{"id":21672,"date":"2023-08-03T12:56:16","date_gmt":"2023-08-03T12:56:16","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=21672"},"modified":"2023-08-10T11:32:14","modified_gmt":"2023-08-10T11:32:14","slug":"hijra-ya-mtume-%ef%b7%ba","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/hijra-ya-mtume-%ef%b7%ba\/","title":{"rendered":"HIJRA YA MTUME \ufdfa"},"content":{"rendered":"<hr \/>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"font-size: 18pt; color: #ff6600;\">AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM<\/span><\/p>\n<hr \/>\n<p>Yalipokamilia Maamuzi ya dhulma ya kumwua Mtume (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>), aliteremka Jibril (Alayhi Salaam) akiwa na wahyi kutoka kwa Mola wa viumbe Aliye Mtukufu na Alimueleza njama za Makuraishi dhidi yake na kuwa Mwenyezi Mungu (\ufdfb) Amempa ruhusa ya kuhama na akampangia wakati wa kuhama kwa kusema:<em><span style=\"color: #0000ff;\"> \u201dUsiku huu Usilale juu ya tandiko lako unalolalia kila siku.\u201d\u00a0 <\/span><\/em><span style=\"color: #000000;\">(1)\u00a0<\/span><\/p>\n<p>Mtume (<strong>\ufdfa<\/strong>) akaenda kwa Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) mchana ili wamalizie taratibu za safari yao ya Hijra. Aisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) alisemaa &#8220;Wakati sisi tumekaa nyumbani kwa Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) mchana, alisema msemaji kumwambia Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake), Angalia, Huyu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) amejifunika uso&#8217;, ulikuwa ni wakati ambao si kawaida yake kutujia kuna jambo lililomletaz Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) akasema, <span style=\"color: #0000ff;\"><em>\u201dUkombozi ni wake, kwa baba yangu na mama yangu, kuna jambo lililomleta saa hizi.\u201d<\/em><\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">Aisha<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) alisemaa \u201dMtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>), akapiga hodi akaruhusiwa, akaingia\u201d, na akasema Mtume (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) kumwambia Abubakar (r.a), <span style=\"color: #0000ff;\"><em>\u201dWatoe nje walioko ndani\u201d<\/em><\/span>, <span style=\"color: #ff6600;\">Abubakar<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) akasema: <em>\u201dKwa hakika hawa ni watu wako &#8211; ninakukomboa kwa baba yangu na mama yangu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.\u201d<\/em> Mtume (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) akasema, <span style=\"color: #0000ff;\"><em>&#8220;Kwa hakika mimi nimeruhusiwa kuhama.\u201d<\/em><\/span><span style=\"color: #ff6600;\"> Abubakar<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) akasema: <em>\u201dNinaomba nifuatane na wewe\u00a0 ninakukomboa kwa baba yangu na mama yangu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>).&#8221;<\/em> Naye Mtume (<em><span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span><\/em>) akajibu, \u201dNdiyo (2)<\/p>\n<p>Baada ya kukamilisha mazungmnzo yao juu ya mpango wao wa kuhama Mtume wa Mwenyezi Mungu (<em><span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span><\/em>) alirejea nyumbani kwake, akiungojea usiku.<\/p>\n<p><span style=\"color: #993300;\"><strong>Kuzingirwa kwa Nyumba ya Mtume<span style=\"color: #993300;\"> (<em>\ufdfa <\/em>)<\/span><\/strong> <\/span><\/p>\n<p>Wakubwa wa waovu wa Makuraishi waliutumia mchana wao katika maandalizi kwa ajili ya kuutekeleza mpango uliokwisha amuliwa na Bunge lao wakati wa asubuhi. Kwa ajili ya utekelezaji wa jambo hilo walichaguljwa viongozi kumi na wawili: &#8211;<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">1. Abu Jahli bin Hisham\u00a0 <\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">2. Al- Hakama bin Abiy Al-\u2019Assi <\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">3. \u2019Uqbah bin Abiy&#8217;Muait-i <\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">4. Al-Nadhri bin A1-Harith <\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">5. Umayya bin Khalaf <\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">6. Zam\u2019a bin Al &#8211; Aswad <\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">7. Tuaymah bin Adiyy <\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">8. Abu Lahb <\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">9. Ubay bin khalaf <\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">10. Nabih bin Al-Hajjaji <\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">11. Ndugu yake Munabbihi bin Al- Hajjajim. <span style=\"color: #000000;\">(3)<\/span><\/span><\/p>\n<p>Ibn Ishaq amesema, \u201dKilipoingia kiza walikutana maka\ufb01ri mlangoni mwa nyumba ya Mtume (<em><span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa <\/strong><\/span><\/em>) wakimsubiri atakapolala wamvamie. Walikuwa na mategemeo makubwa ya kufanikiwa kwa njama hizo. <span style=\"color: #ff6600;\">Abu Jahl<\/span> alisimama kwa kiburi na kuwahulubia wenzake walioizingira nyumba ya Mtume (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa <\/strong><\/span>) kwa kufanya maskhara na kumcheza shere Mtume (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa <\/strong><\/span>), &#8220;Muhammad anadai kwamba iwapo mtamfuata katika dini yake mtakuwa wafalme wa Waarabu na Waajemi, na kisha kufufuliwa baada ya kufa kwenu mmefanyiwa mabustani kama mabustani ya Jordan. Iwapo hamtamfuata na kufanya kazi mliyotumwa basi atakuchinjeni, na baadaye mtafufuliwa baada ya kufa kwenu, kisha mtatupwa motoni na kuchomwa (4) Walikuwa wamekubaliana kumwua baada ya nusu ya usiku, wakaupitisha usiku wakiwa macho wakingojea saa ya kupulizwa kipenga. Mwenyezi Mungu (\ufdfb) ni Mwenye Kushjnda hila zote. Uko mikononi Mwake Ufalme wa mbinguni na ardhini, Anafanya Alitakalo, na Yeye Ndiye Anayenusuru viumbe, kwa hakika Aliyafanya yale ambayo Alimwahidi kwayo Mtum\u00e9 (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>). Baada ya hapo Anamkumbusha Mtume (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) :<\/p>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">\u0648\u064e\u0625\u0650\u0630\u06e1 \u064a\u064e\u0645\u06e1\u0643\u064f\u0631\u064f \u0628\u0650\u0643\u064e \u0671\u0644\u0651\u064e\u0630\u0650\u064a\u0646\u064e \u0643\u064e\u0641\u064e\u0631\u064f\u0648\u0627\u0652 \u0644\u0650\u064a\u064f\u062b\u06e1\u0628\u0650\u062a\u064f\u0648\u0643\u064e \u0623\u064e\u0648\u06e1 \u064a\u064e\u0642\u06e1\u062a\u064f\u0644\u064f\u0648\u0643\u064e \u0623\u064e\u0648\u06e1 \u064a\u064f\u062e\u06e1\u0631\u0650\u062c\u064f\u0648\u0643\u064e\u06da \u0648\u064e\u064a\u064e\u0645\u06e1\u0643\u064f\u0631\u064f\u0648\u0646\u064e \u0648\u064e\u064a\u064e\u0645\u06e1\u0643\u064f\u0631\u064f \u0671\u0644\u0644\u0651\u0647\u064f\u06d6 \u0648\u064e\u0671\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u064f \u062e\u064e\u064a\u06e1\u0631\u064f \u0671\u0644\u06e1\u0645\u064e\u0670\u0643\u0650\u0631\u0650\u064a\u0646\u064e<\/span><\/p>\n<p><em><span style=\"color: #0000ff;\">\u201dNa walipo kupangia mpango walio kufuru wakufunge, au wakuuwe, au wakutoe. Wakapanga mipango yao, na Mwenyezi Mungu akapanga yake. Na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa mipango &#8221;\u00a0<\/span><\/em> (8:30)\u00a0 \u00a02 9 1<\/p>\n<p><span style=\"color: #993300;\"><strong>Mtume (\ufdfa) Anaiacha Nyumba yake:<\/strong> <\/span><\/p>\n<p>Pamoja na ukamilifu wa maanaalizi ya Makuraishi katika kuutekeleza mpango wao, kwa hakika walishindwa vibaya sana. Usiku huo Mtume wa Mwenyezi (\ufdfb) alimwambia <span style=\"color: #ff6600;\">Ali bin Abu Twalib;<\/span> \u2018<em><span style=\"color: #0000ff;\">Lala juu ya tandiko langu, na jifunike shuka yangu hii ya kihadharami ya kijani, hakitapenya kwako kitu unachokichukia.