\nAma kwa upande wa Waislamu, Mwenyezi Mungu (s.w.t) Aliwafaradhisha kupigana baada ya tukio la kikosi cha <span style=\"color: #ff6600;\">Abdillah bin Jahsh<\/span>i (Radhi za Allah ziwe juu yake), katika mwezi wa Shaaban, mwaka wa<br \/>\n2 A. H. na katika hilo Mwenyezi Mungu (s.w.t) Akateremsha<br \/>\naya nyingi zilizowazi:<\/p>\n<div class=\"aya_text\" style=\"text-align: right;\"><span style=\"color: #008000;\">\u0648\u064e\u0642\u064e\u0670\u062a\u0650\u0644\u064f\u0648\u0627\u0652 \u0641\u0650\u064a \u0633\u064e\u0628\u0650\u064a\u0644\u0650\u00a0<b>\u0671\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u0650<\/b>\u00a0\u0671\u0644\u0651\u064e\u0630\u0650\u064a\u0646\u064e \u064a\u064f\u0642\u064e\u0670\u062a\u0650\u0644\u064f\u0648\u0646\u064e\u0643\u064f\u0645\u06e1 \u0648\u064e\u0644\u064e\u0627 \u062a\u064e\u0639\u06e1\u062a\u064e\u062f\u064f\u0648\u0653\u0627\u0652\u06da \u0625\u0650\u0646\u0651\u064e\u00a0<b>\u0671\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u064e<\/b>\u00a0\u0644\u064e\u0627 \u064a\u064f\u062d\u0650\u0628\u0651\u064f \u0671\u0644\u06e1\u0645\u064f\u0639\u06e1\u062a\u064e\u062f\u0650\u064a\u0646\u064e\u00a0<label>(190)<\/label>\u00a0\u0648\u064e\u0671\u0642\u06e1\u062a\u064f\u0644\u064f\u0648\u0647\u064f\u0645\u06e1 \u062d\u064e\u064a\u06e1\u062b\u064f \u062b\u064e\u0642\u0650\u0641\u06e1\u062a\u064f\u0645\u064f\u0648\u0647\u064f\u0645\u06e1 \u0648\u064e\u0623\u064e\u062e\u06e1\u0631\u0650\u062c\u064f\u0648\u0647\u064f\u0645 \u0645\u0651\u0650\u0646\u06e1 \u062d\u064e\u064a\u06e1\u062b\u064f \u0623\u064e\u062e\u06e1\u0631\u064e\u062c\u064f\u0648\u0643\u064f\u0645\u06e1\u06da \u0648\u064e\u0671\u0644\u06e1\u0641\u0650\u062a\u06e1\u0646\u064e\u0629\u064f \u0623\u064e\u0634\u064e\u062f\u0651\u064f \u0645\u0650\u0646\u064e \u0671\u0644\u06e1\u0642\u064e\u062a\u06e1\u0644\u0650\u06da \u0648\u064e\u0644\u064e\u0627 \u062a\u064f\u0642\u064e\u0670\u062a\u0650\u0644\u064f\u0648\u0647\u064f\u0645\u06e1 \u0639\u0650\u0646\u062f\u064e \u0671\u0644\u06e1\u0645\u064e\u0633\u06e1\u062c\u0650\u062f\u0650 \u0671\u0644\u06e1\u062d\u064e\u0631\u064e\u0627\u0645\u0650 \u062d\u064e\u062a\u0651\u064e\u0649\u0670 \u064a\u064f\u0642\u064e\u0670\u062a\u0650\u0644\u064f\u0648\u0643\u064f\u0645\u06e1 \u0641\u0650\u064a\u0647\u0650\u06d6 \u0641\u064e\u0625\u0650\u0646 \u0642\u064e\u0670\u062a\u064e\u0644\u064f\u0648\u0643\u064f\u0645\u06e1 \u0641\u064e\u0671\u0642\u06e1\u062a\u064f\u0644\u064f\u0648\u0647\u064f\u0645\u06e1\u06d7 \u0643\u064e\u0630\u064e\u0670\u0644\u0650\u0643\u064e \u062c\u064e\u0632\u064e\u0627\u0653\u0621\u064f \u0671\u0644\u06e1\u0643\u064e\u0670\u0641\u0650\u0631\u0650\u064a\u0646\u064e\u00a0<label>(191)<\/label>\u00a0\u0641\u064e\u0625\u0650\u0646\u0650 \u0671\u0646\u062a\u064e\u0647\u064e\u0648\u06e1\u0627\u0652 \u0641\u064e\u0625\u0650\u0646\u0651\u064e\u00a0<b>\u0671\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u064e<\/b>\u00a0\u063a\u064e\u0641\u064f\u0648\u0631\u065e \u0631\u0651\u064e\u062d\u0650\u064a\u0645\u065e\u00a0<label>(192)<\/label>\u00a0\u0648\u064e\u0642\u064e\u0670\u062a\u0650\u0644\u064f\u0648\u0647\u064f\u0645\u06e1 \u062d\u064e\u062a\u0651\u064e\u0649\u0670 \u0644\u064e\u0627 \u062a\u064e\u0643\u064f\u0648\u0646\u064e \u0641\u0650\u062a\u06e1\u0646\u064e\u0629\u065e \u0648\u064e\u064a\u064e\u0643\u064f\u0648\u0646\u064e \u0671\u0644\u062f\u0651\u0650\u064a\u0646\u064f\u00a0<b>\u0644\u0650\u0644\u0651\u064e\u0647\u0650<\/b>\u06d6 \u0641\u064e\u0625\u0650\u0646\u0650 \u0671\u0646\u062a\u064e\u0647\u064e\u0648\u06e1\u0627\u0652 \u0641\u064e\u0644\u064e\u0627 \u0639\u064f\u062f\u06e1\u0648\u064e\u0670\u0646\u064e \u0625\u0650\u0644\u0651\u064e\u0627 \u0639\u064e\u0644\u064e\u0649 \u0671\u0644\u0638\u0651\u064e\u0670\u0644\u0650\u0645\u0650\u064a\u0646\u064e\u00a0<label>(193)<\/label><\/span><\/div>\n<div class=\"aya_text\" style=\"text-align: left;\"><span style=\"color: #0000ff;\">\u201cNa piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui.<\/span><\/div>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\">Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipo kutoeni; kwani fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa. Wala msipigane nao kwenye Msikiti Mtakatifu mpaka wakupigeni huko. Wakikupigeni huko basi nanyi pia wapigeni. Na hivi ndivyo yalivyo malipo ya makafiri.<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\">Lakini wakiacha basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\">Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina, na Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu. Na kama wakiacha basi usiweko uadui ila kwa wenye kudhulumu.<\/span><br \/>\nKisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) Aliteremsha aya za namna nyingine, anawafundisha namna ya kupigana, kuwahimiza na kuwawekea wazi baadhi ya hukumu:<\/p>\n<p style=\"text-align: right;\"><span style=\"color: #008000;\">\u0641\u064e\u0625\u0650\u0630\u064e\u0627 \u0644\u064e\u0642\u0650\u064a\u062a\u064f\u0645\u064f \u0671\u0644\u0651\u064e\u0630\u0650\u064a\u0646\u064e \u0643\u064e\u0641\u064e\u0631\u064f\u0648\u0627\u0652 \u0641\u064e\u0636\u064e\u0631\u06e1\u0628\u064e \u0671\u0644\u0631\u0651\u0650\u0642\u064e\u0627\u0628\u0650 \u062d\u064e\u062a\u0651\u064e\u0649\u0670\u0653 \u0625\u0650\u0630\u064e\u0627\u0653 \u0623\u064e\u062b\u06e1\u062e\u064e\u0646\u062a\u064f\u0645\u064f\u0648\u0647\u064f\u0645\u06e1 \u0641\u064e\u0634\u064f\u062f\u0651\u064f\u0648\u0627\u0652 \u0671\u0644\u06e1\u0648\u064e\u062b\u064e\u0627\u0642\u064e \u0641\u064e\u0625\u0650\u0645\u0651\u064e\u0627 \u0645\u064e\u0646\u0651\u064e\u06e2\u0627 \u0628\u064e\u0639\u06e1\u062f\u064f \u0648\u064e\u0625\u0650\u0645\u0651\u064e\u0627 \u0641\u0650\u062f\u064e\u0627\u0653\u0621\u064b \u062d\u064e\u062a\u0651\u064e\u0649\u0670 \u062a\u064e\u0636\u064e\u0639\u064e \u0671\u0644\u06e1\u062d\u064e\u0631\u06e1\u0628\u064f \u0623\u064e\u0648\u06e1\u0632\u064e\u0627\u0631\u064e\u0647\u064e\u0627\u06da \u0630\u064e\u0670\u0644\u0650\u0643\u064e\u06d6 \u0648\u064e\u0644\u064e\u0648\u06e1 \u064a\u064e\u0634\u064e\u0627\u0653\u0621\u064f\u00a0<b>\u0671\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u064f<\/b>\u00a0\u0644\u064e\u0671\u0646\u062a\u064e\u0635\u064e\u0631\u064e \u0645\u0650\u0646\u06e1\u0647\u064f\u0645\u06e1 \u0648\u064e\u0644\u064e\u0670\u0643\u0650\u0646 \u0644\u0651\u0650\u064a\u064e\u0628\u06e1\u0644\u064f\u0648\u064e\u0627\u0652 \u0628\u064e\u0639\u06e1\u0636\u064e\u0643\u064f\u0645 \u0628\u0650\u0628\u064e\u0639\u06e1\u0636\u0656\u06d7 \u0648\u064e\u0671\u0644\u0651\u064e\u0630\u0650\u064a\u0646\u064e \u0642\u064f\u062a\u0650\u0644\u064f\u0648\u0627\u0652 \u0641\u0650\u064a \u0633\u064e\u0628\u0650\u064a\u0644\u0650\u00a0<b>\u0671\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u0650<\/b>\u00a0\u0641\u064e\u0644\u064e\u0646 \u064a\u064f\u0636\u0650\u0644\u0651\u064e \u0623\u064e\u0639\u06e1\u0645\u064e\u0670\u0644\u064e\u0647\u064f\u0645\u06e1\u00a0<label>(4)<\/label>\u00a0\u0633\u064e\u064a\u064e\u0647\u06e1\u062f\u0650\u064a\u0647\u0650\u0645\u06e1 \u0648\u064e\u064a\u064f\u0635\u06e1\u0644\u0650\u062d\u064f \u0628\u064e\u0627\u0644\u064e\u0647\u064f\u0645\u06e1\u00a0<label>(5)<\/label>\u00a0\u0648\u064e\u064a\u064f\u062f\u06e1\u062e\u0650\u0644\u064f\u0647\u064f\u0645\u064f \u0671\u0644\u06e1\u062c\u064e\u0646\u0651\u064e\u0629\u064e \u0639\u064e\u0631\u0651\u064e\u0641\u064e\u0647\u064e\u0627 \u0644\u064e\u0647\u064f\u0645\u06e1\u00a0<label>(6)<\/label>\u00a0\u064a\u064e\u0670\u0653\u0623\u064e\u064a\u0651\u064f\u0647\u064e\u0627 \u0671\u0644\u0651\u064e\u0630\u0650\u064a\u0646\u064e \u0621\u064e\u0627\u0645\u064e\u0646\u064f\u0648\u0653\u0627\u0652 \u0625\u0650\u0646 \u062a\u064e\u0646\u0635\u064f\u0631\u064f\u0648\u0627\u0652\u00a0<b>\u0671\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u064e<\/b>\u00a0\u064a\u064e\u0646\u0635\u064f\u0631\u06e1\u0643\u064f\u0645\u06e1 \u0648\u064e\u064a\u064f\u062b\u064e\u0628\u0651\u0650\u062a\u06e1 \u0623\u064e\u0642\u06e1\u062f\u064e\u0627\u0645\u064e\u0643\u064f\u0645\u06e1\u00a0<label>(7)<\/label>\u00a0<\/span><\/p>\n<p style=\"text-align: left;\">\u201d<span style=\"color: #0000ff;\">Basi mnapo wakuta walio kufuru wapigeni shingoni mwao, mpaka mkiwadhoofisha wafungeni pingu. Tena waachilieni kwa hisani au wajikomboe, mpaka vita vipoe. Ndio hivyo. Na lau angeli taka Mwenyezi Mungu angeli washinda mwenyewe, lakini haya ni kwa sababu akutieni mitihani nyinyi kwa nyinyi. Na walio uliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu hatazipoteza a&#8217;mali zao.<\/span><\/p>\n<p style=\"text-align: left;\"><span style=\"font-size: revert; color: initial;\"><span style=\"color: #0000ff;\">Atawaongoza na awatengezee hali yao. Na atawaingiza katika Pepo aliyo wajuulisha. Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.