{"id":25113,"date":"2025-10-27T11:48:30","date_gmt":"2025-10-27T11:48:30","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=25113"},"modified":"2025-10-29T10:28:07","modified_gmt":"2025-10-29T10:28:07","slug":"ujenzi-wa-matumaini-katika-jamii","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/ujenzi-wa-matumaini-katika-jamii\/","title":{"rendered":"UJENZI WA MATUMAINI KATIKA JAMII"},"content":{"rendered":"<hr \/>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"font-size: 18pt; color: #ff6600;\">AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM<\/span><\/p>\n<hr \/>\n<p>Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) alifanikiwa kusimamisha nguzo za jamii mpya kwa busara na hekima zake.<\/p>\n<p>Bila shaka hali hii iliacha athari kwa Waislamu. Alikuwa akiwaleta katika nuru ya elimu, alizitakasa nafsi zao na akawahimiza kufuata mambo mema na kuwa na mwenendo mzuri. Aidha alikuwa makini kuwafundisha maadili mema na ibada. Muhimu kuliko yote ni Utii kwa Allah (<span style=\"color: #0000ff;\">\ufdfb<\/span>) na Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>). Ipo siku mtu mmoja<br \/>\nalimwuliza Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>), <span style=\"color: #0000ff;\"><em>&#8220;Matendo yapi bora katika Uislamu?.&#8221; Mtume (\ufdfa) akajibu; \u201dWape watu chakula na toa salamu kwa unayemjua na kwa usiyemjua<\/em><\/span> (1)<\/p>\n<p>Abdullah bin Salam alisema; wakati Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) alipo\ufb01ka Madina nilikwenda kumwona, nilipohakikisha kuwa ndiye mwenyewe, nilijua kuwa si mrongo. Maneno ya mwanzo aliyoyasema ni ile ha_dithi yake: <em><span style=\"color: #0000ff;\">&#8220;Enyi watu toleaneni salamu, lisheni chakula, ungeni udugu, Salini usiku na hali ya kuwa watu wamelala mtaingia peponi kwa salama. &#8220;<\/span><\/em> (2)<\/p>\n<p>Katika hadithi yake nyingine, amesema; <em><span style=\"color: #0000ff;\">\u201dHataingia peponi yule ambaye jirani yake hajasalimika na shari zake&#8221;<\/span><\/em> (3)<\/p>\n<p>Akasema; <em><span style=\"color: #0000ff;\">&#8220;Mullslamu ni yule ambaye wamesalimika Waislamu wenzake na ulimi wake na mikono yake &#8221; Akasema; \u201dHawi Muumini kamili mmaja wenu mpaka ampendelee ndugu yake lile umbalo linaipenda nafsi yake&#8221;\u00a0<\/span> <\/em>(4) Akasema <em><span style=\"color: #0000ff;\">\u201dWaumini wote ni kama mtu mmoja, likiumwa jicho lake huumwa mwili mzima, na kikiumwa kichwa chake huumwa mwili mzima.&#8221;<\/span><\/em>\u00a0 (5) Akasema; <em><span style=\"color: #0000ff;\">\u201dMuumini kwa Muumini ni kama jengo moja, kila tofali hutia nguvu tofali jngine&#8221;<\/span><\/em>\u00a0 (6) Akasema; <em><span style=\"color: #0000ff;\">&#8220;Msibughudhiane, msihusudiane na msipeane migongo, Enyi waja wa Mwenyezi Mungu kuweni ndugu, si halali kwa Muislamu kumhama ndugu yake zaidi ya masiku matatu&#8221;<\/span><\/em> (7)<\/p>\n<p>Akasema;_<em><span style=\"color: #0000ff;\"> \u201dMuislamu ni ndugu ya Muislamu mwenzake hamdhulumu na hamsalimishi kwa adui; atakayemkidhia haja ndugu yake Muislamu, Mwenyezi Mungu Atamkidhia haja yake, na mwenye kumuondolea Muislamu mwenzake mateso na dhiki Mwenyezi Mungu Atamuondolea matesa ya siku ya Qiyama; na mwenye kumsitiri Muislamu, Mwenyezi Mungu Atamsitiri siku ya Qiyama.