{"id":22532,"date":"2023-11-30T11:20:56","date_gmt":"2023-11-30T11:20:56","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=22532"},"modified":"2023-11-30T11:22:49","modified_gmt":"2023-11-30T11:22:49","slug":"kufika-kwao-qubaa","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/kufika-kwao-qubaa\/","title":{"rendered":"KUFIKA KWAO QUBAA"},"content":{"rendered":"<hr \/>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"font-size: 18pt; color: #ff6600;\">AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM<\/span><\/p>\n<hr \/>\n<p>Mnamo siku ya Jumatatu tarehe nane mwezi wa Rabiul Awwal, mwaka wa 14 wa Utume nao ni mwaka wa kwanza wa Hijra sawa na 3\/9\/ 622 C.E., Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa) aliwasili Quba. (1)<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">Urwah bin Al-Zubair<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yao) alisema, &#8220;Waislamu wa Madina walisikia kuhama kwa Mtume (\ufdfa) kutoka Makka, wakawa wanatoka kila asubuhi kwenda katika ardhi yenye mawe meusi kumngojea mpaka linawarudisha joto la mchana majumbani kwao. Siku moja baada ya kungoja kwa muda mrefu walipoingia majumbani mwao, alipanda mtu mmoja Myahudi juu ya majabali kwa shughuli zake binafsi, akamwuona Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa) na Masahaba wake (Radhi za Allah ziwe juu yao), wakiwa na mavazi meupe. Myahudi hakuweza kusubiri na akasema kwa sauti yake ya juu: <em>\u201dEnyi Waarabu babu yenu ambaye mnayemngojea, huyo anakuja.\u201d<\/em> Waislamu walisimama na kwenda kuchukuwa silaha zao (2)<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">Ibn Qayyim<\/span> amesema, \u201dKikasika kishindo cha Takbir kwa Banu Amri bin Aufi, na wakatoa Takbira Waislamu wengine kwa sababu ya furaha ya kuwasili kwake. Wakatoka kwenda kumpokea, wakamwamkia maamkizi ya &#8216; Utume, wakamzunguka pembezoni mwake, kwa utulivu na wakati huo wahyi unashuka,<\/p>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">\u0641\u064e\u0625\u0650\u0646\u0651\u064e \u0627\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u064e \u0647\u064f\u0648\u064e \u0645\u064e\u0648\u0652\u0644\u064e\u0627\u0647\u064f \u0648\u064e\u062c\u0650\u0628\u0652\u0631\u0650\u064a\u0644\u064f \u0648\u064e\u0635\u064e\u0627\u0644\u0650\u062d\u064f \u0627\u0644\u0652\u0645\u064f\u0624\u0652\u0645\u0650\u0646\u0650\u064a\u0646\u064e \u06d6 \u0648\u064e\u0627\u0644\u0652\u0645\u064e\u0644\u064e\u0627\u0626\u0650\u0643\u064e\u0629\u064f \u0628\u064e\u0639\u0652\u062f\u064e \u0630\u064e\u0670\u0644\u0650\u0643\u064e \u0638\u064e\u0647\u0650\u064a\u0631\u064c<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\"><em>[..Kwam&#8217; Mwenyezi Mungu ni kipenzi chake, na Jibril na Waislamu wema wote; na zaidi ya hayo Malaika pia watasaidia ] [66:4]<\/em> <\/span><\/p>\n<p>Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yao) alisimama kwa ajili ya watu na wakati huo Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) alikuwa amekaa, ikawa kila Answari ambaye -alikuwa bado hajawahi kumwuona Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) alikuja na kumuamkia. (Na katika mapokezi mengine) Jua lilipompata Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>), Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yao) akaja na akamfunika kwa shuka yake, wakati huo ndio watu wakamjua Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>). (3)<\/p>\n<p>Waislamu wa Madina walitoka kwa wingi kwenda kumpokea. Katika historia ya Madina hakujawahi kutokea siku ya furaha iliyowahi kushuhudiwa kama siku hiyo: Kwa hakika Mayahudi waliuona ukweli wa utabiri wa Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) kutoka kwa Nabii Habakuki, <em>\u201dKwa hakika Mwenyezi Mungu amekuja kutoka Tayman, na Kudusi kutoka milima ya Parani.<\/em> (4)<\/p>\n<p>Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) alipo\ufb01ka Quba ali\ufb01kia kwa<span style=\"color: #ff6600;\"> Kulthum bint Hadim<\/span> na wengine wanasema kwa <span style=\"color: #ff6600;\">Sa&#8217;ad bin Khaitham<\/span>, kauli ya kwanza ndiyo iliyo na nguvu zaidi.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">Ali bin Abu Twalib<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yao) alikaa Makka kwa muda wa siku tatu, mpaka alipomaliza majukumu aliyopewa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) ya kurudisha amana za watu zilizokuwa kwake. Baada ya hapo naye akahama akisafiri kwa miguu, akaungana nao wakiwa Quba, na akafikia kwa <span style=\"color: #ff6600;\">Kulthum bint Hadim<\/span>. Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) alikaa Quba kwa muda wa siku nne, Jumatatu, Jumanne, Jumatano na Al khamisi, (5) na kuasisi Msikiti wa Quba na akasali ndani yake. Huo ndio Msikiti wa kwanza uliojengwa kwa ajili ya kumcha Mwenyezi Mungu <span style=\"color: #008000;\">(\ufdfb)<\/span> baada ya Utume. Ilipofika siku ya tano-Ijumaa-aliondoka kwa amri ya Mwenyezi Mungu (\ufdfb), Abubakar akiwa nyuma yake, wakati huo amekwishapeleka ujumbe kwa <span style=\"color: #ff6600;\">Banu Najjari,<\/span> wajomba zake, nao wakamuitika wakaja wakiwa wamezivaa panga zao. Wakaelekea upande wa Madina. Ijmnaa ikamkuta kwa <span style=\"color: #ff6600;\">Banu Saalim bin Aufi,<\/span> akasali nao katika Msikiti ambao ulikuwa jangwani, na walikuwa kiasi cha watu mia moja.<\/p>\n<div>\n<hr \/>\n<\/div>\n<div><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>1)\u00a0 <span style=\"color: #000000;\">Rahmatun Lil &#8216;Alamin, Iuzuu 1, Uk. 102. Siku hii ndio aliyotimiza Mtume (s.a.w) miaka hamsini na tatu, na hivyo kutimiza miaka kumi na tatu ya Utume wake. Kuna wenye kusema kuwa alipewa Utume tarehe 9, Rabbiul Awwal, mwaka wa 41 katika mwaka wa Tembo. Kwa wanaosema alipewa Utume katika Rumadhan ya mwaka wa 41 wa mwaka wa Tembo, katika siku hiyo inatimia miaka 12, miezi 5, na siku 18 au 22. 315<\/span>\u00a0<\/em><\/span><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">2) Sahihil Bukhari, Iuzuu 1, Uk. 555&#8230;<\/span><\/em><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">3) Sahihil Bukhari, Juzuu 1, Uk. 555<\/span><\/em><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">4) Habakuki: 3:3.<\/span><\/em><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">5) <span style=\"color: #000000;\">Zaadil Mu&#8217;ad, Iuzuu 2, Uk. 54. Ibn Hisham, juzuu 1, Uk.\u2018 493. Rahmatun Lil &#8216;AIamin, Iuzuu 1, Uk. 102. 31\u00b0 Imepokewa na Ibn Isha-q. Ibn Hisham, Juzuu 1, Uk. 494. Na hili ndilo alilolichagua mwanazuoni Mansourpuri (Angalia, Rahmatun Lil \u2018Alamin, Iuzuu 1, Uk. 102). Katika Sahihil Bukhari alikaa Qubaa siku ishirini na nne (Iuzuu 1, Uk. 61). Vile vile, siku kumi (Bukhari, Juzuu 1, Uk. 555), siku kumi na nne (Bukhari, Iuzuu 1, Uk. S60). I-Iili la mwisho ndilo alilolichagua Ibn Qayyim, na kusema kuwa siku Mtume aliposhukia Quba ilikuwa ni Iumatatu na aliondoka siku ya Ijumaa (Zaad Ma\u2019ad, juzuu 2, \u2018Uk. 54-55). Cha muhimu, ni kuwa tofauti ya masiku haizidi siku kumi. Kuondoa siku ya ku\ufb01ka na kuondoka, haizidi siku kumi na mbili ikiwa ni katika wiki mbili. <\/span><\/span><\/em><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">6) Rahmatun Lil &#8216;Alamin, Iuzuu 1, Uk. 101.<\/span><\/em><\/div>\n<div><em><em><span style=\"color: #ff6600;\">7) <\/span><\/em><span style=\"font-size: revert; color: #ff6600;\">Sahihil Bukhari, Iuzuu 1, Uk. 554. 306<\/span><\/em><\/div>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM Mnamo siku ya Jumatatu tarehe nane mwezi wa Rabiul Awwal, mwaka wa 14 wa Utume nao ni mwaka wa kwanza wa Hijra sawa na 3\/9\/ 622 C.E., Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa) aliwasili Quba. (1) Urwah bin Al-Zubair (Radhi za Allah ziwe juu yao) alisema, &#8220;Waislamu wa Madina walisikia kuhama kwa Mtume (\ufdfa) [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":15476,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[57],"tags":[],"class_list":["post-22532","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-sera-ya-mtume"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/22532","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=22532"}],"version-history":[{"count":3,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/22532\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":22535,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/22532\/revisions\/22535"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/15476"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=22532"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=22532"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=22532"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}