{"id":21309,"date":"2023-07-13T10:52:46","date_gmt":"2023-07-13T10:52:46","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=21309"},"modified":"2023-07-13T10:58:37","modified_gmt":"2023-07-13T10:58:37","slug":"mwanzo-wa-mazunumzo-na-ufafanuzi-wa-abbas-kutokana-na-ukumbwa-wa-jukumu","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/mwanzo-wa-mazunumzo-na-ufafanuzi-wa-abbas-kutokana-na-ukumbwa-wa-jukumu\/","title":{"rendered":"MWANZO WA MAZUNUMZO NA UFAFANUZI WA ABBAS KUTOKANA NA UKUMBWA WA JUKUMU."},"content":{"rendered":"<hr \/>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"font-size: 18pt; color: #ff6600;\">AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM<\/span><\/p>\n<hr \/>\n<p>Baada ya kikao kukamilika yalianza mazungumzo kwa kuupitisha mwafaka wa kidini na kijeshi, na mzungumzaji wa kwanza alikuwa ni <span style=\"color: #ff6600;\">\u2019Abbas bin Abdil Muttwalib,<\/span> ammi wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa) ambaye alizungumza ili kuwawekea wazi ukubwa wa jukumu ambalo watakabidhiwa, ikiwa ni matokeo ya muafaka huu, akasema: <em>\u201dEnyi jamaa katika Khazraji! (na walikuwa Waarabu wanawaita Answanfi &#8211; Khazraji \u2014 wale ambao ni Khazraji na wale ambao ni Ausi wote wawili) kwa hakika nyote mnafahamu nafasi aliyonayo Muhammad kwetu sisi. Kwa hakika tumemhami dhidi ya jamaa zetu walio bado katika shirki, kwa hivyo yeye yuko katika nguvu za jamaa zake na kinga katika mji wake. Kwa hakika yeye amewakataa watu wake na anataka kuwaegemeeni na kujiunga nanyi, ikiwa mnaona kuwa mtamtekelezea lile ambalo mmemwita kwalo na kuwa mtamlinda na wale wanaompinga. Basi mnaachwa mbebe jukmnu hilo, na kama mtaona kuwa nyinyi mtamtoa na mtamwachia baada ya kumchukua na kwenda naye kwenu basi tokea sasa mwacheni, kwani yeye yumo katika ulinzi na himaya ya jamaa zake na mji wake.\u201d<\/em> <span style=\"color: #ff6600;\">Ka\u2019ab<\/span> amesema tukamwambia, &#8220;Tumeyasikia yale ambayo umeyasema, zungmnza ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa) na chukua kwa ajili yako binafsi na Mola Wako lile ambalo unalipenda (1) Jibu hili linatufahamisha hali waliyokuwa nayo, misimamo thabiti, azma, ushujaa, imani na ikhlasi zao katika kulibeba jukumu hili kubwa na kuyakubali matokeo yake yenye hatari.<\/p>\n<p>Baada ya hapo Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa) akatoa ufafanuzi wake, na kisha makubaliano yakakamilika.<\/p>\n<p><span style=\"color: #993300;\"><strong>Vifungu vya Mkataba:<\/strong> <\/span><\/p>\n<p>Imam Ahmad ameyapokea haya kutoka kwa Jabir (Radhi za Allah ziwe juu yake) kwa ufafanuzi. Jabir (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema;<\/p>\n<p style=\"text-align: right;\"><span style=\"color: #008000;\">\u0642\u0644\u0646\u0627 : \u064a\u0627 \u0631\u0633\u0648\u0644 \u0627\u0644\u0644\u0647 \u060c \u0639\u0644\u0627\u0645 \u0646\u0628\u0627\u064a\u0639\u0643 \u061f \u0642\u0627\u0644 : \u062a\u0628\u0627\u064a\u0639\u0648\u0646\u064a \u0639\u0644\u0649 \u0627\u0644\u0633\u0645\u0639 \u0648\u0627\u0644\u0637\u0627\u0639\u0629 \u0641\u064a \u0627\u0644\u0646\u0634\u0627\u0637 \u0648\u0627\u0644\u0643\u0633\u0644 \u060c \u0648\u0639\u0644\u0649 \u0627\u0644\u0646\u0641\u0642\u0629 \u0641\u064a \u0627\u0644\u0639\u0633\u0631 \u0648\u0627\u0644\u064a\u0633\u0631 \u060c \u0648\u0639\u0644\u0649 \u0627\u0644\u0623\u0645\u0631 \u0628\u0627\u0644\u0645\u0639\u0631\u0648\u0641 \u0648\u0627\u0644\u0646\u0647\u064a \u0639\u0646 \u0627\u0644\u0645\u0646\u0643\u0631 \u0648\u0623\u0646 \u062a\u0642\u0648\u0644\u0648\u0627 \u0641\u064a \u0627\u0644\u0644\u0647 \u060c \u0644\u0627 \u064a\u0623\u062e\u0630\u0643\u0645 \u0641\u064a \u0627\u0644\u0644\u0647 \u0644\u0648\u0645\u0629 \u0644\u0627\u0626\u0645 \u060c \u0648\u0639\u0644\u0649 \u0623\u0646 \u062a\u0646\u0635\u0631\u0648\u0646\u064a \u0625\u0646 \u0642\u062f\u0645\u062a \u0639\u0644\u064a\u0643\u0645 \u064a\u062b\u0631\u0628 \u060c \u0648\u062a\u0645\u0646\u0639\u0648\u0646\u064a \u0645\u0645\u0627 \u062a\u0645\u0646\u0639\u0648\u0646 \u0645\u0646\u0647 \u0623\u0646\u0641\u0633\u0643\u0645 \u0648\u0623\u0632\u0648\u0627\u062c\u0643\u0645 \u0648\u0623\u0628\u0646\u0627\u0621\u0643\u0645 \u0648\u0644\u0643\u0645 \u0627\u0644\u062c\u0646\u0629 . \u0641\u0642\u0644\u0646\u0627 : \u0646\u0628\u0627\u064a\u0639\u0643<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\">\u201dTulimuuliza\u2018ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa) tunakupa ahadi kwa jumbo gimi?&#8217; Akujibu: \u201dKwanza, Kunisikiliza nu kunitii wakati wote wa uchangamfu na wakati wa uvivu. Pili, Kutoa mali wakati wa uzito na wepesi. Tutu, Kuamrisha mema na kukataza maovu. Nne, Kuwa mtasimamia majukumu kwa ajili ya Allah (\ufdfb) bila kujali lawama ya mwenye kulaumu. Tano, Na kuwa mtaninusuru wakati nitakapo\ufb01ka kwenu Yathrib na kunikinga kwa yale mnayojikinga kwa ajili ya nafsi zenu na wake zenu na watoto wenu , nu nyinyi kwa ajili hiyo mtapata pepo.\u00a0 Tukasema Tumekupa ahadi &#8220;2\u201c<\/span><\/p>\n<p>Katika mapokezi ya <span style=\"color: #ff6600;\">Ka&#8217;ab,<\/span> kutoka kwa <span style=\"color: #ff6600;\">Ibn Ishaq,<\/span> kifungu cha mwisho ka\ufb01ka vifungu hivi alisema: Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa) akazungumza na baadaye akasoma Qur\u2019an na akawakumbusha watu umuhimu wa Kumtii Mwenyezi Mungu (\ufdfb) na akawataka waingie kwenye Uislamu. Kisha akasema: <em><span style=\"color: #0000ff;\">\u201dNinapeana ahadi na nyinyi kuwa mtanikinga na kile ambacho mnanajikinga nacho wake zenu na watoto wenu&#8221;,<\/span><\/em> <span style=\"color: #ff6600;\">Baraa bin Ma&#8217;arour<\/span> akaukamata mkono wake na akasema: <em>\u201dNdiyo ninaapa kwa yule ambaye amekuleta kwa ukweli (kama Mtume) kwa hakika tutakulinda na tunachojilinda nacho, tunakuomba upeane ahadi na sisi, ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w). Tunaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, sisi ni watu wa vita na ni watu wa misimamo, tumeyarithi yote kutoka kwa mababu zetu.\u201d<\/em> <span style=\"color: #ff6600;\">Abu Haytham bin Tayhani<\/span> akayaingilia maneno haya na hali yakuwa Baraa bado anazungumza na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na akasema: <em>\u201dEwe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa); Kwa hakika kati yetu na jamaa zetu wapo watu ambao wanaweza kuivunja ahadi hii (akiwakusudia Mayahudi). Hivi iwapo sisi tutafanya hivyo kisha Mwenyezi Mungu (\ufdfb) Akakupa mafanikio, utarejea kwa watu wako na kutuacha?.