{"id":25097,"date":"2025-10-26T12:30:49","date_gmt":"2025-10-26T12:30:49","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=25097"},"modified":"2025-10-27T10:05:49","modified_gmt":"2025-10-27T10:05:49","slug":"kuunganisha-udungu-miongoni-mwa-waislamu","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/kuunganisha-udungu-miongoni-mwa-waislamu\/","title":{"rendered":"KUUNGANISHA UDUNGU MIONGONI MWA WAISLAMU"},"content":{"rendered":"<hr \/>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"font-size: 18pt; color: #ff6600;\">AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM<\/span><\/p>\n<hr \/>\n<p>Kama ambavyo Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) alivyosimama kwa ajili ya ujenzi wa msikiti, makao makuu ya kukutanika Waislamu na kuzoeana kwa siku mara tano, pia alisimamia kazi nyingine. Miongoni mwa mambo bora ambayo yamepokelewa na historia ni kazi ya kuunganisha udugu kati ya Muhajirina kutoka Makka na ndugu zao Maansar pale Madina.<br \/>\n<span style=\"color: #ff6600;\">Ibn Qayyim<\/span> alisema; \u201cKisha Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) aliunganisha udugu, kati ya Muhajirina kutoka Makka na Ansaar pale Madina, katika nyumba ya Anas bin Walikuwa watu sabini, nusu yao ni katika Muhajirina, na nusu ni katika Answar, alifanya udugu kati yao kwa kuliwazana na walikubaliana kurithiana baada ya kufa, hali hii iliindelea mpaka wakati wa vita vya Badri, Mwenyezi Mungu (\ufdfb) Alipoterenisha Maneno haya:-<\/p>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">\u00a0\u0648\u064e\u0623\u064f\u0648\u0652\u0644\u064f\u0648\u0627\u0652 \u0671\u0644\u06e1\u0623\u064e\u0631\u06e1\u062d\u064e\u0627\u0645\u0650 \u0628\u064e\u0639\u06e1\u0636\u064f\u0647\u064f\u0645\u06e1 \u0623\u064e\u0648\u06e1\u0644\u064e\u0649\u0670 \u0628\u0650\u0628\u064e\u0639\u06e1\u0636\u0656 \u0641\u0650\u064a \u0643\u0650\u062a\u064e\u0670\u0628\u0650 \u0671\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u0650\u06da<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\"><em>&#8220;Na ndugu wa nasaba wanastahikiana wenyewe kwa<\/em> wenyewe (katika kurithiana. Ndio ilivyo) katika kitabu cha Mwenyezi Mungu.. .<\/span>&#8221; (8:75) &#8216;<br \/>\nImeelezwa pia kuwa alijenga udugu kati ya Muhajirina wenyewe kwa wenyewe na baadhi kufanya udugu wa pili, na kauli iliyo madhubuti ni ile ya kwanza. Muhajirina walikuwa wametosheka na udugu wa Kiislamu, udugu wa mji, na udugu wa kuzaliwa. (1)<br \/>\nKama alivyosema Muhammad Al-Ghazaly, \u201dMaana ya udugu huu ilikuw\u00e9 ni kuyayuka kwa ung\u2019ang&#8217;anizi wa kijahilia na kuporomoka kwa tofau\ufb01 za uzawa, rangi na nghi. Kukawa hakuna, heshima, utukufu na ari isipokuwa kwa ajili ya Uislamu; na kwa sababu hiyo ikawa hatangulizwi mtu yeyote wala hawekwi nyuma isipokuwa kwa murua wake, na uchamungu wake.<\/p>\n<p>Kwa hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) aliufanya udugu huu kuwa ni mkataba uliopitishwa nakutekelezwa, na sio tamko lililokosa utekelezwaji; na aliufanya udugu huu kitendo kinachofumgamana na damu na mali, siyo maamkizi ambayo zinaporoja kwayo ndimi na haisimami kwayo athari yoyote.<\/p>\n<p>Hali ya udugu wa Kiislamu na hisia za kumjali mwenzake ziliondoa ubinafsi katika mioyo ya Waislamu na kuza matumda mazuri (2)\u00a0 Kwa mfano, Saad bin Rabia (Radhi za Allah ziwe juu yake) &#8211; Answaar, alirnwambia nduguye Abdur-Rahman bin Awf (Radhi za Allah ziwe juu yake);<\/p>\n<p>\u201dMie ni tajiri sana miongoni mwa Answaar. Nina furaha kugawana nawe mali yangu nusu kwa nusu. Nina wake wawili, niko tayari kumtaliki mmoja na baada ya kuisha eda yake umwoe. Lakini Abdur Rahman bin Awf hakuwa tayari kupokea chochote, si mali wala nyumba. Alimshukuru nduguye na akamwambia, \u201dTafadhali nielekeze sokoni ili nipate kuchuma kwa mikono yangu.