{"id":21466,"date":"2023-07-20T11:12:10","date_gmt":"2023-07-20T11:12:10","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=21466"},"modified":"2023-07-20T11:12:13","modified_gmt":"2023-07-20T11:12:13","slug":"mambo-yaliyotanguli-hijra-kuhama-kwa-mtume-%ef%b7%ba","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/mambo-yaliyotanguli-hijra-kuhama-kwa-mtume-%ef%b7%ba\/","title":{"rendered":"MAMBO YALIYOTANGULI HIJRA, (KUHAMA KWA MTUME \ufdfa."},"content":{"rendered":"<hr \/>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"font-size: 18pt; color: #ff6600;\">AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM<\/span><\/p>\n<hr \/>\n<p>Baada ya kukamilika kwa mkataba wa Al-Aqaba wa pili, na Uislamu kufanikiwa kuanzisha Dola yake katikati ya jangwa lililojaa uka\ufb01ri na ujinga, na kwa kuzingatia hali ngumu ambayo Uislamu tokea mwanzo wa Da&#8217;awa yake uliyapata pale Makka, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) aliwaruhusu Waislamu kuhama na kwenda Yathrib (Madina).<\/p>\n<p>Katika jumla ya vikwazo vya Hijra vilikuwa ni mtu kupoteza maslahi yake ya kidunia na kupelekea kujitoa mhanga, kwa kuacha mali na kuhatarisha maisha yake. Jambo ambalo linaweza kummaliza tu pale atakapoanza safari yake ya Hijra.<\/p>\n<p>Waislamu walianza kuhama huku wakiwa wanayaelewa mambo yote hayo. Mushirikina wakawazuia wasihame, kwa sababu ya yale ambayo walikuwa wanayaogopa miongoni mwa hatari za Waislamu kukusanya nguvu zao nje ya eneo la Makka. Mfano wa hayo:<\/p>\n<p>1. <span style=\"color: #ff6600;\">Abu Salama<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) alikuwa mtu wa kwanza kuhama, alihama kabla ya Ba&#8217;ia Al-Aqabah Al-Kubra (kubwa) kwa muda wa mwaka mmoja, kwa mujibu wa mapokezi ya <span style=\"color: #808000;\">Ibn Ishaq,<\/span> akiwa pamoja na mkewe na mtoto wake. Alipokuwa tayari kwa safari, wakweze walimwambia, \u2019Wewe umetushinda, Lakini huyu mtu wetu (mke wake Abu Salama) hatukuachii uende naye.\u201d <span style=\"color: #ff6600;\">Abu Salama<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) akanyang\u2019anywa mkewe na hilo likawafanya nduguze <span style=\"color: #ff6600;\">Abu Salama<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) wakasirishwe na jambo hili alilofanyiwa ndugu yao, wakasema, \u201dHatumwachi mwanetu kwa mama yake kwani mmemnyang\u2019anya kutoka kwa ndugu yetu.&#8221; Wakavutana kumnshindania yule mtoto na kuondoka naye.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\"><span style=\"color: #000000;\"><strong>1.<\/strong><\/span> Abu Salama<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) akaelekea Madina peke yake ilhali mkewe baada ya kuondoka mumewe na kupotea kwa mwanawe akawa anatoka kila siku asubuhi nje kwenda kwenye ardhi yenye changarawe huku akilia mpaka jioni, aliendelea katika hali hiyo kwa muda wa mwaka mzima. Mmoja kati ya ndugu zake akamhurumia. Akasema: <em>\u201dKwa nini hanmiruhusu nikamfariji huyu maskini?<\/em> Mmemtenganisha na mume wake na mtoto wake. Wakamwambia, <em>\u201dUngana na mume wako kama unataka\u201d,<\/em> akataka mtoto arejeshwe kwa jamaa zake ndugu wa mume wake. Akatoka akiwa anakusudia kwenda Madina, safari ambayo inafikia kiasi cha kilometa mia tano\u00a0 na hakuwa na mtu yeyote pamoja naye miongoni mwa viumbe wa Mwenyezi Mungu mpaka alipofika mahali paitwapo <span style=\"color: #ff6600;\">Tani\u2019im.<\/span> Alikutana na \u2019<span style=\"color: #ff6600;\">Uthman bin Twalha bin Abi Twalha<\/span> na baada ya kuielewa hali yake, alifuatana naye mpaka akamfikisha Madina. Alipouona mji wa Qubaa alisema; Mume wako yuko katika kijiji hiki, ingia kwenye kijiji kwa baraka za Mwenyezi Mungu (\ufdfb) kisha <span style=\"color: #ff6600;\">\u2019Uthmani<\/span> akaondoka kurejea Makka. (1)<\/p>\n<p><span style=\"color: #000000;\"><strong>2.