&#8221;<\/em> Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa) akatabasamu na akasema: &#8216;Isipokuwa damu kwa damu na ubomoaji kwa ubomoaji Mimi ni miongoni mwenu na nyinyi ni miongoni mwangu, nitapiguna vita na yule ambaye mnapigana naye na nitafunya amani na yule ambuye mnafanya naye amani (3)<\/p>\n<p><span style=\"color: #993300;\"><strong> Kutilia Mkazo Uzito wa Mkataba.<\/strong> <\/span><\/p>\n<p>Baada ya kukamilika kwa mazungumzo kuhusu mashati ya mkataba na kukubaliana namna ya utaratibu wa utekelezaji wake, walisimama watu wawili kutoka katika kundi la kwanza midngoni mwa wale waliosilimu wakati wa msimu wa kumi na moja na kumi na mbili wa Utume, na alisimama mtu mwingine, wote walisisitizia ukubwa wa jukumu lao, ili wasije wakapeana naye ahadi na kula kiapo kwa jambo ambalo bado halijawa wazi kwao, na ili wajue kiwango cha maandalizi yanayotakiwa na kujitoa muhanga na wawe na uhakika na jambo hilo.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">Ibn Ishaq<\/span> amesema: \u201dWalipokutana kwa madhumuni ya kutoa ahadi <span style=\"color: #ff6600;\">\u2018Abbas bin &#8216;Ubada bin Nadhla<\/span> aliwauliza, <em>\u201dJe mnajua bmnapeana ahadi kwa jambo gani na mtu huyu?.<\/em>\u201d Wakajibu,<em> \u201dNdiyo.&#8221;<\/em> Akasema: <em>&#8220;Kwa hakika nyinyi mnapeana naye ahadi ya kushirikiana naye katika kazi yake ya kutangaza Dini, na kumpiga vita adui yeyote, awe mwekundu au mweusi katika watu kama mtaona kuwa ipo haja ya kufanya hivyo kwa hofu ya kuteketezewa mali zenu, au mkiwaona watukufu wenu wanauliwa mtamwachia na kumtoa kwa adui?. Hili lisemeni kutokea sasa, hata hivyo; Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu iwapo mtalifanya jambo hilo basi huo ni udhalili wenu wa duniani na kesho akhera. Kama mnaona kuwa nyinyi mtamtekelezea lile mlilomwitia, hata kwa kuteketezwa mali na kuuliwa kwa Watukufu wenu mchukuweni. Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, kwa hakika kumnchukua kwenu ndio jambo la kheri kwenu hapa duniani na kesho akhera.&#8221;<\/em> Wakasema; &#8220;Kwa hakika sisi tunamchukua bila ya kujali kuteketezwa kwa mali au kuuliwa kwa Watukufu wetu. Tutapata nini, ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa) sisi tukikutekelezea hilo?.\u201d Akawajibu; \u201dMtapata pepo.\u201d Wakamwambia, \u201dUnyooshe mkono wako, akaukunjua mkono wake wakampa ahadi ya ut-ii.<\/p>\n<p>Katika mapokezi ya Jabir (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema; \u201dTukasimama na tukatoa ahadi, wakati huo <span style=\"color: #ff6600;\">As\u2019ad bin Zurarah<\/span> amekamatwa mkono wake &#8211; na hali ya kuwa yeye ni mdogo zaidi wa Wale watu sabini waliokuwepo.\u201d Akasema; &#8220;Taratibuni enyi watu wa Yathrib, kwa hakika sisi hatukusa\ufb01ri kwa ngamia kuja huku kwa madhumuni ya kuja kwake, ila ni baada ya kuelewa kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu (\ufdfb). Tokea leo, hili lizingatiwe kuwa ni kutengana na Waarabu wote na kuuliwa kwa wabora wetu, na kuwakateni nyinyi panga. Kama mko tayari kuyavumilia hayo mchukuweni na malipo yenu yako kwa Mwenyezi Mungu (\ufdfb). Iwapo nyinyi mna hofu juu ya nafsi zenu, hofu kubwa, basi mwacheni, maana hilo ni udhuru wa kutosha kwenu mbele ya Mwenyezi Mungu (\ufdfb).