\u201d Alifanikiwa katika shughuli zake na akaweza kuoa baada ya muda mfupi.<\/p>\n<p>Akafululiza kutoka wakati wa asubuhi kwa kipindi kirefu na siku moja akaja akiwa na alama ya umanjano; Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) akamuuliza, \u2018Ni lipi lililokuzukia?.&#8217; Akajibu, \u2019Nimeoa.\u2019 Akamuuliza, Ni kiasi gani umempa mke?.\u2019 Akajibu, \u2019Kipande cha dhahabu (mfano wa Kokwa la tende). (3)<\/p>\n<p>Imepokewa kutoka kwa\u2018 Abu Huraira (Radhi za Allah ziwe juu yake) kuwa amesemh; \u201dAnswar walimwambia Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) agawe kati yao na Muhajirina mitende, sawa kwa sawa, Mlume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) aliona wasitoe, hivyo akawaambia Muhajirina wafanye kazi kalika mashamba ya mitende na Ansaar, na wagawane mavuno sawa kwa sawa. Wakasema, \u201dTumesikia na tumetii\u00a0 (4)<br \/>\nKitendo hiki kinatufahamisha jinsi Answari walivyokuwa na moyo wa ukarimu kwa ndugu zao Muhajirina na kuwa tayari kutoa wanavyovipenda kwa ajili ya ndugu zao katika Answari walitoa kipaumbele katika mambo yote yaliyo muhimu katika kuhakikisha kuwa Muhajirina hawapati shida isiyo ya lazima. Muhajirina kwa upande wao waliushukuru, waliuthamini na kuuheshimu ukarimu huu wa kweli kutoka<br \/>\nkwa ndugu zao. Walichukua kile kilichowatosha tu kuishi maisha ya kawaida.<br \/>\nKwa ufupi ni kuwa sera hii ya udugu wa kipekee wa kisiasa ilijengwa kwenye misingi ya hekima kubwa<br \/>\niliyosababisha kuleta uuumubuzi wa kiajabu wa matatizo yaliyokuwa yakiwakabili Waislamu.<\/p>\n<div>\n<hr \/>\n<\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">1) Fiqhi Siim, Uk. 140-141..<\/span><\/em><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">2) Sahihil Bukhari, Juzuu 1, Uk. 553.<\/span><\/em><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">3) Sahihil Bukhari, Juzuu 1, Uk. 312<\/span><\/em><\/div>\n<div>\n<hr \/>\n<\/div>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM Kama ambavyo Mtume (\ufdfa) alivyosimama kwa ajili ya ujenzi wa msikiti, makao makuu ya kukutanika Waislamu na kuzoeana kwa siku mara tano, pia alisimamia kazi nyingine. Miongoni mwa mambo bora ambayo yamepokelewa na historia ni kazi ya kuunganisha udugu kati ya Muhajirina kutoka Makka na ndugu zao Maansar pale Madina. Ibn Qayyim alisema; [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":15476,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[57],"tags":[],"class_list":["post-25097","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-sera-ya-mtume"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/25097","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=25097"}],"version-history":[{"count":8,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/25097\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":25112,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/25097\/revisions\/25112"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/15476"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=25097"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=25097"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=25097"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}