<\/span><\/em>&#8221; (8) Akasema; <em><span style=\"color: #0000ff;\">\u201dWahurumieni walio katika ardhi watawahurumia nyinyi walio mbinguni&#8221;<\/span><\/em> (9) Akasema; <em><span style=\"color: #0000ff;\">Si Muumini yule anaeshiba na hali ya kuwa jirani yake ni mwenye njaa ubavuni mwake&#8221;<\/span><\/em> (10)\u00a0 Akasema; <em><span style=\"color: #0000ff;\">\u201dKumtukana Muislamu ni kutoka katika utii wa Mwenyezi Mungu na kugombana naye ni uka\ufb01ri&#8221;<\/span><\/em> (11)<br \/>\nAlifudisha kwa vitendo kuwa, &#8220;jumbo la kuondosha uchafu njiani ni Sadaka na jambo hilo huhesabiwa kuwa ni tawi miongoni mwa matawi ya Imani&#8221; (12)<\/p>\n<p>Alikuwa akiwahimiza Waislamu kutoa katika mali zao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #0000ff;\">\ufdfb<\/span>) na alikuwa akiwatajia fadhila za kutoa na faida za kiroho zinazopatikana kwa kufanya hivyo. Alikuwa akisema;<\/p>\n<p><em><span style=\"color: #0000ff;\">\u201dSadaka huzima makosa na madhambi kama maji yanavyozima moto&#8221;<\/span> <\/em>(13)<br \/>\nAkasema; <em><span style=\"color: #0000ff;\">\u201dMuislamu yeyote atakayemvisha nguo Muislamu mwenzake, Mwenyezi Mungu Atamvisha nguo za kijani zilizo peponi. Muislamu yeyote atakayemlisha Muislamu mwenzake aliye na njaa Mwenyezi Mungu (\ufdfb) Atamlisha kutoka katika matunda ya peponi; na Muislamu yeyote atakayemnywesha Muislnmu mwenzake aliye na kiu, Mwenyezi Mungu Atamnywesha kutoka<\/span><\/em><br \/>\n<em><span style=\"color: #0000ff;\">katika mvinyo uliochundiwa&#8221;<\/span><\/em> (14) Na akasema; <em><span style=\"color: #0000ff;\">\u201dOgopeni moto ijapokuwu kwa kutoa kipande cha tende, na kama hukukipata basi angalau kwa maneno mazuri.&#8221;<\/span><\/em> (15)<br \/>\nPamoja na, yote hayo Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) alikuwa akihimiza watu kujizuia na kujichunga na tabia ya kuomba, na akawa anataja fadhila za kusubiri na kutosheka. Alifundisha kuwa kuomba ni dosari kwa mwenye kuoma isipokuwa kama mtu atakuwa hana budi amezidiwa sana.<\/p>\n<p>Kama alivyokuwa akiwazungumzia mambo ya ibada, fadhila na malipo yake kwa Mwenyezi Mungu, alikuwa akiwaletea ushahidi ili kuunganisha mambo ya kiroho na kimwili, kwa mujibu wa wahyi uliokuwa ukishuka kwake kutoka mbinguni.<\/p>\n<p style=\"text-align: left;\">Alikuwa anawasomea Qur&#8217;an ili kuwashajiisha kutekeleza majukumu na wajibu wao na wakati huhuo kutilia mkazo ufahamu na kuzingatia.<br \/>\nHivyo ndivyo alivyoinyanyua ari yao, matumaini yao, vipaji vyao na akawafunza maadili ya juu na mambo yaliyo bora mpaka wakawa ni sura ya kilele cha juu cha ukamilifu ulioeleweka katika historia ya watu baada ya Mitume.<br \/>\nAbdullah bin Masoud (r.a) amesema;<\/p>\n<p style=\"text-align: right;\"><span style=\"color: #808000;\">\u0645\u064e\u0646 \u0643\u0627\u0646\u064e \u0645\u064f\u0633\u0652\u062a\u064e\u0646\u064b\u0651\u0627 \u060c \u0641\u064e\u0644\u0652\u064a\u064e\u0633\u0652\u062a\u064e\u0646\u064e\u0651 \u0628\u0645\u0646 \u0642\u062f \u0645\u0627\u062a\u064e \u060c \u0641\u0625\u0646\u064e\u0651 \u0627\u0644\u062d\u064a\u064e\u0651 \u0644\u0627 \u062a\u064f\u0624\u0645\u064e\u0646\u064f \u0639\u0644\u064a\u0647 \u0627\u0644\u0641\u0650\u062a\u0652\u0646\u064e\u0629\u064f \u060c \u0623\u0648\u0644\u0626\u0643 \u0623\u0635\u062d\u0627\u0628\u064f \u0645\u062d\u0645\u062f &#8211; \u0635\u0644\u0649 \u0627\u0644\u0644\u0647 \u0639\u0644\u064a\u0647 \u0648\u0633\u0644\u0645 &#8211;\u00a0 \u0643\u0627\u0646\u0648\u0627 \u0623\u0641\u0636\u0644\u064e \u0647\u0630\u0647 \u0627\u0644\u0623\u0645\u0629 : \u0623\u0628\u0631\u064e\u0651\u0647\u0627 \u0642\u0644\u0648\u0628\u064b\u0627 \u060c \u0648\u0623\u0639\u0645\u0642\u064e\u0647\u0627 \u0639\u0644\u0645\u064b\u0627 \u060c \u0648\u0623\u0642\u0644\u064e\u0651\u0647\u0627 \u062a\u0643\u0644\u064f\u0651\u0641\u064b\u0627 \u060c \u0627\u062e\u062a\u0627\u0631\u0647\u0645 \u0627\u0644\u0644\u0647 \u0644\u0635\u062d\u0628\u0629 \u0646\u0628\u064a\u0650\u0651\u0647 \u060c \u0648\u0644\u0625\u0642\u0627\u0645\u0629 \u062f\u0650\u064a\u0646\u0647 \u060c \u0641\u0627\u0639\u0631\u0650\u0641\u0648\u0627 \u0644\u0647\u0645 \u0641\u0636\u0644\u064e\u0647\u0645 \u060c \u0648\u0627\u062a\u0628\u0639\u064f\u0648\u0647\u0645 \u0639\u0644\u0649 \u0623\u062b\u0631\u0647\u0645 \u060c \u0648\u062a\u0645\u0633\u064e\u0651\u0643\u0648\u0627 \u0628\u0645\u0627 \u0627\u0633\u062a\u064e\u0637\u064e\u0639\u0652\u062a\u064f\u0645 \u0645\u0646 \u0623\u062e\u0644\u0627\u0642\u0650\u0647\u0645 \u0648\u0633\u064a\u064e\u0631\u0650\u0647\u0645 \u060c \u0641\u0625\u0646\u0647\u0645 \u0643\u0627\u0646\u0648\u0627 \u0639\u0644\u0649 \u0627\u0644\u0647\u064f\u062f\u064e\u0649 \u0627\u0644\u0645\u0633\u062a\u0642\u064a\u0645<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\">&#8220;Mwenye kutaka kufuata basi na awafuate Wale walio kufa kwani ni vigumu kwa aliye hai kusalimika na \ufb01tna, hao ni Masahaba wa Muhammad (s.a.w) walikuwa ni wabora wa umma huu, wema zadi kwa nyoyo na wajuzi zaidi kwa elimu zao. Mwenyezi Mungu (s.w.t) Aliwachagua wao ili wawe masahaba wa Mtume Wake na wasimamishaji wa Dini Yake, kwa hivyo jueni ubora wao na fuateni nyayo zao, na shikamaneni na zile ambazo mnaziweza katika tabia zao, na mwenendo wao, kwani wao walikuwa kwenye uongofu<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #0000ff;\">ulionyoka.&#8221;<\/span> (16)<br \/>\nMtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) alikuwa ni mwenye kusi\ufb01ka kwa sifa za kitabia zilizo wazi na anasi\ufb01ka kwa ukamilifu wa vipaji na matendo mazuri, mambo yaliyofanya watu wampende na wawe tayari kumpigania na kujitolea uhai wao kwa ajili yake. Kila alipotamka Masahaba wake walifanya haraka kutekeleza aliloagiza, ilikuwa hatoi maelekezo yoyote au uongozi wowote isipokuwa walishindana katika kujipamba na mambo<br \/>\nhayo. \u00bb<br \/>\nKwa msingi huu Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) aliweza kujenga katika mji wa Madina jamii mpya iliyo bora na iliyotukuka na ambayo imefahamika katika historia. Aliweza kuyapatia ufumbuzi matatizo yote ya kijamii. Kuwafanya watu wafaidike na wastawi kutokana na ufumbuzi huo kwa kuhisi raha baada ya kuwa wametaabika kwa muda mrefu kwa sababu ya giza totoro lililokuwa limewafunika.<br \/>\nKwa mfano wa mambo kama haya ya kiimani na yaliyo makubwa ilikamilika misingi ya kuijenga jamii mpya ambayo ilipambana na kila mawimbi na matatizo kwa kipindi kirefu mpaka mwisho wa uelekeo wake, na ikaugeuza mapito ya masiku na historia.<\/p>\n<div>\n<hr \/>\n<\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">1) Sahihil Bukhari, Iuzuu 1,Uk. 6, 9.<\/span><\/em><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">2) Ttirmidhi, Ilm Majah na Darimy. Mishkatu Masabiih, Juzuu 1, Uk. 168.