{"id":21305,"date":"2023-07-13T08:56:24","date_gmt":"2023-07-13T08:56:24","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=21305"},"modified":"2023-07-13T09:03:17","modified_gmt":"2023-07-13T09:03:17","slug":"bayatul-aqabah-kiapo-cha-ahadi-ya-utii-cha-pili","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/bayatul-aqabah-kiapo-cha-ahadi-ya-utii-cha-pili\/","title":{"rendered":"BAY\u2019ATUL AQABAH KIAPO CHA AHADI YA UTII CHA PILI."},"content":{"rendered":"<hr \/>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"font-size: 18pt; color: #ff6600;\">AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM<\/span><\/p>\n<hr \/>\n<p>Wakati wa msimu wa Hijja katika mwaka wa kumi na tatu wa Utume sawasawa na mwezi wa Juni mwaka 622 C.E. walihudhuria Waislamu zaidi ya sabini kutoka Yathrib kwa madhumuni ya kutekeleza matendo ya Hijja. Walikuja mahujaji wa kutoka huko wakichanganyika na Mushirikina. Waislamu hawa walikuwa wameulizana kati yao (hali ya kuwa wao bado wako &#8220;Yathrib au walipokuwa njiani), \u2018Mpaka. lini tutamwacha Mjumb\u00e9 wa Mwenyezi\u2018 Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) akizunguka zunguka na kufukuzwa katika majabali ya Makka akiwaogopa Mushiriki.na?.\u2019 Walipo\ufb01ka Makka walifanya mawasiliano ya siri kati yao na Mtume (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) yaliyowafanya kukubaliana kuwa makundi yao mawili yakutane katikati ya masiku ya Tashriq, katika bonde ambalo liko mbele ya Aqabah mahali ambapo kipo kikuta cha mwanzo cha Mina na kuwa kukutana huko kufanyike kwa siri kubwa wakati wa kiza cha usiku. Na tumwache mmoja wa viongozi wa Answari atusimulie kuhusu mkutano huu wa kihistoria ambao uliyageuza mapito ya masiku katika mapambano ya Upagani na Uislamu;<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">Ka&#8217;ab bin Malik Al Answary<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yao) alisema;<em> \u201dTulitoka tukielekea kwenye Hijja, na tulikuwa tumemuahidi Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\"><strong>\ufdfa<\/strong><\/span>) kuwa tutakutana naye pahala tulipoahidiana, katikati ya masiku ya Tashriq na ulikuwa ni usiku tulioahidiana na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (<strong>\ufdfa<\/strong>). Pamoja nasi alikuwepo <span style=\"font-size: revert; color: initial;\">Abdullah bin Amri bin Hizam. Bwana miongoni mwa mabwana zetu na Mtukufu miongoni mwa Watukufu wetu, tulimchukua pamoja nasi\u00a0 wakati wote tulikuwa tukiwa\ufb01cha jamaa z\u00e9tu waliokuwa bado ni Mushirikina jambo Tukazungumza nae; &#8220;Ewe Aba Jabir kwa hakika wewe ni Bwana miongoni mwa mabwana zetu na ni Mtukufu miongoni mwa Watukufu wetu, kwa hakika sisi tunakushauri kuwa ni bora ukaachana na itikadi uliyonayo ili usije kuwa kuni za moto wa Jahannam. <\/span><\/em><\/p>\n<p><span style=\"font-size: revert; color: initial;\">Baada ya hapo tukamlingania aufate Uislamu na tukamweleza kuhusu ahadi tuliyonayo ya kukutana na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (<strong>\ufdfa<\/strong>) huko Aqaba, alisilimu na akahudhuria pamoja nasi Aqaba akiwa kiongozi.\u201d <span style=\"color: #ff6600;\">Kaab alisema:<\/span> \u201dUsiku ule tulilala pamoja na jamaa zetu katika kambi zetu mpaka ilipopita theluthi ya usiku, tulitoka katika kambi zetu ili kwenda kutimiza ahadi tuliyowekeana na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (<strong>\ufdfa<\/strong>), tulichomoka kama ndege wadogo, kwa kuji\ufb01cha mpaka tukakusanyika katika bonde mbele ya Aqabah kama tulivyokubaliana, Tukiwa watu sabini na watatu wanaume na wanawake wawili katika wake zetu. Nao ni<span style=\"color: #ff6600;\"> Sibah bint Ka\u2019ab<\/span> na <span style=\"color: #ff6600;\">Ummu \u2019Amaarah katika Banu Maazin bin Najjar,<\/span> na <span style=\"color: #ff6600;\">Asmaa bint \u2019Amru Ummu Manii<\/span>\u00a0 katika Banu Salma. Tukakusanyika katika bonde tukimsubiri Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (<strong>\ufdfa<\/strong>) mpaka alipofika akiwa p\u00e9moja na ammi yake <span style=\"color: #ff6600;\">\u2018Abbas bin Abdl Muttwalib<\/span> na hali ya kuwa bado yu katika dini ya watu wake &#8211; alifanya hivyo kwa sababu alipenda kuhudhuria jambo la mtoto wa ndugu yake, alimthibitisha na alikuwa mtu wa kwanza kuzungumza\ufb01\ufb01i.<\/span><\/p>\n<div>\n<hr \/>\n<\/div>\n<div><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>1) <span style=\"font-size: revert; color: initial;\"><span style=\"color: #ff6600;\">Ibn Hisham, Iuzuu 1, Uk. 440-441<\/span><\/span><\/em><\/span><\/div>\n<div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>*) Arrahiq Al-Makhtuum Uk -265-266<\/em><\/span><\/div>\n<\/div>\n<hr \/>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM Wakati wa msimu wa Hijja katika mwaka wa kumi na tatu wa Utume sawasawa na mwezi wa Juni mwaka 622 C.E. walihudhuria Waislamu zaidi ya sabini kutoka Yathrib kwa madhumuni ya kutekeleza matendo ya Hijja. Walikuja mahujaji wa kutoka huko wakichanganyika na Mushirikina. Waislamu hawa walikuwa wameulizana kati yao (hali ya kuwa wao [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":15476,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[57],"tags":[],"class_list":["post-21305","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-sera-ya-mtume"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/21305","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=21305"}],"version-history":[{"count":3,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/21305\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":21308,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/21305\/revisions\/21308"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/15476"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=21305"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=21305"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=21305"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}