<\/span>\u201d (47:47\u201c (3)<\/span><\/p>\n<p>Kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t) Amewataja kwa ubaya Wale ambao nyoyo zao zilitetemeka na kutaharuki wakati waliposikia imeteremka amri ya kupigana vita na maadui:<\/p>\n<p style=\"text-align: right;\"><span style=\"color: #008000;\">\u00a0\u0641\u064e\u0625\u0650\u0630\u064e\u0627\u0653 \u0623\u064f\u0646\u0632\u0650\u0644\u064e\u062a\u06e1 \u0633\u064f\u0648\u0631\u064e\u0629\u065e \u0645\u0651\u064f\u062d\u06e1\u0643\u064e\u0645\u064e\u0629\u065e \u0648\u064e\u0630\u064f\u0643\u0650\u0631\u064e \u0641\u0650\u064a\u0647\u064e\u0627 \u0671\u0644\u06e1\u0642\u0650\u062a\u064e\u0627\u0644\u064f \u0631\u064e\u0623\u064e\u064a\u06e1\u062a\u064e \u0671\u0644\u0651\u064e\u0630\u0650\u064a\u0646\u064e \u0641\u0650\u064a \u0642\u064f\u0644\u064f\u0648\u0628\u0650\u0647\u0650\u0645 \u0645\u0651\u064e\u0631\u064e\u0636\u065e \u064a\u064e\u0646\u0638\u064f\u0631\u064f\u0648\u0646\u064e \u0625\u0650\u0644\u064e\u064a\u06e1\u0643\u064e \u0646\u064e\u0638\u064e\u0631\u064e \u0671\u0644\u06e1\u0645\u064e\u063a\u06e1\u0634\u0650\u064a\u0651\u0650 \u0639\u064e\u0644\u064e\u064a\u06e1\u0647\u0650 \u0645\u0650\u0646\u064e \u0671\u0644\u06e1\u0645\u064e\u0648\u06e1\u062a\u0650\u06d6 \u0641\u064e\u0623\u064e\u0648\u06e1\u0644\u064e\u0649\u0670 \u0644\u064e\u0647\u064f\u0645\u06e1\u00a0<label>(20)<\/label>\u00a0<\/span><\/p>\n<p style=\"text-align: left;\"><span style=\"color: #0000ff;\">\u201d&#8230;Na inapo teremshwa Sura madhubuti na ikatajwa ndani yake khabari ya vita, utawaona wenye maradhi katika nyoyo zao wanakutazama mtazamo wa anaye zimia kwa mauti. Basi ni bora kwao\u201d<\/span> (47: 20)<br \/>\nKufaradhishwa vita na kufanya maandalizi kabla ya mapambano ni jambo lisiloepukika kutokana na hali<br \/>\nilivyokuwa. Endapo kungekuwa na jemedari ambaye aliyatathmini mazingira yaliyokuwepo angewaamrisha askari wake wajiandae kwa vita sembuse Mola Aliye Mjuzi na Mtukufu.<\/p>\n<p style=\"text-align: left;\">Hivyo, mazingira yalikuwa yanalazimisha kutokea kwa mapambano ya kumwaga damu kati ya haki na batili.<br \/>\nTukio la kikosi cha <span style=\"color: #ff6600;\">Abdillah bin Iahshi<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) lilikuwa ni pigo kubwa liliondosha kiburi chao na likawaacha wanapinduka pinduka mfano wa kaa la moto.<br \/>\nAya za kuamrisha vita zilifahamisha, kukaribia mapambano ya umwagaji damu na kuwa nusra na ushindi ni wa Waislamu. Tazama namna Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #0000ff;\">\ufdfb<\/span>) Alivyowaamrisha Waislamu kuwatoa Mushirikina mahali pale ambapo waliwatoa, na namna Anavyowafundisha jinsi askari atakavyowatendea mateka wake, na namna ya kumaliza nguvu za maadui mpaka vita vitakapokwisha. Hizi zote mpaka sasa ni ishara zenye kuonyesha ushindi kwa Waislamu, isipokuwa yote yalikuwa yamesitiriwa hadi atakapoonesha mtu binafsi uchungu wake.<br \/>\nKatika masiku haya, katika mwezi wa<span style=\"color: #ff6600;\"> Shaaban mwakawa 2 A.H.