{"id":21935,"date":"2023-08-24T12:59:01","date_gmt":"2023-08-24T12:59:01","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=21935"},"modified":"2023-11-30T10:02:44","modified_gmt":"2023-11-30T10:02:44","slug":"njiani-kuelekea-madina","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/njiani-kuelekea-madina\/","title":{"rendered":"NJIANI KUELEKEA MADINA"},"content":{"rendered":"<hr \/>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"font-size: 18pt; color: #ff6600;\">AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM<\/span><\/p>\n<hr \/>\n<p>Kazi ya kuwatafuta (Mtume (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) na rafiki yake) ilisimama baada ya kuendelea kwa muda wa siku tatu pasina mafaniko yoyote. Mtume wa Mwenyezi Mungu na rafiki yake walijiandaa kutoka na kueleka Madina. Walikuwa wamemkodi <span style=\"color: #ff6600;\">Abdillah bin Urayqit Al-Laythy<\/span> ambaye aljkuwa ni mwongozaji hodari wa njia. Alikuwa kafiri lakini walimwamini kwa hilo, walimkabidhi wanyama wao na walikuwa wameahidiana kukutana naye katika pango la Jabal Thaur, baada ya siku tatu. Akiwa na wanyama wao usiku wa Jumatatu \u2013 mwaka wa kwanza A.H \u2013 sawa na mwezi wa 9 mwaka 622 C.E. alikuja <span style=\"color: #ff6600;\">Abdullah bin Urayqiti<\/span> na wanyama wawili. Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) alisema kumwambia Mtume (s.a.w), \u2019Ninakukomboa kwa baba yangu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>), chukua mmoja miongoni mwa wanyama wangu\u2019, na akamsogezea aliyekuwa bora zaidi katika wao, Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) akasema; \u201dNakubali lakini kwa malipo.\u201d<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">Asmaa binti Abubakar<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) aliwapelekea chakula na akasahau kukiwekea kamba chombo chenye Chakula hicho. Walipoondoka \u2018 aliamua kukitundika chombo hicho lakini hapakuwa na kamba ya\u2018 kufungia. Alichana ukanda wake sehemu mbili, akakitundika chombo kile, na hii ndio sababu ya kuitwa mwenye mikanda miwili. (1)<\/p>\n<p>Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) na Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) wakasa\ufb01ri pamoja na <span style=\"color: #ff6600;\">\u2018Amir bin Fihr<\/span> pamoja na yule mwelekezaji<span style=\"color: #ff6600;\"> Abdullah bin Urayqti,<\/span> kwa njia ya ufukweni. Baada ya kutoka pangoni tu walielekea Kusini upande wa Y\u00e9m\u00e9n, kisha wakageuza na kuelekea Magharibi upande wa ufukweni, mpaka wakafika kwenye njia ambayo \u201cwatu hawajaizoea, wakaelekea upande wa Kaskazini karibu\u2019 na Pwani ya Bahari Nyekundu. Njia hizi hazikuwa zinatumiwa na mtu yeyote isipokuwa kwa nadra sana.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">Ibn Ishaq<\/span> ametaja njia alizopita Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>); alisema: \u2019-\u2019Alipotoka nao muelekezaji, alipita pamoja nao njia ya chini ya Makka, kisha akaenda nao njia ya Pwani mpaka akaikingamia njia ya chini ya Usfana, kisha akapita nao sehemu ya chini ya mji akavuka nao mpaka akaikingamia njia ya kuvuka Qudaid. Baada ya hapo akavuka nao kutoka mahali hapo, akaenda nao Al-Kharar, \u2018halafu akaenda nao Thaniyyat Al-Murra, kisha akaenda nao Laqfa, kutoka hapo akavuka