{"id":22536,"date":"2023-11-30T12:29:47","date_gmt":"2023-11-30T12:29:47","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=22536"},"modified":"2023-12-07T11:01:29","modified_gmt":"2023-12-07T11:01:29","slug":"kuingia-madina","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/kuingia-madina\/","title":{"rendered":"KUINGIA MADINA"},"content":{"rendered":"<hr \/>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"font-size: 18pt; color: #ff6600;\">AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM<\/span><\/p>\n<hr \/>\n<p>Baada ya Sala ya Ijumaa, Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) aliingia Madina, na kutokea siku hiyo ukaitwa mji wa Yathrib, kuwa ni mji wa Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>). Unatamkwa kwa jina la Madina kwa kufupisha; Ilikuwa ni siku ya kihistoria iliyo nzuri kwani majumba na njia zilijaa kishindo kwa sauti za Kumsifu Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) na Kumtakasa. Mabinti wa Ki-Answar waliimba beti zifuatazo kwa furaha na shangwe<\/p>\n<p style=\"text-align: center;\">\u0637\u0644\u0639 \u0627\u0644\u0640\u0628\u062f\u0631 \u0639\u0644\u064a\u0640\u0646\u0627\u00a0 \u00a0 \u00a0\u0645\u0640\u0646 \u062b\u0646\u064a\u0640\u0627\u062a \u0627\u0644\u0648\u062f\u0627\u0639<\/p>\n<p style=\"text-align: center;\">\u0648\u062c\u0628 \u0627\u0644\u0634\u0643\u0640\u0631 \u0639\u0644\u064a\u0640\u0646\u0627\u00a0 \u00a0 \u00a0 \u00a0\u0645\u0640\u0627 \u062f\u0639\u0640\u0640\u0640\u0640\u0627 \u0644\u0644\u0647 \u062f\u0627\u0639<\/p>\n<p style=\"text-align: center;\">\u0623\u064a\u0647\u0627 \u0627\u0644\u0645\u0628\u0639\u0648\u062b \u0641\u064a\u0646\u0627\u00a0 \u00a0 \u062c\u0626\u062a \u0628\u0627\u0644\u0623\u0645\u0631 \u0627\u0644\u0645\u0637\u0640\u0627\u0639<\/p>\n<p>\u00a0\u201d llmeangaza mwezi kwetu, kutoka katika lango la maagano<\/p>\n<p>Ni wajibu wetu kushukuru (kwa neema hiya), kwa kuwa tuna mlinganiaji, kwa Mwenyezi Mungu mwenye kulingania,\u00a0 \u00a0Ewe ulieletwa kwetu\u00a0 Umekuja na jambo lenye kufuatwa.\u201d<\/p>\n<p>Answar hawakuwa watu wenye utajiri mkubwa, pamoja na hali hiyo kila mmoja wao alikuwa anatamani Mtume (\ufdfa) ku\ufb01kia kwake. Ikawa Mtume (\ufdfa) hapiti katika nyumba yoyote katika nymnba za Answar isipokuwa walikamata hatamu ya ngamia wake, Wakisema; <em>\u201dNjoo fikia kwetu tuko tayari kukupokea kwani idadi yetu ni kubwa, tuna silaha na tuna uwezo wa kukulinda.&#8221;<\/em><\/p>\n<p>Mtume (\ufdfa) akawa akiwaambia, <span style=\"color: #008000;\">\u201dIachieni njia yake kwani ngamia huyo ameamrishwa\u201d,<\/span> Ngamia hakusita alienda mpaka alipofika mahali ambapo ndipo ulipo Msikiti wa Mtume (\ufdfa) hivi leo, akapiga magoti. Mfume (\ufdfa) hakushuka kutoka juu ya ngamia huyo mpaka aliposimama tena na kwenda kidogo, kisha akageuka kidogo na kurejea na kupiga magoti mahali pale pa kwanza, akashuka. Hapo palikuwa ni kwa <span style=\"color: #ff6600;\">Banu Najjar,<\/span> wajomba zake Mtume (\ufdfa). Ilikuwa ni katika uwezesho wa Mwenyezi Mungu (\ufdfb) kwa ngamia huyo kufanya alivyofanya. Kwani Mwenyezi Mungu (\ufdfb) alipenda Mtume (\ufdfa) a\ufb01kie kwa wajomba zake Akikusudia Kuwakirimu kwa kitendo hicho.<\/p>\n<p>Watu wengi walijitokeza na kumuomba Mtumbe wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa) ashukie kwao. Lakini ni <span style=\"color: #ff6600;\">Abu Ayub Al-Answar<\/span> ndiye aliyechukua mizigo yake na kuiingiza nymnbani mwake. Mtume wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa) akawa anasema; &#8220;Mtu anakuwa na mizigo yake (usiichukue).&#8221; <span style=\"color: #ff6600;\">As\u2019ad bin Zurarah<\/span> akaja akachukua hatamu ya mnyama wake na akafikia kwake,<\/p>\n<p>Katika upokezi wa <span style=\"color: #ff6600;\">Anas<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) kutoka kwa Bukhari, inasemwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa) alihoji; <span style=\"color: #008000;\">\u201dNi nyumba gani katika nyumba za watu wetu iliyo karibu sana?.&#8221;<\/span> Abu Ayub akasema; &#8220;Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa) hii ni nyumba yangu, na huu ni mlango wangu\u201d, Mtume (\ufdfa) akasema, <span style=\"color: #008000;\">\u201dTwende ukatuandalie mapumziko.\u201d<\/span> Mtume (\ufdfa) akasema (kumwambia ngamia), <span style=\"color: #008000;\">\u201dSimama kwa baraka za M wenyezi Mungu.