&#8217;<\/span><\/em> Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) alikuwa akilala katika shuka yake hiyo. (5)<\/p>\n<p>Kisha, Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) alitoka na kuzipenya safu zao, akachukua gao la mchanga, akawa anaunyunyiza juu ya vichwa vyao, wakati huo Mwenyezi Mungu (\ufdfb) Ameyakamata macho yao hawamuoni, akatoka huku akisoma:<\/p>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">\u0648\u064e\u062c\u064e\u0639\u064e\u0644\u06e1\u0646\u064e\u0627 \u0645\u0650\u0646\u06e2 \u0628\u064e\u064a\u06e1\u0646\u0650 \u0623\u064e\u064a\u06e1\u062f\u0650\u064a\u0647\u0650\u0645\u06e1 \u0633\u064e\u062f\u0651\u0657\u0627 \u0648\u064e\u0645\u0650\u0646\u06e1 \u062e\u064e\u0644\u06e1\u0641\u0650\u0647\u0650\u0645\u06e1 \u0633\u064e\u062f\u0651\u0657\u0627 \u0641\u064e\u0623\u064e\u063a\u06e1\u0634\u064e\u064a\u06e1\u0646\u064e\u0670\u0647\u064f\u0645\u06e1 \u0641\u064e\u0647\u064f\u0645\u06e1 \u0644\u064e\u0627 \u064a\u064f\u0628\u06e1\u0635\u0650\u0631\u064f\u0648\u0646\u064e<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\"><em>Tumeweka kizuizi mbele yao, na kizuizi nyuma yao, na tumewafunika macho yao; kwa hivyo hawaoni. (36: 9)<\/em> <\/span><\/p>\n<p>Katika wao hakuna aliyesalimika, wote walikuwa wamewekwa mchanga katika vichwa vyao. Mtume (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) akaenda nymnbani kwa <span style=\"color: #ff6600;\">Abubakar<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake), wakatokea katika mlango mdogo katika nyumba ya <span style=\"color: #ff6600;\">Abubaka<\/span>\u00a0(Radhi za Allah ziwe juu yake) na kuondoka usiku huo huo mpaka wakafika katika pango la Thouri uelekeo wa Yemen. Wazingiraji walikuwa bado wanasubiri\u00a0kufika kwa saa ya kupigwa kipenga, na nyuma kidogo kabla ya kufika kwa muda huo kuliwadhihirikia kushindwa kwao.<\/p>\n<p>Alikuja mtu ambaye hakuwa pamoja nao tokea mwanzo, akawaona wakiwa mlangoni kwa Mtume (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) akawauliza; <em>\u201dNi kitu gani mnachokingojea hapa?.\u201d<\/em> Wakamjibu; <em>&#8220;Muhammad.&#8221;<\/em> Akawaambia, <em>\u201dMmetoka kapa na mmepata hasara, ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, amewapitieni na nyote amekunyunyizieni mchanga vichwani mwenu, na ameondoka kama alivyokuwa amepanga.\u201d<\/em> Wakasema, \u201dKwa hakika hatukumwona,\u201d Wakasimama huku wakikung&#8217;uta michanga kutoka vichwani mwao,-kabla ya kuchukua hatua yoyote usiku ule walichungulia katika upenyo wa mlango na wakamwona mtu amelala katika tandiko la Mtume (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>), wakasema, \u201dKwa hakika Muhammad bado amelala na ile ni shuka yake, waliendelea na hali hiyo mpaka wakapambazukiwa&#8221;, na Ali (Radhi za Allah ziwe juu yake) akasimama kutoka katika tandiko. Wakafedheheka. Wakamwuliza kuhusu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w), akawajibu, \u201dSina ujuzi wa khabari zake.<\/p>\n<div>\n<hr \/>\n<\/div>\n<div><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>1) Ibn Hisham, juzuu 1, Uk. 482. Zaadil Ma\u2019ad, Juzuu 2, Uk. 52.<\/em><\/span><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">2) Sahihil Bukhari, Juzuu 1, Uk. 553.<\/span><\/em><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">3) Zaad Ma\u2019ad, Iuzuu 2, Uk. 52. 289<\/span><\/em><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">4) Ibid. uk. 483.<\/span><\/em><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">5) Ibid. Uk. 483. Zaad Ma&#8217;rzd, Juzuu 2, Uk. 52<\/span><\/em><\/div>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM Yalipokamilia Maamuzi ya dhulma ya kumwua Mtume (\ufdfa), aliteremka Jibril (Alayhi Salaam) akiwa na wahyi kutoka kwa Mola wa viumbe Aliye Mtukufu na Alimueleza njama za Makuraishi dhidi yake na kuwa Mwenyezi Mungu (\ufdfb) Amempa ruhusa ya kuhama na akampangia wakati wa kuhama kwa kusema: \u201dUsiku huu Usilale juu ya tandiko lako unalolalia [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":15476,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[57],"tags":[],"class_list":["post-21672","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-sera-ya-mtume"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/21672","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=21672"}],"version-history":[{"count":8,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/21672\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":21845,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/21672\/revisions\/21845"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/15476"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=21672"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=21672"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=21672"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}