nao Midlajat Laqfa, halafu akazama nao Midlajat Mujaj. Alipotoka hapo akaenda nao Marjah Majaji, halafu Marjah Akanidi, halafu Dhikashiri, ikifuatiwa na Jadaajidi, kisha Ajrad, halafu akaenda nao mpaka Dhaa Salam ka\ufb01ka bonde la Aadai Midlaja Taahin. Halafu akavuka nao Al- Ababid, na tena akavuka nao Al-Faja, kisha akaenda naq Thaniyyati Athir, \u2013 kuliani kwa Rakouba mpaka akafika nao Katika bonde la Riim, na baadaye Quba. (2)<\/p>\n<p><span style=\"color: #993300;\"><strong>Yafuatayo ni baadhi ya mambo yaliyotokea njiani:-<\/strong> <\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #993300;\"><strong>1.<\/strong><\/span> Bukhari amepokea kutoka kwa Abubakar Swiddiq (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: <em>\u201dTulikwenda usiku mzima na siku iliyofuata mpaka mchana wa jua kali sana, njia ilikuwa Tupu hapiti mtu yeyote, jiwe refu lenye kivuli ambalo halikupatwa na jua, likanyanyuliwa na tukajihifadhi katika kivuli chake. Nikamtengenezea Mtume (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) mahali kwa mikono yangu na nikamkunjulia ngozi ili alale hapa; Nikamwambia, \u201d Lala upumzike ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) na nitakuondolea vilivyo pembezoni mwako\u201d, Akalala. Nikatoka nikamuondolea vilivyo pembezoni mwake, gha\ufb02a katika kuzunguka kwangu nikakutana uso kwa uso namchungaji wa mbuzi akiwa anakuja na mbuzi wake kwenye lile jiwe. Akitoka kwenye jiwe mfano wa lile alipokuwa amelala Mtume (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) nikamwuuliza: \u201dWewe ni mtumishi wa nani? Akasema, \u201cWa mtu mmoja katika watu wa Madina au Makka\u201d, nikasema tena: \u201dJe katika mbuzi wako yupo anayetoa maziwa?\u201d Akasema, \u201dNdiyo\u201d, nikasema: \u201dJe unakamua?\u201d Akajibu, \u201dNdiyo\u201d, akamkamata mbuzi, nikamwambia, \u201dKasa\ufb01she kiwele kwa kuondoa mchanga, manyoya na uchafu\u201d, kisha akakamua katika chuchu yenye maziwa machache ndani ya chombo nilichokuwa nacho kwa ajili ya matumizi ya Mtume (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) ya kunywea maji na kutawadhia. Nilimwendea Mtume (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) nikiwa na maziwa yale lakini nikaona vibaya kumwamsha, basi niliketi karibu nae mpaka alipoamka nikayamimina maji katika chomba chenye maziwa, mpaka ikapoa sehemu yake ya\u2019 chini, nikasema, \u201dKunywa ewe Mtumbe wa Mwenyezi Mungu\u201d, akanywa mpaka nikaridhika kuwa ametosheka, kisha akasema, \u201cHivi bado hauja\ufb01ka wakati wa safari? Nikamjibu, \u201cNaon: ume\ufb01ka.\u201d Akasema, \u201dBasi na twende zetu.\u201d<\/em> (3)<\/p>\n<p><span style=\"color: #993300;\">2.<\/span> Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) alikuwa na sifa ya kuwa ni mzee maarufu anayejulikana, na Mtume (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) alikuwa Kijana asiyejulikana, kwa sababu hiyo kila aliyekutana nao njiani alimwuliza Abubakar: \u201cNi nani huyu mtu ambaye yuko mbele yako?.\u201d Naye alikuwa akijibu kwa kusema: \u201dHuyu ni mtu anaeniongoza njia.\u201d Wakadhani kuwa anakusudia njia ya kawaida, lakini alikuwa anakusudia njia ya Akhera.<\/p>\n<p><strong><span style=\"color: #993300;\">3.