<\/span><\/em><\/div>\n<div><em><em><span style=\"color: #ff6600;\">3)<\/span><\/em><\/em><span style=\"color: #ff6600;\"> <em><span style=\"font-size: revert;\">Muslim, Mishkatu Masabiih, Juzuu 2, Uk. 422<\/span><br \/>\n<\/em><\/span><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">4) Sahihul Bukhari, Iuzuu 1, Uk. 6.<\/span><\/em><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">5) Muslim, Mishkatu Masabih, juzuu 2, Uk. 422<\/span><\/em><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">6) Bukhari na Muslim, Mishkatu Masabih, Juzuu 2, Uk.422<\/span><\/em><\/div>\n<div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">7)<\/span><\/em><span style=\"color: #ff6600;\"> <em>Sahihul Bukhari, Iuzuu 1, Uk. 6.<\/em><em><br \/>\n<\/em><\/span><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">8) Sahihul Bukhari, Muslim Miskaul masabihh Juzuu 2, Uk. 422<\/span><\/em><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">9) Sunan Abu Daud, Juzuu 2, Uk. 235. Iami&#8217;u Ttirmidhy, Juzuu 2, Uk. 14.<\/span><\/em><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">10) Bayhaqi, Mishkatul Masabih, Juzuu 2, Uk. 424.<\/span><\/em><\/div>\n<div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">11) Sahihil Bukhari, Iuzuu 2, Uk. 893.<\/span><\/em><\/div>\n<div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">12)<\/span><\/em><span style=\"color: #ff6600;\"> Bukhari na Muslim, Mishkatul Masabih, Iuzuu 1, Uk. 12, 167<em>.<\/em><em><br \/>\n<\/em><\/span><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">13) Ahmad, Ttirmidhy, Ibn Majah, Mishkatul Masabih, Juzuu 1, Uk. 14.<\/span><\/em><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">14) Sunan Abu Daud, ]ami&#8217;u Ttirmidhy, Mishkatul Masabih, Juzuu 1, Uk. 169.<\/span><\/em><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">15) Sahihil BukI1ari,]uzuu 1, Uk. 190, Iuzuu 2, Uk. 890.<\/span><\/em><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">16) Amepokea Razin, Mishkatul Masabih, Juzuu 1, Uk. 32.<\/span><\/em><\/div>\n<\/div>\n<\/div>\n<hr \/>\n<\/div>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM Mtume (\ufdfa) alifanikiwa kusimamisha nguzo za jamii mpya kwa busara na hekima zake. Bila shaka hali hii iliacha athari kwa Waislamu. Alikuwa akiwaleta katika nuru ya elimu, alizitakasa nafsi zao na akawahimiza kufuata mambo mema na kuwa na mwenendo mzuri. Aidha alikuwa makini kuwafundisha maadili mema na ibada. Muhimu kuliko yote ni Utii [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":15476,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[57],"tags":[],"class_list":["post-25113","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-sera-ya-mtume"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/25113","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=25113"}],"version-history":[{"count":8,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/25113\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":25158,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/25113\/revisions\/25158"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/15476"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=25113"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=25113"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=25113"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}