<\/strong> <\/span><span style=\"color: #ff6600;\">Suhayb<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) alipotaka kuhama makafiri wa Kikuraishi walimwambia, \u201d<em>Ulikuja hapa ukiwa mnyonge na lofa, mali yako imekuwa nyingi na kutajirika na kufikia hali hii ambayo umeifikia ndio sasa unataka kuondoka na mali yako? Tunaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu hilo halitakuwa.\u201d<\/em> <span style=\"color: #ff6600;\">Suhayb<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) akawauliza, <em>\u201dJe, mnaonaje nikiwapeni mali yangu yote mtaniacha niende zangu?<\/em> Wakasema, \u201dNdiyo.\u201d Akasema, <span style=\"color: #008000;\"><em>\u201d Kwa hakika mimi nimewapeni mali yangu yote.\u201d<\/em><\/span> Mtume wa Mwenyezi Mungu (<strong>\ufdfa<\/strong>) akapata khabari na akasema, <span style=\"color: #0000ff;\">\u201dAmepata faida Suhayb, amepatafaida\u00bb<\/span> (2).<\/p>\n<p><span style=\"color: #000000;\"><strong>3.<\/strong> <\/span><span style=\"color: #ff6600;\">Umar bin Al-Khattab<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) na <span style=\"color: #ff6600;\">Ayyashi bin Abi Rabia<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) na <span style=\"color: #ff6600;\">Hisham ibn Assi bin Wail<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake), waliahidiana kukutana asubuhi siku iliyofuata, kisha wahame kuelekea Madina. Walikutana <span style=\"color: #ff6600;\">\u2019Umar<\/span> na <span style=\"color: #ff6600;\">Ayyash<\/span> lakini <span style=\"color: #ff6600;\">Hisham<\/span> alizuiwa.<\/p>\n<p>Walipo\ufb01ka Madina walishukia Qubaa, Abu jahli na ndugu yake Al-Harith walikuja kwa <span style=\"color: #ff6600;\">Ayyash.<\/span> Wakamwambia, <em>\u201dHakika mama yako ameweka nadhiri kuwa hatochana nywele zake na hatokaa kwenye kivuli hadi akuone. Kwa hiyo mhurumie.\u201d<\/em> \u2019Umar akamwambia, <span style=\"color: #808000;\"><em>\u201dEwe Ayyash, kwa hakika kwa jinsi mambo yalivyo, Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu (\ufdfb) watu wako wanakusudia kukufitini na Dini yako, kwa hiyo tahadhari nao.\u201d<\/em><\/span> <em><span style=\"color: #808000;\">\u201dNinaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu (\ufdfb), kama chawa watamuudhi mama yako kiasi cha kutosha bila ya shaka yoyote atachana nywele zake, na joto la jua la Makka likimzidi atajifunika.\u201d<\/span><\/em> <span style=\"color: #ff6600;\">Ayyash<\/span> akaamua kutoka nao, ili ahalalishe kiapo cha mama yake.<span style=\"color: #ff6600;\"> \u2019Umar<\/span> akamwambia, <em>&#8220;Kama ukiwa umechukuwa uamuzi huo chukua ngamia wangu huyu kwani ngamia huyu ni bora na mwepesi,<\/em> <span style=\"color: #808000;\"><em>usiache mgongo wake, na iwapo utapata mashaka kuhusu jambo lolote kutokana na watu hawa, jiokoe ukiwa juu ya Ngamia huyu.\u201d<\/em><\/span> Akatoka akiwa juu ya ngamia huyo pamoja nao, mpaka walipokuwa njiani, Abu Jahl akamwambia, \u201dEwe mtoto wa ndugu yangu, Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, kwa hakika ngamia wangu amekuwa mzito, ni bora tukapokezana? Akasema, \u201dSi vibaya, niko tayari kufanya hivyo\u201d, akampigisha magoti, waliposhuka na wote kuwa chini walimrukia na kumkamata kisha wakamfunga kamba, na kuingia naye Makka wakati wa mchana na hali ya kuwa amefungwa. Wakawa wakiwanadia watu; <em>&#8220;Enyi watu wa Makka wajinga ndio waliwao, wafanyieni wajinga wenu hivi kama&#8217; tulivyomfanya sisi huyu (3)<\/em><\/p>\n<p>Hii ni mifano mitatu ya yale ambayo Mushrikina walikuwa wakiwafanyia wale ambao walikuwa wanataka kuhama. Pamoja na yote haya walitoka watu, makundi kwa makundi wanafuatana. Baada ya miezi tokea Mkataba wa Al-Aqabah Al-Kubra, Waislamu hawakubakia Makka isipokuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (<strong>\ufdfa<\/strong>), <span style=\"color: #ff6600;\">Abubakar<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) na <span style=\"color: #ff6600;\">Ali<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake), wengine ni wale waliozuiliwa na Mushirikina kwa kulazimishwa. Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (<strong>\ufdfa<\/strong>) alifanya maandalizi yake akingojea siku atakayopewa amri ya kutoka, akiwa na Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake). (4)<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">Bukhari<\/span> amepokea kutoka kwa <span style=\"color: #ff6600;\">Aisha<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake); Alisema Mtume wa Mwenyezi Mungu (<strong>\ufdfa<\/strong>) kuwaambia Waislamu; <span style=\"color: #0000ff;\">\u201dHakika nimeuona mji wenu wa kuhamia, una mitende iliyo kati ya majabali mawili. Wakahamia baadhi yao Madina na sehemu kubwa ya wale waliokuwa wamehamia Habasha walihamia Madina. Abubakar (alikuwa amejiandaa kuhama kuelekea Madina. Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (<strong>\ufdfa<\/strong>) akamwambia, &#8220;Polepole usiwe na haraka, ninatarajia kupewa ruhusa ya kuhama.&#8221;<\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">Abubakar<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) akamwuliza, &#8220;Hivi unalitarijia jambo_ hilo?.&#8221; Akasema, <span style=\"color: #0000ff;\">\u201dNdiyo.\u201d<\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">Abubakar<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) akaizuia nafsi yake na kumsubiri Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) afuatane naye; \u201cna akaanza matayarisho ya safari kwa kuwaandaa wanyama wake wawili kwa kuwapa chakula kizuri kwa muda wa miezi minne. (5)<\/p>\n<div>\n<hr \/>\n<\/div>\n<div><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>1) Ibn Hislmm, juzuu 1, Uk. 468-470.<\/em><\/span><\/div>\n<div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>2) lbid. Iuzuu 1, Uk. 477.<\/em><\/span><\/div>\n<div><span style=\"color: #808000;\">3)<\/span> Hisham pamoja na \u2019Iyash walibaki wamefungwa na Maka\ufb01ri hadi alipofanya Hijra Mtume (<strong>\ufdfa<\/strong>). Mtume (<strong>\ufdfa<\/strong>) siku moja alisema, <em>&#8216;Ni nani ataniletea \u2019Iyash na Hisham?<\/em> Akajibu Al-Walid bin Al-Walid, \u2018Mimi nitakuletea ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.\u2019 Akaondoka Walid kwa kujificha mpaka Makka, huko akamkuta mwanamke akiwapelekea wakina &#8216;Iyash &#8216;_na Hisham chakula, akamfuatilia mpaka aka\ufb01ka sehemu waliyofungwa. Ilikuwa ni katika nyumba isiyokuwa na dari, ilipo\ufb01ka jioni alipanda ukuta na akawafungua pingu zao na kuwabeba kwenye ngamia wake hadi Madina (Angalia, Ibn Hisham, juzuu 1, Uk 474-476. Sahihil Bukhari, Juzuu 1, Uk. 558.)<\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>4) lZaad Ma&#8217;ad, Iuzuu 2, Uk. 52. 282.<\/em><\/span><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">5) Sahihil Bukhari, juzuu 1, Uk. 553.<\/span><\/em><\/div>\n<\/div>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM Baada ya kukamilika kwa mkataba wa Al-Aqaba wa pili, na Uislamu kufanikiwa kuanzisha Dola yake katikati ya jangwa lililojaa uka\ufb01ri na ujinga, na kwa kuzingatia hali ngumu ambayo Uislamu tokea mwanzo wa Da&#8217;awa yake uliyapata pale Makka, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa) aliwaruhusu Waislamu kuhama na kwenda Yathrib (Madina). Katika jumla ya vikwazo [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":15476,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[57],"tags":[],"class_list":["post-21466","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-sera-ya-mtume"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/21466","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=21466"}],"version-history":[{"count":2,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/21466\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":21468,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/21466\/revisions\/21468"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/15476"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=21466"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=21466"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=21466"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}