<\/span><\/strong> <span style=\"color: #ff6600;\">Suraqa bin Maliki<\/span> aliwafuata. Suraqa bin Maliki alisema: \u201dWakati nikiwa nimekaa katika Baraza moja la jamaa zangu Banu Mudliji, alikuja mtu miongoni mwetu akatusalimia hali ya kuwa sisi tumekaa na kisha akasema; \u201dEwe Suraqa nimeona kundi la watu wakipita kule ufukweni punde tu, bila shaka ni Muhammad na Masahaba zake.\u201d Akasema Suraqa, nikajua kuwa hao ni wao, lakini nikamwambia kwa hakika hao sio wao, lakini umewaona fulani na fulani ambao wameondoka huku tukiwaona, baada ya kusema hivyo akaendelea kukaa katika lile baraza kwa muda wa saa moja zaidi na baada ya hapo, \u201cNikasimama na kuingia ndani na kumuamrisha mjakazi wangu aniletee farasi wangu ambaye yuko nyuma ya kichuguu ili amfunge na amuandae, wakati nikijitayarisha. Baada ya hapo nikauchukua mkuki wangu, nikatoka nao nje ya nyumba na nikaichora ardhi kwa kile chmna chake, nikainamisha sehemu yake ya juu na kisha nikamwendea farasi wangu, nikampanda, nikijua kuwa ataniwezesha kuwafikia, njiani farasi wangu alijikwaa na nikaanguka kutoka juu yake, nikasimama, nikaupeleka mkono wangu kwenye ziaka (mfuko wa kuwekea mishale) langu nikatoa vibua vya kutazamia bahati (kupigia ramli), nikatazama kwavyo bahati kwa kuviuliza, \u201dJe, niwadhuru au La?.\u201d Kikatoka kile ambacho ninakichukia (kilichosema usiwadhuru). Nikampanda farasi wangu tena na. kuviasi vibua.<\/p>\n<p>Farasi akaendelea kunisogeza mpaka nika\ufb01ka karibu kiasi cha kusikia kisomo cha Mtume wa Mwenyezi Mungu, hali ya kuwa hageuki nyuma. Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) ndiye aliyekuwa akigeuka mara kwa mara. Gha\ufb02a miguu ya mbele ya farasi wangu ilizama katika Ardhi mpaka magotini, nikaanguka tena kutoka katika mgongo wa farasi wangu, nikamkemea akasimama lakini kidogo ashindwe kuitoa miguu yake ya mbele mahala ilipozama. Niligundua kuwa miguu yake imeathirika vibaya, tahamaki likatoka vumbi lililozagaa sehemu kubwa mfano wa moshi mzito, nikataka kujua bahati kwa vibua, kikatoka kile ambacho ninakichukia, nikalazimika kuwaita kwa kuwataka msamaha, wakasimama nikampanda farasi wangu mpaka nikawafikia.<\/p>\n<p>Wakati huo nina wasiwasi mkubwa jinsi farasi alivyozamishwa ardhini kuwa litadhihiri jambo la Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) , nikamwambia; \u201cKwa hakika jamaa zako wameweka zawadi kwa atakayekuuwa, na nikawaeleza khabari za mambo ambayo watu wamedhamiria kuwafanyia, na nikawataka wajiandae vizuri, hawakuniomba chochote isipokuwa waliniambia; \u201cUitunze siri hii.\u201d Nikamuomba aniandikie maandishi ya amani. Alimuamrisha \u2018Amir bin Fahairah naye katika karatasi ya ngozi, kisha Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) akaendelea na safari yake.3\u00b0\u201c<\/p>\n<p>Katika mapokezi mengine kutoka kwa\u2019 Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema, \u201dTulisa\ufb01ri na hali ya kuwa watu wanatutafuta,<span style=\"color: #ff6600;\"> Suraqa bin Maliki bin Jaatham<\/span> alitukia akiwa juu ya farasi wake, nikasema, \u201cEwe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hawa watafutaji wamekwisha tu\ufb01kia,\u00a0 yeye akanijibu,<\/p>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">\u201c\u0644\u0627 \u062a\u062d\u0632\u0646 \u0625\u0646 \u0627\u0644\u0644\u0647 \u0645\u0639\u0646\u0627\u201d<\/span><\/p>\n<p><em><span style=\"color: #0000ff;\">\u201cUsihuzunike hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi.\u201d<\/span><\/em>\u00a0 3\u00b09<\/p>\n<p>Akarejea Suraqa, aliwakuta watu bado wamo katika kuwatafuta, akasema, \u201dKwa hakika nimekwisha kuwatafulieni khabari zilizo sahihi, bila shaka mmetoshwa na mambo yaliyopo hapa, mchana aliwatafuta kwa juhudi, na mwisho wake akawa mlinzi wao\u201d\u00a0 31\u00b0<\/p>\n<p><strong><span style=\"color: #993300;\">4.<\/span><\/strong> Katika safari yake Mtume (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) alipita kwenye mahema mawili ya <span style=\"color: #ff6600;\">Ummu Maabadi Al-Khuzaiyyah.<\/span> Alikuwa mwanamke aliyewashinda wenzake kwa ubora na ushujaa. Mwanamke huyo alijifunika kwa nguo yake akiwa uwanjani mwa hema, akiwalisha na kuwanywesha watu waliompitia, walimwuuliza kama alikuwa na kitu chochote cha kula?. Akajibu: \u201cNaapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu lau kingekuwapo na kitua chochote kusingekuwa na matatizo kwenu kupewa takrima ya ugeni. Kwani wanyama hawana malisho, mwaka huu ni mwaka wa ukame.\u201d Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) akamuona mbuzi aliye pembezoni mwa hema akasema: <em><span style=\"color: #0000ff;\">\u201dNi mbuzi gani huyu ewe Ummu Maabadi?\u2019<\/span><\/em> Akasema: \u201cHuyu ni mbuzi amebaki nyumbani kwa sababu ya maradhi hakuweza kutoka na mbuzi wengine.\u201d Akasema, <span style=\"color: #0000ff;\">\u201d ]e ana maziwa?\u201d<\/span> Akasema: \u201dYeye ana maradhi makubwa hawezi kuwa na maziwa.\u201d Akasema: <em><span style=\"color: #0000ff;\">\u201dJe unaniruhusu nimkamue?\u2019<\/span><\/em> Akasema: \u201dNdiyo, ninakukomboa kwa baba yangu na mama yangu, kama unaona anatoa maziwa basi mkamue.\u201d Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) akapangusa kwa mkono wake kiwele chake na akamtaja Mwenyezi Mungu na akaomba, kikajaa Kiwele chake na kikatowa maziwa, akataka apelekewe chombo chake kikubwa cha kuwatosha watu wengi, akakamulia ndani yake mpaka povu likakaa juu. Akamnywesha mpaka alipotosheka na akawanywesha Masahaba zake mpaka wakatosheka, na yeye akanywa mwisho. Baada ya hapo akakamua kwa mara ya pili na kukijaza chombo, akamuachia<span style=\"color: #ff6600;\"> Ummu Maabadi<\/span> na wakaendelea na safari yao.<\/p>\n<p>Haukupita muda mrefu mume wake Abu Maabadi akarejea kutoka machungani, hali\u2019 ya kuwa anawachunga mbuzi wakondefu wanayumba kutokana na ukondefu, alipoyaona maziwa alistaajabu sana! kwani mbuzi hawakupata majani. Na hapana mbuzi anayefaa kwa kukamuliwa nyumbani. Mke wake akasema: \u2019Ninaapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu, kapita mtu mwenye kubarikiwa khabari zake hivi na hivi na katika hali yake hivi na hivi \u2013 hakika mimi ninamwuona kuwa huyu ndiye yule bwana anaetafutwa na Makuraishi\u201d, naye akasema: \u201dNisi\ufb01e mtu huyo alivyo ewe Ummu Maabadi.\u201d Akamsifu kwa sifa zake ambazo ni nzuri zenye kuvutia kwa maneno yenye kuvutia kana kwamba mwenye kusikia anamwuona na yuko mbele yake. Abu Maabadi akasema: \u201dNaapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu huyu ni swahibu wa Makuraishi ambaye wanazungumzia khabari zake, kwa hakika ninakusudia kufuatana naye, na kwa hakika nitafanya hivyo iwapo upo uwezekano huo.