<\/p>\n<p><span style=\"color: #993300;\"><strong>Kiapo cha Ahadi ya Utii <\/strong><\/span><\/p>\n<p>Baada ya kupitishwa vifungu vya mkataba na baada ya mkazo na kusisitizwa umuhimu wa jambo lenyewe, Mkataba ulianzwa kufungwa kwa kupeana mikono. Jabir (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema; &#8220;Baada ya kuyazungumzia maneno ya <span style=\"color: #ff6600;\">As\u2019ad, bin Zurarah;<\/span> wakasema Ewe As&#8217;ad. tuondolee mkono wako, tunaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu (\ufdfb) kuwa hatuuachi mkataba huu na hatutauvunja.<\/p>\n<p>Wakati huo ndio As&#8217;ad alielewa kiwango cha maandalizi ya wale watu kwa ajili ya kujitoa muhanga katika njia ya Dini. Kutokana na hilo akapata uhakika wa kuungwa mkono, hasa kwa vile yeye ndiye aliyekuwa mlinganiaji mkubwa pamoja na <span style=\"color: #ff6600;\">Mus\u2019ab bin \u2019Umair<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) na kwa kawaida yeye ndiye aliyekuwa kiongozi wa Kidini wa hawa waliokuwa wanatoa ahadi, yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kutoa ahadi hii.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">Ibn Ishaq<\/span> alisema; \u201dBanu Najjari wanadai kuwa Abu As&#8217;ad bin Zurarah ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kumpa mkono wa utii Mtume (\ufdfa), na baada yake wengine wakafuata katika kutoa ahadi zao.\u201d<\/p>\n<p>Jabir (Radhi za Allah ziwe juu yake) alisema, \u201dTukasimama mbele yake mtu mmoja baada ya mwingine, akapokea ahadi kutoka kwa kila mmoja wetu, naye akimbashiria pepo kila aliyetoa ahadi.<\/p>\n<p>Ama kuhusu ahadi ya wale wanawake wawili ambao walishuhudia tukio hilo, ahadi yao ilitolewa kwa matamko tu bila ya kupeana mikono, kwani Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa) hakuwa na tabia ya kuwapa mkono wanawake ajnabi, isipokuwa wakeze na binti zake_. (4)<\/p>\n<p><span style=\"color: #993300;\"><strong> Viongozi Kumi na Wawili<\/strong> <\/span><\/p>\n<p>Baada ya kukamilika kwa mkataba, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa) alitaka kuchaguliwa kwa viongozi kumi na wawili watakaokuwa wasimamizi wa jamaa zao, na watakaobeba majukumu ya kuhakikisha utekelezwaji wa vifungu vya mkataba. Aliwaambia watu waliokuwa wamekusanyika pale, <span style=\"color: #0000ff;\">\u201dNichagulieni kutoka miongoni mwenu viongozi kumi na wawili ili wawe wasimamizi wa jamaa zao, kwa yale mambo ambayo yako kwao.\u201d<\/span> Uchaguzi ukafanyika na wakati ule ule wakachaguliwa watu tisa kutoka upande wa Khazraji na watatu kutoka upande wa Ausi, kama ifuatavyo: &#8211;<\/p>\n<p><span style=\"color: #993300;\"><strong>Viongozi Kutoka Upande wa Khazraji<\/strong><\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\"> 1. As&#8217;ad bin Zurarah bin Adas<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">2. Sa\u2019ad bin Rabia bin \u2019Amru<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">3. Abdullah bin Rawaha bin Tha&#8217;alaba<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">4. Rafii bin Malild bin A1-Ajilan<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">5. Al-Baraa bin Maarour bin Swakhri<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">6. Abdullah bin \u2019Amru bin Hiram<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">7. \u2019Ubada bin Swamiti bin