<\/span> sawa na Februari 624 C.E., Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #0000ff;\">\ufdfb<\/span>) Aliamrisha kugeuzwa kwa Qibla kutoka Baitul-Muqaddas na kuelekea Msikiti Mtukufu Wa Makka. Tukio hili liliwaathiri watu wenye imani dhaifu na wanafiki wa Kiyahudi ambao<br \/>\nwalikuwa wameingia katika safu za Waislamu kwa madhumuni ya kuzusha machafuko. Walifichuka na walirejea kwenye yale waliyokuwa wakiyafanya. Hivyo ndivyo zilivyosafika safu za Waislamu, zikaondokana na udanganyifu na khiyana.<br \/>\nQibla kugeuzwa ilikuwa ni ishara nzuri sana ya kuanza kwa Awamu mpya ya mapambano ya kukiteka Qibla hiki. Kwani ilikuwa muhali Qibla cha Waislamu kubaki mikononi mwa maadui zao. Baada ya maamrisho haya na ishara mbalimbali, Waislamu walizidisha hamasa, hali ya kupenda<br \/>\nJihadi, kukutana na maadui katika vita vyenye kupambanua mambo ya haki na batili, kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #0000ff;\">\ufdfb<\/span>) iliongozeka.<\/p>\n<hr \/>\n<p><em><span style=\"color: #ff6600;\">1) Al-Mawahibu Alladunniya, ]uzuu 1 Uk. 75.<\/span><\/em><\/p>\n<p><em><span style=\"color: #ff6600;\">2) Maelezo haya ya Ghazwa na Saraya, yamenukuliwa kutoka kitabu, Zaad Ma\u2019ad, juzuu 2, Uk 83-85; Ibn Hisham, Juzuu 1, Uk. 561-605. Rahmatun Lil \u2019Alamin, Juzuu 1, Uk. 115-116, Juzuu 2, Uk. 215-216, 468-470. Katika rejea hizi kuna tofauti za mtiririko wa kutajwa Saraya na Ghazawat. Rejea zetu<\/span><\/em><br \/>\n<em><span style=\"color: #ff6600;\">zimetegemea uhakiki wa Wanazuoni wawili Ibn Qayyim na Mansourpuri<\/span><\/em><\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\"><em>3) Abu \u2018Ala Maududi amehakiki na kusema kuwa Surntu Muhammad<\/em><\/span><br \/>\n<span style=\"color: #ff6600;\"><em>imeteremka kabla ya Badr (Angalia, Tafhimul Qur\u2019an, Iuzuu 5, Uk. 11-12).<\/em><\/span><\/p>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Hali ya Vikosi Hivi Ilikuwa kama Ifuatavyo: 1) Kikosi cha Saifu Al-Bahri, Mnamo mwezi wa Ramadhani mwaka wa 1 A.H., sawa na mwaka 623 C.E, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa) alimpa uongozi wa kikosi hiki Hamza bin Abdi Al-Muttalib (Radhi za Allah ziwe juu yake) na aliongoza watu thelathini katika Muhajirina. Alitumwa akazuie msafara wa [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":15476,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[57],"tags":[],"class_list":["post-25380","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-sera-ya-mtume"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/25380","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=25380"}],"version-history":[{"count":22,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/25380\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":25407,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/25380\/revisions\/25407"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/15476"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=25380"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=25380"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=25380"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}