\u201d<\/p>\n<p>Ikatokea sauti katika mji wa Makka watu wanaisikia na hawaoni msemaji. Sauti hiyo ikiomba:<\/p>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">\u062c\u0632\u0649 \u0627\u0644\u0644\u0647 \u0631\u0628 \u0627\u0644\u0639\u0631\u0634 \u062e\u064a\u0631 \u062c\u0632\u0627\u0626\u0647 *** \u0631\u0641\u064a\u0642\u064a\u0646 \u062d\u064e\u0644\u0627\u0651\u064e \u062e\u064a\u0645\u0640\u0640\u062a\u064a \u0623\u0645 \u0645\u064e\u0639\u0652\u0628\u064e\u0640\u0640\u062f\u0650<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #008000;\">\u0647\u0640\u0645\u0640\u0627 \u0646\u0632\u0644\u0627 \u0628\u0627\u0644\u0628\u0650\u0640\u0640\u0640\u0631\u0651\u0650 \u0648\u0627\u0631\u062a\u062d\u0644\u0627 \u0628\u0647 *** \u0648\u0623\u0641\u0644\u062d \u0645\u0646 \u0623\u0645\u0633\u0649 \u0631\u0641\u064a\u0642 \u0645\u062d\u0645\u0640\u0640\u062f<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #008000;\">\u0641\u064a\u0627 \u0644\u0642\u064f\u0635\u064e\u064a\u0651 \u0645\u0640\u0640\u0627 \u0632\u064e\u0648\u064e\u0649 \u0627\u0644\u0644\u0647 \u0639\u0646\u0643\u0640\u0640\u0645 *** \u0628\u0647 \u0645\u0646 \u0641\u0639\u0627\u0644 \u0644\u0627 \u064a\u064f\u062d\u064e\u0627\u0630\u0649 \u0648\u0633\u064f\u0640\u0640\u0624\u0652\u062f\u064f\u062f<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #008000;\">\u0644\u0650\u064a\u064e\u0647\u0652\u0646\u0650 \u0628\u0646\u064a \u0643\u0639\u0640\u0628 \u0645\u0643\u0640\u0640\u0627\u0646 \u0641\u064e\u062a\u0627\u062a\u0650\u0647\u0640\u0640\u0645 *** \u0648\u0645\u0642\u0639\u062f\u064f\u0647\u0640\u0627 \u0644\u0644\u0645\u0624\u0645\u0646\u0640\u064a\u0646 \u0628\u064e\u0645\u0652\u0631\u0635\u064e\u0640\u062f<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #008000;\">\u0633\u064e\u0644\u064f\u0648\u0627 \u0623\u062e\u062a\u0643\u0645 \u0639\u0646 \u0634\u0627\u062a\u0647\u0640\u0627 \u0648\u0625\u0646\u0627\u0626\u0647\u0640\u0627 *** \u0641\u0625\u0646\u0643\u0645 \u0625\u0646 \u062a\u0633\u0623\u0644\u0648\u0627 \u0627\u0644\u0634\u0640\u0627\u0629 \u062a\u064e\u0634\u0652\u0640\u0647\u064e\u0640\u0640\u0640\u062f<\/span><\/p>\n<p><em>\u201cNa Awalipe Mwenyezi Mungu Mola Wa Arshi ubora wa malipo yake<\/em><\/p>\n<p><em>Marafiki wawili walio\ufb01ka katika Mahema Mawili ya llmmi Maabadi;<\/em><\/p>\n<p><em>Wao wali\ufb01ka kwa wema na wamesa\ufb01ri kwa wema, Na amefuzu yule ambaye amekuwa ni ra\ufb01ki wa Muhammad. <\/em><\/p>\n<p><em>Enyi kina Qusway, yale ambayo Mwenyezi Mungu Ameyakusanya kutoka kwenu<\/em><\/p>\n<p><em>Kwa sababu yake miongoni mwa Matendo hayatalipwa na ubwana.<\/em><\/p>\n<p><em>Na iwafurahishe Banu Kaabi nafasi ya kijana wao, Na makao yao kwa Waumini kutika kuwalindilia<\/em><\/p>\n<p><em>Muulizeni dada yenu kuhusu Mbuzi wake nu chombo chake<\/em><\/p>\n<p>Kwa hakika kama nyinyi mtamuuliza Mbuzi kuhusu khabari hizo, atashuhudia.