Qaysi<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">8. Sa\u2019ad bin \u2019Ubada bin Dolaym<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">9. Al-Mundhiri bin \u2019Amru bin Khunaysi<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #993300;\"><strong>Viongozi Kutoka Upande wa Ausi<\/strong> <\/span><\/p>\n<p>1. \u2019Usaid bin Khudhair bin Simaki<\/p>\n<p>2. Sa\u2019ad bin Khaithama bin Harithi<\/p>\n<p>3. Rifaa bin Abdul A1- Mundhir bin Zubair. (5)<\/p>\n<p>Baada ya uchaglwi kukamilika, Mtume (\ufdfa) alichukua ahadi nyingine kutoka kwao kwa ile sifa yao ya kuwa viongozi ambao wangewajibika. Aliwaambia; <span style=\"color: #0000ff;\">\u201dNyinyi ni wadhumini wa yule yaliyo kwa jamaa zenu kama walivyopewa dhamana wafuasi wa Isa mwana wa Mariam na mimi ni mdhamini juu ya Waislamu wote.&#8221;<\/span> Wote wakaitikia, \u201dNdiyo.&#8221;<\/p>\n<div>\n<hr \/>\n<\/div>\n<div><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>1) <span style=\"font-size: revert; color: initial;\"><span style=\"color: #ff6600;\">Ibn Hisham, Iuzuu 1, Uk. 440-441<\/span><\/span><\/em><\/span><\/div>\n<div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>2) Imam Ahmad, imesahihishwa na Al-Hakim na Ibn Hibban (Angalia Mukhtasar Siratu Rrasul, Uk. 155; na llm Hisham, Iuzuu 1, Uk. 454).Arrahiq Al-Makhtuum Uk -265-266<\/em><\/span><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\">3)<\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">Ibn Qutayba amesema, \u2018Wakati wa kufanya mikataba ya kunusuriana na kusaidiana au mikataba ya ujirani, Waarabu walikuwa na msemo waliopenda kuutumia; damu yangu ni damu yako na kubomoa kwako ni kubomoa kwangu-maana yake-huu ni mshikamano wa kidugu. (Wafasiri) 1\u201c Ilm Hislmm, juzuu 1, Uk. 442. 269<\/span><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>4) Sahihi Muslim Juzuu 2, Uk 131<\/em><\/span><\/div>\n<div><em><span style=\"color: #ff6600;\">5) Ibnu\u00a0Hisham, juzuu 1, Uk. 443-444, 446.<\/span><\/em><\/div>\n<\/div>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM Baada ya kikao kukamilika yalianza mazungumzo kwa kuupitisha mwafaka wa kidini na kijeshi, na mzungumzaji wa kwanza alikuwa ni \u2019Abbas bin Abdil Muttwalib, ammi wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa) ambaye alizungumza ili kuwawekea wazi ukubwa wa jukumu ambalo watakabidhiwa, ikiwa ni matokeo ya muafaka huu, akasema: \u201dEnyi jamaa katika Khazraji! (na walikuwa [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":15476,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[57],"tags":[],"class_list":["post-21309","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-sera-ya-mtume"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/21309","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=21309"}],"version-history":[{"count":5,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/21309\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":21315,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/21309\/revisions\/21315"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/15476"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=21309"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=21309"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=21309"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}