<\/span> &#8221; (1)<\/p>\n<p>Baada ya siku chache mke wake <span style=\"color: #ff6600;\">Sauda<\/span> na mabin\ufb01 zake wawili, <span style=\"color: #ff6600;\">Fatma na Ummu_Kulthum,<\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">na Usama bin Zaidi<\/span> na<span style=\"color: #ff6600;\"> Ummu Ayman<\/span> walifika Madina. Pamoja nao katika safari hiyo alikuwa <span style=\"color: #ff6600;\">Abdullah bin Abubakar<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake), familia ya <span style=\"color: #ff6600;\">Abubakar<\/span> pamoja na<span style=\"color: #ff6600;\"> Aisha<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake). Aliyebaki miongoni mwao alikuwa ni Bi<span style=\"color: #ff6600;\"> Zainab<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake), alibaki kwa Abu Al-Assi, hakuweza kutoka mpaka alipohama baada ya vita vya Badri. (2)<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">Aisha<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) ainesema, &#8220;Mtume wa Mwenyezi Mmmgu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) alipofika \u2019Madina, masahaba wake, <span style=\"color: #ff6600;\">Abubakar<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) na Bilal (Radhi za Allah ziwe juu yake) walipatwa na maradhi nikaenda nyumbani mwao na kuwasalimia; &#8220;U hali gani baba yangu, na unajisikiaje ewe Bilal\u201d; Aisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) anasema Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) akajibu, <em>\u201dKila mtu ni mwenye kupambazukiwa akiwa kati- ya watu wake, na hali ya kuwa kifo ki karibu sana kuliko kamba ya kiatu chake.\u201d<\/em> (haya maneno alikuwa akipenda kuyatamka Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) wakati akiwa na homa).<\/p>\n<p>Ilikuwa ni kawaida ya Bilal (Radhi za Allah ziwe juu yake) anapoumwa na homa kunyanyua sauti yake na akisema, &#8220;Eee, Allah natamani kujuwa ikiwa nitalala usiku mmoja katika jangwa na hali ya kuwa pembeni mwangu kuna mti uitwao Idhkhir, na mti uitwao Jalili, na Ie, iko siku nitayaendea maji ya soko liitwalo Mijamma, na Je, nitapata bahati ya kuyaona majabali yaitwayo Shama na Tufail &#8211; ya Makka?<\/p>\n<p>Aisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema; &#8220;Nikamwendea Mtume wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa) na kumuelezea khabari hiyo\u201d; Akaomba; &#8220;Ewe Mala Wangu wa Haki, tufanye tuipende Madina kama tunavyoipenda Makka au zaidi yake, na ifanye Madina kuwa ni mahali pa kupata afya njema, na tia baraka katika pishi yake na kibaba chake na ihamishe homa yake ipeleke huko Juhfa. &#8221; (3)<\/p>\n<p>(Mpaka hapa imekomea sehemu,moja ya maisha ya Mtume (\ufdfa) na kukamilika kwa awamu ya da&#8217;awa ya Kiislamu ya Makka.)<\/p>\n<div>\n<hr \/>\n<\/div>\n<div><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>1)\u00a0 Sahihil Bukhari, Juzuu 1, Uk. 556.\u00a0<\/em><\/span><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">2) Zaad Ma\u2019ad, Juzuu 2, Uk. 55.\u00a0<\/span><\/em><\/div>\n<div><em><em><span style=\"color: #ff6600;\">3) sahihi Bukhari, Iuzuu 1, Uk. sss-589<\/span><\/em><\/em><\/p>\n<hr \/>\n<\/div>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM Baada ya Sala ya Ijumaa, Mtume (\ufdfa) aliingia Madina, na kutokea siku hiyo ukaitwa mji wa Yathrib, kuwa ni mji wa Mtume (\ufdfa). Unatamkwa kwa jina la Madina kwa kufupisha; Ilikuwa ni siku ya kihistoria iliyo nzuri kwani majumba na njia zilijaa kishindo kwa sauti za Kumsifu Mwenyezi Mungu (\ufdfa) na Kumtakasa. Mabinti [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":15476,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[57],"tags":[],"class_list":["post-22536","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-sera-ya-mtume"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/22536","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=22536"}],"version-history":[{"count":11,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/22536\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":22614,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/22536\/revisions\/22614"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/15476"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=22536"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=22536"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=22536"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}