\u201d<\/p>\n<p>Asmaa (Radhi za Allah ziwe juu yake) alisema hatukujua ni wapi ameelekea Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>), gha\ufb02a alikuja mtu mmoja katika majini-, kutokea ya Makka, akaimba beti hizi na hali ya kuwa watu wanamfuata na wanamsikiei sauti yake na hawamuoni, mpaka akatoka Makka. amesema, \u201dTuliposikia kauli yake, tulielewa mahali alipo elekea Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alielekea Madina (5)<\/p>\n<p>5. Alipokuwa njiani Mtume (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) alikutana na Aba Buraida, ambaye alikuwa ni kiongozi wa jamaa zake, alitoka katika kumtafuta Mtume (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) na Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) kwa kutaraji kufanikiwa kwa kupata zawadi kubwa ambayo Makuraishi wameitangaza. Alipomkabili Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) na kuzungumza naye, alisilimu pale pale, pamoja na watu sabini katika jamaa zake. Kisha akavua kilemba chake na akakifunga katika mkuki wake, akakifanya kuwa ni bendera; bendera ambayo ilitangaza kuwa Mfalme wa amani na salama amedhihiri ili aijaze dunia uadilifu na usawa. (6).<\/p>\n<p>6. Njiani Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alikutana na Al- Zubair hali yakuwa yumo katika msafara wa Waislamu, wafanyabiashara waliokuwa wakirejea kutoka Sham, akamvalisha nguo nyeupe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) na Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake). (7)<\/p>\n<div>\n<hr \/>\n<\/div>\n<div><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>1) \u00a0Sahihil Bukhari, Juzuu 1, Uk. 533, 555. Ibn Hisham, Iuzuu 1, Uk. 486.<\/em><\/span><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">2) Ibn Hisham, Juzuu 1, Uk. 491,492.<\/span><\/em><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">3) Ibid. luzuu 1, Uk 554. Zilad Mll\u2019ad, Iuzuu 2<\/span><\/em><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">4) Sahihul Bukhari, Iuzuu 1, Uk. 516. 31 Zaad Mu\u2019ad, Iuzuu 2, Uk. 53. 303 i Z}<\/span><\/em><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">5) Zaad Ma\u2019ad, Iuzuu 2, Uk. 53-54. 311\u00a0<\/span><\/em><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">6) Rahmatun Lil \u2018Alamin, Iuzuu 1, Uk. 101.<\/span><\/em><\/div>\n<div><em><em><span style=\"color: #ff6600;\">7) <\/span><\/em><span style=\"font-size: revert; color: #ff6600;\">Sahihil Bukhari, Iuzuu 1, Uk. 554. 306<\/span><\/em><\/div>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM Kazi ya kuwatafuta (Mtume (\ufdfa) na rafiki yake) ilisimama baada ya kuendelea kwa muda wa siku tatu pasina mafaniko yoyote. Mtume wa Mwenyezi Mungu na rafiki yake walijiandaa kutoka na kueleka Madina. Walikuwa wamemkodi Abdillah bin Urayqit Al-Laythy ambaye aljkuwa ni mwongozaji hodari wa njia. Alikuwa kafiri lakini walimwamini kwa hilo, walimkabidhi wanyama [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":15476,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[57],"tags":[],"class_list":["post-21935","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-sera-ya-mtume"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/21935","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=21935"}],"version-history":[{"count":13,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/21935\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":22531,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/21935\/revisions\/22531"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/15476"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=21935"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=21935"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=21935"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}